Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Ezekiel Maige akizungumza wakati akizindua Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Utalii nchini TTB alioufanya Aprili 04,2012 jini Dar es Salaam  katika jengo la Mpingo makao makuu ya Wizara ya Maliasili na Utalii. kulia kwako ni Mwenyekiti wa bodi hiyo Balozi Charles Sanga na anayefuatia ni Mkurugenzi  Mwendeshaji wa TTB Dkt Alloyce Nziku ambaye ni Katibu wa bodi hiyo na Mhe. Abdulkarim Shah Mbunge wa Mafia ambaye pia ni mjumbe wa bodi hiyo.
  Balozi Charles Sanga akisikilizwa na Waziri Maige na Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Bibi Maimuna Tarishi
Wajumbe wa Bodi Mpya ya Utalii wakiwa katika Picha ya Pamoja na Mhe. Waziri , Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu Bibi Nuru Millao mara baada ya bodi yao kuzinduliwa rasmi jijini Dar es salaam
Kupata hotuba ya Waziri Maige BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Ankal uwiano wa kijinsia kwa wajumbe wa bodi umekaaje?? Mhe Maige apo vipi?

    ReplyDelete
  2. DUUH!! KWELI ANONI YAANI HAKUNA MJUMBE WA KIKE ATA MMOJA. MAMA TARISHI NA MAMA MILLAO HAO NI WATENDAJI AU SIYO?? APA MHE MAIGE AMECHEMSHA..

    ReplyDelete
  3. Teddy mapunda ni mjumbe kwa taarifa yenyu nyie wadau hapo juu. ila mi nauliza wanapatikanaje hawa na siye wakina nanihii tuombe?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...