Baadhi ya washiriki wa Miss Tabata 2012 wakiwa kwenye pozi.

Na Adam Fungamwango

Mazoezi ya shindano la Miss Tabata yanatarajiwa kuendelea tena kesho (Jumamosi 14,Aprili ) baada ya mapumziko ya sikukuu ya Pasaka.Mratibu wa shindano hilo Joseph Kapinga Kalinga amesema kuwa warembo hao wanatarajia kuanza mazoezi kwenye ukumbi wa Da’ West Park.

Miss Tabata mwaka 2012 mwaka huu inatarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi Mei, ambapo watakaofanya vizuri watapata nafasi ya kushiriki Miss Ilala na kama huko wataendelea kufanya vizuri wanashiriki Miss Tanzania msimu huu.

Kalinga amesema kuwa bado wanatoa nafasi kwa warembo wenye sifa kujitokeza kushiriki.

Amesema kuwa baada ya warembo hayo kuiva kimazoezi, watapata fursa ya kutembelea mbuga za wanyama za Mikumi, pamoja na mikoa mbalimbali nchini ili kujifunza mambo mengi na mazingira pia.

Warembo wanaojiandaa na Miss Tabata ambao watarajia kuanza mazoezi leo ni Neema Saleh (18), Paulina Valentine (18), Khadija Nurdin (19), Phillios Lemi (20), Noela Michael (20), Khadija Ramadhani (18), Axer Peter (20), Rahma Hassan (19) na Mercy Mlay (21).

Wengine ni Neema Innocent (19), Ellen Sule (22), Willihemina Mvungi (20), Queen Issa (20), Suzanne Deodatus (19), Everline Andrew (21), Josephine Peter (20), Nadya Omary (21), Hycalica Joseph (18) na Jamila Omary (19).

Mrembo anayeshikilia taji la Miss Tabata ni Faiza Ally.

Warembo wa Tabata wamekuwa wakifanya vizuri katika mashindano ya Miss Tanzania ambapo mwaka juzi Consolata Lukosi alishinda nafasi ya tatu kabla ya kutangazwa kuwa balozi wa kinywaji cha Redds. Katika shindano la mwaka juzi Julliet William pia alishinda nafasi ya tatu katika ngazi ya taifa.

Michuano ya Miss Tabata huandaliwa na Bob Entertainment na Keen Arts chini ya udhamini wa Konyagi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...