Mkurugenzi Mwakilishi wa shirika la kazi Duniani (ILO) Bw. Alexio Musindo akizungumza kwa niaba ya Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa katika maadhimisho ya miaka 18 ya mauaji ya Kimbari Rwanda leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mwakilishi wa shirika la kazi Duniani (ILO) Bw. Alexio Musindo akizungumza kwa niaba ya Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa katika maadhimisho ya miaka 18 ya mauaji ya Kimbari Rwanda leo jijini Dar es Salaam.Mh. Lambert alisema Serikali ya Rwanda kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania wameweza kufanikisha kwa kiasi kikubwa haki kutendeka kwa watu wa Rwanda kupitia mahakama ya Umoja wa Mataifa huko Arusha.
Msemaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Rwanda Bw. Roland Amoussouga akitoa hotuba yake ya Maendeleo ya Kesi za mauaji ya Kimbari nchini Rwanda katika maadhimisho hayo leo jijini Dar es Salaam. Bw. Roland alisema kati ya kesi 92 za mauaji ya Kimbari 83 zimeshasikilzwa.
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya nchi za nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Mahadhi Juma Maalim akitoa hotuba rasmi ya kuadhimisha Mauaji ya Kimbari na kuwahakikishia Wanyarwanda kwamba Serikali ya Tanzania itaendelea kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Serikali ya Rwanda.
Mh. Zitto Kabwe (wa kwanza kushoto) alikuwa ni miongoni mwa wageni waalikwa.
Mabalozi na wawakilishi mbalimbali wa Umoja wa Mataifa wakifuatilia hotuba ya Mh. Mahadhi Juma Maalim.
Wanafunzi wa shule mbalimbali wakisoma mabango na machapisho mbalimbali ya kumbukumbu ya mauaji ya Rwanda.
Balozi mdogo wa Rwanda nchini Tanzania Mh. Sano Lambert (kushoto) akisalimiana na Msemaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Rwanda Bw. Roland Amoussouga.Katikati ni Afisa habari wa Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari Rwanda Bw. Danford Mpumilwa.
Afisa habari wa Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari Rwanda Bw. Danford Mpumilwa akimuonesha Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya nchi za nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Mahadhi Juma Maalim mabango mbalimbali ya kukumbuka mauaji ya Kimbari ya Rwanda wakati maadhimisho ya miaka 18 ya Kimbari jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...