Wanachama wa UWF wakiwa na baadhi ya washindi wa waliong'ara vizuri kwenye shindano la kumsaka Mwanamke Mjasiliamali,kupitia tuzo ya Mwanamakuka (lililofanyika March 8),na hatimaye kuwapata washindi watano wa tuzo hiyo.(KUONA TUKIO ZIMA LILIVYOFANYIKA BOFYA HAPA).
Meneja Miradi wa UWF,Bi.Mariam Shamo akimkabidhi Bi Nassra Mussa  hundi ya shilingi laki tano kwa kuibuka mshindi wa tano wa shindano la Mwanamke Mjasiliamali (tuzo ya Mwanamakuka).Pichani kulia ni  Mwenyekiti wa UWF,Bi Mwate Madinda.Hafla hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki kwenye ofisi za UWF zilizopo Mikocheni, jijini Dar
Muwakilishi wa Clouds FM,Abdull Mohamed akimkabidhi Bi.Joyce Mabula hundi ya shilindi laki saba unusu kwa kuibuka mshindi wa nne wa tuzo ya Mwanamke Mjasiliamali (tuzo ya Mwanamakuka). 
Baadhi ya Washindi wa shindano la Mwanamke Mjasiliamali kupitia tuzo ya Mwanamakuka wakifuatilia jambo
Meneja Miradi wa UWF,Bi.Mariam Shamo akizungumza machache mbele ya wageni waalikwa waliofika kwenye hafla hiyo,iliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye ofisi za UWF zilizopo Mikocheni, jijini Dar.
Mwenyekiti wa UWF,Bi Mwate Madinda akiwakaribisha wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye hafla hiyo sambamba na wanachama wenyewe wa UWF.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Angalau haya mahela yote ya Wezi Mawaziri Bilioni 550 bora wangemwagiwa hawa akina mama Wajasiriamali nafikri Jamii ingekombolewa!

    ReplyDelete
  2. The THEN MOBITEL Team - nawapenda

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 01, 2012

    Pongezi nyingi kwa kuwainua kina mama. Wanaume tukabaliane; Mwanamke ni nguzo ya maendeleo labda mawaziri wote wangekuwa wanawake kusingekuwa na ufisadi.
    Wadau naona siku hizi watu waweka simu zao juu ya meza kwani vibaka wametosheka na simu siku hizi? Nakumbuka nilifuatwa na mkufu wangu wa dhahabu nawaogopa wale watu acha kabisa!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...