Tanzania imewasilisha Mpango Kazi wake katika Mkutano wa Mwaka wa Wakuu wa Nchi zinazoshiriki katika Mpango wa Ubia wa Uwazi Serikalini (Open Government Partnership) unaoendelea nchini Brazil. Nchi tatu za Afrika (Tanzania, Kenya na Afrika ya Kusini) ni kati ya Nchi 52 zilizowasilisha mipango yao
Mheshimiwa Mathias Chikawe (Mb) Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora) akiwasilisha Mpango Kazi wa Tanzania wa Open Government Partnership ambao umejikita katika kuleta uwazi, uwajibikaji na ufanisi katika maeneo matatu( Afya, Elimu na Maji).
Ushiriki wa Asasi zisizo za Kiserikali ni muhimu katika kuhakikisha malengo ya OGP yanafikiwa. Bw. John Ulanga, Mkurugenzi Mwendeshaji wa Foundation for Civil Society – Tanzania akichangia kuhusu mpango kazi wa Tanzania. Bw. Ulanga alisifu maeneo ambayo Tanzania imejikita katika mpango huo kwa kuwa yanawagusa wananchi moja kwa moja.
Bi. Susan Mlawi, Naibu Katibu Mkuu – IKULU (wa pili kulia) na Bw. Joseph Meza, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakifuatilia kwa makini wakati wa uwasilishwaji wa mpango kazi wa Tanzania.
Wadau kutoka nchi mbalimbali wakisikiliza kwa makini wakati Tanzania inawasilisha Mpango Kazi wake.
Mhe. Chikawe akizungumza na Balozi Kirimi Kaberia, Balozi wa Kenya Nchini Brazil mara baada ya Tanzania, Kenya na Afrika ya Kusini kuwasilisha Mipango kazi yao.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...