Na Zalha Kassim MCC  
Wananchi wa Zanzibar wametakiwa kushiriki kikamilifu katika Tamasha la Pasaka ambalo linatarajiwa kufanyika April 8 mwaka huu katika ukumbi wa Ngome kongwe mjini Zanzibar.
 Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Tanzania Gospel Music Conceters, Robert Cristopher Bamanisa (ROPRES )katika ukumbi wa habari maelezo Zanzibar wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na Sherehe za Pasaka.
 Ropres amesema lengo kubwa la tamasha hilo la Pasaka ni kuwapa ladha za muziki wa Injili wakazi wa Zanzibar kama ambavyo wanaupata watu wa maeneo mbali mbali duniani.
 Amesema anafahamu kwamba wakaazi wa Zanzibar ni waumini wa dini mbali mbali lakini jambo hilo haliwafanyi kushindwa kushiriki katika Sherehe hizo ambazo ni za kumsifu Mungu.
 Ropres ameongezea kuwa watu wengi wamekuwa wakishiriki katika matamasha mengi ambayo hayaendani na maadili jambo ambalo limekuwa likipelekea mmomonyoko wa maadili katika jamii.
 Ametoa rai kwa wanajamii kumuunga mkono katika harakati zake za muziki huo wa Injili kwani lengo la muziki wao ni kuhamasisha maadili ambayo Mungu anayaridhia.
Aidha ameelezea sababu ya kujiingiza katika muziki huo wa Injili kuwa ni kuahkikisha muziki huo unakuwa na kupokewa vizuri katika Visiwa vya Zanzibar ambavyo ni chemchem isiyo na matabaka.
 Akielezea kuhusu viingilio vya tamasha hilo ambalo litahudhuriwa na wasanii mbalimbali wa Injili Ropres amesema kuwa, kwa watoto wanatakiwa kujitayarisha na Tsh.2000, watu wazima Tsh.3000 na Jukwa la watu maalum Tsh.5000

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Ndugu zangu, wananchi ya zanzibar taasis zinazo husuki, nawaomba kwa kauli moja kataani hizi tamasha za gospel ni hatari kwenu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...