MJUMBE wa Kamati ya Utendaji wa klabu ya Young Africans Sports Club,Wakili Theonist Rutashoborwa (pichani) amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya Agha Khan alipokuwa amepelekewa usiku huo mara baada ya kuzidiwa na ugonjwa wa Shinikizo la Damu na Kisukari.

Rutashoborwa alikuwa mjumbe wa kamati ya utendaji wa klabu ya Young Africans toka mwaka 2010,akiingia katika kamati hiyo iliyoingia madarakani katika uchaguzi mkuu wa klabu chini ya uongozi wa Mwenyekiti Llyod Nchunga.

Marehemu amefariki ghafla jana usiku, ikiwa ni mda mchache toka afike uwanja wa ndege wa Mwl. JK Nyerere akitokea Kilimanajaro ambapo siku mbili zilizopita alikuwa jijini Mwanza pia kwa shughuli zake za kikazi za uanasheria.

Msemaji wa familia ya marehemu amesema kuwa mara baada ya kufika uwanja wa ndege wa KIA jana alianza kujisikia vibaya na kulalamika kuishiwa nguvu hivyo mara baada ya kufika uwanja wa ndege wa JK Nyerere alikimbizwa moja moja hospitali ya Agha Khan, ambapo mauti yalimfika.

Marehemu alishiriki kikamilifu shughuli zote za kamati ya utendaji na klabu kwa ujumla, na mara ya mwisho alikuwepo jijini Tanga na timu ya Young Africans wiki mbili zilizopita katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom kati ya wenyeji Coastal Union na Young Africans.

Marehemu ataagwa Jumatatu katika kanisa Katoliki Parokia ya Kijichi,na jioni mwili wa marehemu utasafirishwa kuelekea mjini Bukoba,mazishi yatafanyika siku ya Jumatano katika kijiji cha Bukayaba kilomita 22 kutoka Bukoba mjini.

Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi Amen!

Bwana ametoa na Bwana ametwaa!



Wakati huo huo, Rais Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Mwenyekiti  wa klabu ya mpira wa miguu ya Young Africans Sports Club (Yanga)  Bw. Lyod Nchunga kufuatia kifo cha Mjumbe wake wa Kamati ya Utendaji, wakili Theonist Rutashoborwa, aliyefariki dunia usiku wa kuamkia leo kutokana na ugonjwa wa Shinikizo la Damu na Kisukari.
“Nimepokea kwa Masikitiko na huzuni sana taarifa za wakili Theonist Rutashoborwa kilichotokea usiku wa Kuamkia leo, hili ni pigo na pengo kubwa katika klabu ya Yanga katika kipindi hiki cha kushiriki ligi kuu” Rais amesema.
“Naomba unifikishie rambirambi zangu za dhati kwa familia, wachezaji na wana Yanga wote kwa kuondokewa na Mjumbe wao katika kipindi hiki” Rais ameongeza na kuwataka wana Yanga wawe wavumilivu wakati wa msiba huu na kumuombea Bw. Rutashoborwa mapumziko mema ya Milele.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Mungu ailaze mahala pema peponi roho yako. Tubadilike na kuanza mazoezi na kubadili tunavyokula jamani. RIP

    ReplyDelete
  2. Its true; visukari na BP vimezidi sana kwa sasa; nadhani kuna haja ya kuhamasisha jamii hasa wanaume maana ndio wahanga wakuu, umuhimu wa mazoezi na ku watch diet. Nyama choma na bia kila jioni ni sumu wajameni.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...