SSP JOSEPH KONYO  AKIONESHA MOJA YA SILAHA HIZO
 KAIMU KAMANDA KIHENYA KIHENYA AKIWAONESHA WAANDISHI WA HABARI SILAHA MBILI ZA KIVITA AINA YA SMG ZILIZOKAMATWA
 SSP KIHENYA AKIWONESHA WAANDISHI WA HABARI RISASI MBILI ZILIYOKAMATWA PAMOJA NA SILAHA HIZO


Jeshi la polisi mkoa wa kigoma linachukua fursa hii kuwashukuru wananchi waliotoa ushirikiano katika kupambana na uhalifu na wahalifu katika kipindi cha maadhimisho ya sikukuu ya pasaka. sherehe hizo zimeadhimishwa katika hali ya amani na utulivu kwa kuwa hakuna tukio lolote kubwa lililoripotiwa katika mkoa wakati wa maadhimisho ya sherehe za pasaka. sanjari na hayo jeshi la polisi limendelea na operesheni endelevu ya kupambana na uhalifu na wahalifu katika kipindi hiki jumla ya silaha mbili za kivita aina ya smg na risasi mbili zimweza kukamatwa maeneo ya nguruka na mabamba. watuhumiwa wanne wakiwemo raia wawili wa burundi wanashikiliwa  na polisi kwa kumiliki  silaha kinyume cha sheria. sambamba na hayo kumekuwepo na tukio moja la mauaji na tukio la mtu kujinyonga wilaya ya kasulu. maelezo ya matukio hayo ni kama ifuatavyo :-

kupatikana na silaha :-
 Kaimu kamanda Kihenya SSP amesema mnamo tarehe 07/04/2012  katika kitongoji cha Lugongoni kata na tarafa ya Nguruka wilaya ya kigoma mkoa wa kigoma. askari polisi waliwakamata watu wanne Ndolimana Alfred Ndoli, 29, muhutu, mkaazi wa Lutana kiharu nchini Burundi na Matata Chubwa Ntasamba, 36, , mkulima mkaazi wa kijiji cha kitanga Wilaya ya Kasulu.  Ndegeya Medard,  28, mkulima, mkaazi wa kijiji cha kitanga wilaya ya kasuliu mkoa wa kigoma, 4.  Bosco  Yohana Gabriel, 35, Mhutu, mkulima mkaazi wa kibimba giharu nchini burundi wakiwa na silaha ya kivita aina ya smg no. 56 – 2500509 na magazine mbili magazine moja ikiwa na risasi mbili. watuhumiwa watafikishwa mahakamani wakati wowote.
  
Kaimu kamanda amesema katika maeneo ya  mto Ruguzye kijiji  cha Mabamba Wilaya ya Kibondo kufuatia msako dhidi ya uhalifu na wahalifu na wananchi kukubali kutoa ushrikiano kwa jeshi la polisi kupitia falsafa ya polisi jamii na ulinzi shirikishi. Silaha moja ya kivita aina ya SMG ambayo haiwezi kusomeka namba kutokana na kuwa na kutu nyingi ilisalimishwa kwa kutupwa porini na mtu/watu wasiojulikana. Silaha hiyo haikuwa na magazine na mwananchi aliyetoa taarifa za kusalimishwa kwa silaha hiyo ni  mkulima mkaazi wa Mabamba

kujinyonga :-
 Pia kaimu kamanda Kihenya amesema katika kitongoji cha mrusi  kasulu mjini wilaya ya kasulu mkoa wa kigoma. Elizabeth  Kanyungu,  46, mkulima, mkaazi wa seremala kitongoji cha mrusi alijinyonga ndani ya nyumba kwa kutumia kamba ya katani. marehemu alitumia nafasi ya familia yake kwenda kanisani kusali ndipo yeye alibaki peke yake nyumbani na kujinyonga. chanzo cha tukio hilo bado hakijajulikana na uchunguzi unaendelea.

mauaji :-
 Kamanda Kihenya asema tukio la mauaji mnamo tarehe 08/04/2012 majira ya saa sita usiku katika kijiji cha kasangezi wilaya ya Kasulu Mkoa wa Kigoma Zakayo N,  37, mkulima na mkaazi wa kijiji cha Kasangezi aliuawa na wananchi wenye hasira kali wakati akiwa katika ofisi ya mtendaji wa kijiji kwa tuhuma za kuwajeruhi watu saba  Vicent  Mdadili,  mkulima, 30. Linus  Joseph, muha, mkulima, 25. Samson  Rutabina, muha, miaka 45, mkulima, Shukuru Musunu, muha, miaka 30, mkulima 5. kulwa s/o mathias, muha, miaka 27, mkulima. Rashid  Musunu, 35  mkulima na John  Rumie,  55, mkulima wote wakaazi wa kijiji cha kasangezi,   majeruhi wote wamekimbizwa katika hospitali ya wilaya ya Kasulu kwa matibabu zaidi na kati yao majeruhi wawili Samson  Rutabina na Shukuru  Musunu hali zao ni mbaya. chanzo cha mtuhumiwa huyo kuwajeruhi watu ni kutokana na unywaji wa pombe na kuvuta bhangi.

Kamanda  Kihenya amesema jeshi la polisi linawataka wananchi waache kujichukulia sheria mkononi kwa kuwaua wahalifu kwa kuwa kufanya hivyo ni kosa la jinai. wananchi hawana budi kuheshimu mamlaka ya vyombo vya hakijinai. mwisho natoa rai kwa wananchi kuendelea kutoa ushrikiano wa hali na mali kwa jeshi la polisi mkoa wa kigoma katika mikakati yake ya kupambana na uhalifu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Jeshi la polisi Kigoma linastahili pongezi maana kampeni yake ni nzuri na inaonyesha mafanikio mazuri maana kuna watu wengine walisalimisha silaha zao. Pongezi nyingi polis Kigoma NA MKUU WA POLIS KIGOMA. Mmeokoa maisha ya watu wengi maana hizi silaha huenda zingeangamiza maisha ya watu wengi. Wito wangu ni mikoa yote indeleze hili zoezi maana silaha haramu huenda zipo mikononi mwa watu ambao wanahatarisha amani ya taifa letu la amani.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...