Mh Balozi John kijazi akikabidhiwa kombe na timu nzima
NA TANZANREP NEW DELHI
Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania [New Delhi] nchini India wiki hii ulifanya hafla kubwa kusherehea ushindi na kuipongeza Timu ya Mpira wa Miguu ya Ubalozi kwa kunyakua Ubingwa wa Mashindano ya "United Cup 2012" ambayo huzishirikisha Timu za Balozi mbali mbali zilizoko nchini India - Inter Embassies Soccer Tournament.
Timu ya ya Ubalozi wa Tanzania iliibuka kidedea kwa kuifunga Timu ngumu ya Ubalozi wa Botswana magoli 2-0. Mashindano haya yalianza rasmi tarehe 29 Machi na kufikia kilele tarehe 1 Aprili 2012.
Timu ya Ubalozi ilijumuisha Familia za Maafisa wa Ubalozi na Wanafunzi wa Tanzania wanosoma katika Jimbo la Delhi pamoja na Majimbo mengine ya jirani.
Vile vile, Timu ya Ubalozi ilishinda mechi zote za awali kabla ya kufanikiwa kuingia fainali. Timu ya Ubalozi wa Botswana ilichukua nafasi ya pili na nafasi ya tatu ilichukuliwa na Timu ya Ubalozi wa Saudi Arabia.
Balozi nyingine zilizoshiriki katika Mashindano haya ni Denmark, China, Spain, France, Egypt, Saudi Arabia, Indonesia, Netherlands na Israel, United Nations na Timu ya “Touch of Hope Foundation” na wenyeji India.
Mashindano haya huandaliwa "New Delhi United Football Club" kwa kushirikiana na Wadau wengine kwa madhumuni ya kuimarisha urafiki, Ushirikiano, upendo na kujenga afya za washiriki.
Safi sana huu ndio utangazaji halisi wa Nchi yetu naona wahindi walikuwa hawajui Tanzania iko wapi na siku hiyo weng iwao ndio walijua baada ya timu hiyo kuchukuwa kikombe.Hongereni sana Ubalozi na timu nzima kwa ujumla Tangaza Tanzania!!!
ReplyDelete