Baadhi ya waangalizi wa amani wa Umoja wa Mataifa ambao wapo tayari nchi Syria, wakiwa wamezingirwa na wananchi wa Syiria. Hadi mwishoni mwa wiki hii kulikuwa na waangalizi wapatao 14 idadi ambayo haitoshi. Mkuu wa Idara ya Operesheni za Ulinzi wa Amani ya Umoja wa Mataifa Balozi Herve Ladsous ameziomba nchi ambazo zimepelekewa maombi ya kutoa waangalizi wa amani kuwasilisha majina ya maofisa watakaowapendekeza haraka iwezekanavyo. Tanzania ni kati ya nchi zilizoombwa kutoa maafisa wanajeshi kushirikia katika zoezi hilo. Lengo ni kupelekea waangalizi 300 katika kipindi cha siku 90.

Na Mwandishi Maalum

New York

Mkuu Idara ya Operesheni za Ulinzi wa Amani za Umoja wa Mataifa (DPKO) , Balozi Herve Ladsous,ameziomba nchi ambazo zimepelekewa maombi ya kutoa waangalizi wa amani kwenda kuhudumu nchini Syria, kutoa waangalizi hao haraka na mapema iwezekanavyo.

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ni kati ya mataifa ambayo yameombwa kutoa wanajeshi wake.

Balozi Ladsous ametoa wito huo siku ya ijumaa wiki hii, wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na wawakilishi wa nchi ambazo zinashiriki katika Operesheni za ulinzi wa kulinda amani za UN maarufu kama TCC.

Ombi la Balozi Ladsous kwa nchi hizo linakuja ikiwa ni takribani wiki moja tangu Baraza Kuu la Usalama kupitisha Azimio namba 2043 ( 2012) linalotakamka pamoja na mambo mengine, kuanzishwa kwa Misheni ya Umoja wa Mataifa ya kusimamia amani Syria ( UNSMIS) itakayokuwa na waangalizi 300 wanaotakiwa kupelekwa nchi humo ndani ya kipindi cha siku 90 tangu kupitishwa kwa Azimio hilo.

“ Ninawaomba sana sana, tafadhali fanyeni hima, kutupatia waangalizi wa amani, wasilianeni na Makao Makuu ya Nchi zenu. Hatuna muda na dunia inatuangalia”. Akasisitiza na kusihi ombai alilokuwa akirudia mara kwa mara ,Mkuu huyo wa DPKO aliyekuwa ameandama na maafisa waandamizi kutoka Idara hiyo.

Kwa mujibu wa Bw. Herve Ladsous ili Azimio hilo liweze kutekelezwa kikamilifu, waangalizi wa amani 100 wanatakiwa wawe wamewasili nchini Syria ndani ya siku 30 na idadi itakayobakia ya waangalizi 200 iwe imekamilika ndani ya siku 60.

Akasema kwamba ili malengo hayo yaweze kufikiwa kama ilivyopangwa, ni vema na muhimu nchi zilizoombwa zikawasilisha majina ya wanajeshi wanaowapendekeza haraka na mapema iwezekanavyo ili taratibu za maandalizi ya kuwapeleka Syria yaweze kutekelezwa.

Akifafanua zaidi kuhusu majukumu ya waangalizi hao, ambao hawatakuwa na silaha za aina yoyote ile , kuwa jukumu lao kuu la msingi litakuwa ni kufuatilia na kusimamia kwa ukamilifu utekelezaji wa ajenda Sita za mpango wa amani kama zilivyoainishwa na Mjumbe Maalum wa Umoja wa Mataifa na Muungano wa Nchi za Kiarabu, Bw. Kofi Annan.

Mapendekezo hayo yanataka pande zote husika nchini humo kusitisha mapigano na vitendo vyovyote vya uvunjifu wa amani, kuondoa wanajeshi na silaha katika makazi ya watu, kuruhusu mashirika ya misaada ya kibinadamu na hatimaye kuruhusu kuanza mchakato wa mazungumzo ya amani yatakayozingatia matakwa ya watu wa Syria.

Akabainisha kwamba waangalizi hao wa amani 300 watasambazwa katika maeneo 25 ambayo yameainishwa kama maeneo tete yanayohitaji uwepo wa maafisa hao.

Hadi kufikia siku ya ijumaa wiki hii kulikuwa na waangalizi wa amani wapatao 14 ambao wapo tayari nchini Syria kwa lengo la kusimamia mchakato huo wa usitishswaji wa mapigano na uondoaji wa silaha katika makazi ya watu na pia kutoa taarifa ya kile kinachoendelea.

Hata hivyo idadi hiyo ya waangalizi hao imekuwa ikilalamikiwa na wananchi wa Syria kwamba haitoshi ikilinganishwa na ukubwa wat atizo.

