Wanachama wa UWF wakiwa na baadhi ya washindi wa waliong'ara vizuri kwenye shindano la kumsaka Mwanamke Mjasiliamali,kupitia tuzo ya Mwanamakuka (lililofanyika March 8),na hatimaye kuwapata washindi watano wa tuzo hiyo.(KUONA TUKIO ZIMA LILIVYOFANYIKA BOFYA HAPA).
Meneja Miradi wa UWF,Bi.Mariam Shamo akimkabidhi Bi Nassra Mussa hundi ya shilingi laki tano kwa kuibuka mshindi wa tano wa shindano la Mwanamke Mjasiliamali (tuzo ya Mwanamakuka).Pichani kulia ni Mwenyekiti wa UWF,Bi Mwate Madinda.Hafla hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki kwenye ofisi za UWF zilizopo Mikocheni, jijini Dar
Muwakilishi wa Clouds FM,Abdull Mohamed akimkabidhi Bi.Joyce Mabula hundi ya shilindi laki saba unusu kwa kuibuka mshindi wa nne wa tuzo ya Mwanamke Mjasiliamali (tuzo ya Mwanamakuka).
Baadhi ya Washindi wa shindano la Mwanamke Mjasiliamali kupitia tuzo ya Mwanamakuka wakifuatilia jambo
Meneja Miradi wa UWF,Bi.Mariam Shamo akizungumza machache mbele ya wageni waalikwa waliofika kwenye hafla hiyo,iliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye ofisi za UWF zilizopo Mikocheni, jijini Dar.
Mwenyekiti wa UWF,Bi Mwate Madinda akiwakaribisha wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye hafla hiyo sambamba na wanachama wenyewe wa UWF.
Angalau haya mahela yote ya Wezi Mawaziri Bilioni 550 bora wangemwagiwa hawa akina mama Wajasiriamali nafikri Jamii ingekombolewa!
ReplyDeleteThe THEN MOBITEL Team - nawapenda
ReplyDeletePongezi nyingi kwa kuwainua kina mama. Wanaume tukabaliane; Mwanamke ni nguzo ya maendeleo labda mawaziri wote wangekuwa wanawake kusingekuwa na ufisadi.
ReplyDeleteWadau naona siku hizi watu waweka simu zao juu ya meza kwani vibaka wametosheka na simu siku hizi? Nakumbuka nilifuatwa na mkufu wangu wa dhahabu nawaogopa wale watu acha kabisa!