Steve Annu, mpiga picha mpya wa Globu ya Jamii, amekamata taswira kadhaa jioni hii kuionesha jinsi mvua kubwa iliyonyesha toka milango ya saa tisa hivi iliyoleta mafuriko sehemu mbalimbali ambazo mitaro yake ina kwikwi.
Taswira hizi ni za Mikocheni kati ya Tanesco na Shoppers Plaza ambako pamekuwa kero kutokana na mitaro yake kutofanyiwa kazi miaka nenda miaka rudi. Wakati huo huo tishio la Tsunami ambalo lilileta wasiwasi kwa wakazi wengi wa jiji la Dar na kwingineko limeinuliwa baada ya tetemeko kubwa huko Indonesia.
Tamko rasmi la Idara ya Hali ya Hewa Tanzania limetolewa Bungeni Dodoma muda mfupi uliopita kuthibitisha kwamba hali imeanza kutengamaa baada ya tishio hilo kupita, na kutoa rai kwamba vyombo vya usafiri majini hususan katika Bahari ya Hindi wasubiri hadi kesho asubuhi kabla ya kuendelea na shughuli zao, na kwamba hakuna habari za madhara ya watu ama mali zao hapa nchini. Globu ya Jamii inafuatilia kwa karibu swala hili
Maji kila mahali
Tutafika tu kwa Kudra zake Mola
Hii sasa balaa
Moka zikivaliwa baada ya kuvuliwa kutokana na mvua
Kufa kufaana
Balaa
Mafuriko
Twende mbele...
Bora kufika salama
Leo kazi ipo
Hii adha hapa Mikocheni itaisha lini toba....
mwe!mwe! hii ni bongo tambarare ya kina ras makunja,kesho ajuae mungu,
ReplyDeleteBongo tambarare
Dah! poleni sana Dar es salaam. Hali inatisha mno.
ReplyDeletehili eneo mikocheni ilibidi liwe wazi hadi milele
ReplyDeleteeneo la kupata chumvi eneo la mabwawa ya chumvi eneo ytangu miaka ya 80's wakati hakuna majumba hayo palikuwa panajaa maji sema kulikuwa na mifereji maji yanaenda baharini
sasa serikali imeruhusu watu kujenga mifereji imezibwa mtategemea nini hapo?
kuvunja waliopewa vibali kwa rushwa ndio solution
Nafikiri wakati umefika kuweka sheria inayokataza mtu mzima kubebwa kuvushwa barabarani kwasababu ya kukwepa maji. Zanzibar baada ya mapinduzi tulipiga marufuku kutumiwa kwa Ma-"rickshaw" kwasababu yanamzalilisha mtu.
ReplyDeletePoor sewage planning
ReplyDelete