Wakati huo huo katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, ametangaza uteuzi wa Meja Jenerali Robert Mood raia wa Norway kuwa Mkuu wa Misheni ya Usimamizi ya Umoja wa Mataifa nchini Syria (UNSMIS)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Syria ni sehemu ya hatari kweli kweli lakini watakaothubutu kwenda watatengeneza dola za kutosha.

    David V

    ReplyDelete
  2. TAFADHALI MSIPELEKE ASKARI WETU KUFA HUKO KWA SABABU HAWA WATU WENYEWE HAWAPENDI MASIHA YAO WANAJIUA HOVYO HOVYO KILA SIKU KWA HIYO WATAWAUA TU WANAJESHI WETU HASA UKIZINGATIA KUWA NI WEUSI. SI MNAKUMBUKA MAREKANI ALIPOENDA KUTAKA KURUDISHA AMANI SOMALIA ILIKUWAJE?

    ReplyDelete
  3. Hawa watu wabaya sana kaka na niwanafiki, wasyemtaka wanamzushia kila jambo ili muradi tu wapate nafasi ya kumtumia jeshi la laki za watu na kumg'oa, inasikitisha yanayotokea sio syria tu mpaka palestine, Myanmar, Somalia lakini kwa kuwa syria ni mtu wao watatoa kila sababu kweli leo wanajeshi 300 wanawashindwa kutoa kwenda huko mpaka watuombe na sie maskini jibu huu umoja wa sote ni mujibu kusaidiana mbona wakienda mission zao na sie hawatuchukui jibu tajiri hazidi kuwa tajiri na maskini hazidi kuwa maskini. Kweli haya ndio walio declare 10/10/1948 kwamba sote ni sawa lakini ukweli si hivyo, Ikumbukwe haya mataifa makubwa karne tatu,nne zilizopita zilikuwa si kitu cha ajabu zaidi mmoja yao lilikuwa linatawaliwa na mengine watu wake walikuwa watumwa lakini leo mungu amewanyanyua imekuwa wao sasa ni wenye kuwadhulumu na kusaidia kuwakandamiza wanyonge, basi ninaamini huko mbele sie tumelala makabulini maskini na yeye hatakuwa mkubwa na hatawawajibisha yule ambaye aliyemfanyia dhiaka wakati hakiwa chini,tunashangaa pengine mambo fulani yanatukuta kwanini pengine sababu ni jambo walilifanya wazee wetu kisha wakasau hivyo leo sisi tunawajibishwa huyo ndio muumba he's very so fair,Sometimes unaona laivu mtu anadhulumiwa ukaamua kureact lakini kabla ya kureact inabidi ufikiri kwanza inawezekana ukireact result yake ni greater consequences rather than not reacting, just hate whatever is been done and pray to god for them and this makes you a better human being than the one who reacted in an aim to restore peace but caused further bloodshed and lost of innocent civilians soles. This is true peace we all know that helping a fellow humanity is a necessity to every one who can but before we decide to send our brave soldiers to syria we should ask ourselves questions about the people who are asking us to do that,what kind of people are they in real sense, what will our participation mean cause who ever sides with an hypocrite he too becomes one intentionally or vice versa thats why when the tsunami comes it takes whatever soul is on the way good or bad, child or old and me and you kaka know what tomorrow is going to happen. This mission looks good on the paper but logically it has complication and consequences and what type of consequences and complications are they only god knows and i believe the person making the last decision is president and he's a muslim so let god be the one who helps you make the final decision not anyone else pray the prayer of guidance(istikhara) and god willing he will show you the way, the way that definitely has no or less complication sand consequences to the people of the united republic of tanzania and its future generation.
    Mungu ibariki Tanzania na watu wake.

    ReplyDelete
  4. Wapinga Muungano Mnaona hii?

    Mkiambiwa Muungano unaleta amani na mshikamano mnakuwa wabishi, tizameni Wananchi wa Syria wanavyomtazama kwa kiu Askari wa Umoja wa Mataifa Mwangalizi wa Amani!

    Mwarabu mnaomtegemea mkivunja Muungano na Bara mmojawapo ni huyu Syria mambo yake ni kama hayo hapo,,,mazito!

    ReplyDelete
  5. THAMANI YA AMANI:

    Mwangalizi wa Amani wa UN anapokelewa a nkushangaliwa na Wananchi wa Syria kama Nabii!

    Wazanzibari na Wana Chadema mnaopenda kuyakoroga mpo hapo?

    ReplyDelete
  6. HII YOTE NI KAZI YA MUISLAELI. KUENEZA FITNA DUNIANI. MUISLAEL ANAPANGA MMAREKANI ANATEKELEZA...AU SIYO??? TUACHE KUPELEKESHWA KAMA GARI BOVU. UBAYA WAO TUWAACHIYE WENYEWE NA SISI TUJIVUNIE NA UMASIKINI WETU ULIOAMBATANA AMANI NA UTULIVU. WAO MATAIFA YA MAGHARIBI WANA SILAHA ZA KISASA WANA MAEXPERTS WAPELEKE WATU WAO.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...