Kutokana na Mvua ya kiaina aina iliyonyesha leo jijini Dar es Salaam,imepelekea eneo hili la Tandika Davies Corner kujaa maji na kupelekea vyombo vya usafi kupita kwa shida katika eneo hilo.
Dereva wa Bodaboda akihandaika kuinasua bodaboda yake mara baada ya kukwama kwenye tope.
Wengine wakihangaika kuhamisha friji.
Mwanadada ambaye alikuwa ametoka gengeni akilazimika kupita kwenye maji machafu yaliyotuama kutokana mvua iliyonyesha leo jijini Dar es Salaam.
NEW YORK YETU HIO MJAMAA
ReplyDeleteMLIOKUWA MAJUU NA MSITHUBUTU KURUDI HUKU NI BALAA HAKI YA MUNGU AFADHALI MFIE HUKO HUKO
hii ni hatari sana kwa afya zetu ,tujaribuni sana kuangalia barabara zetu kujengwa mitaro ya maji yaende ....hapo ni maji ya mvua na makaro yamechanganyika ndio yanatuingia mwilini mwetu, na utasikia ati dar imeendelea magorofa kwa wingi vikwanguwa anga km 5 kutoka kwenye magorofa watu wanalala na maji ya mavi je hayo ni maendeleo ......ni aibu kubwa sana hata kumpeleka mgeni huna njia yakumpitisha ....
ReplyDelete