Na Mary Ayo,Arusha


VYUO Vikuu Afrika Mashariki vimetakiwa kuwafunduisha wanafunzi wao mafunzo ya ujasiliamali na masomo yanaoendana na mahitaji ya soko la ajira la Afrika Mashariki.


Wito huo ulitolewa na mwenyekiti wa Umoja wa Waajiri Afrika Mashariki, Jackline Mugo kwenye uzinduzi rasmi wa umoja huo uliofanyika jijini hapa mwishoni mwa wiki.


Alisema waajiri wengi katika ukanda wa Afrika mashariki wanakumbana na changamoto nyingi ikiwemo kutopata wafanyakazi walioiva kwenye maeneo yao ya kazi.


“Hii ni moja tu ya changamoto nyingi tunazokumbana nazo katika utendaji wetu wa kila siku kama waajiri na hivyo tunaamini kupitia mwamvuli huu tutaweza kukaa pamoja kama waajiri na wadau wengine kupata suluhisho la matatizo yetu.” Alisema Mugo.




“Wanafunzo wanaomaliza vyuo wanatakiwa kuivishwa vya kutosha kabla ya kuingia kwenye soko la ajira,” alisema na kuongeza: “Waajiri wanamchango mkubwa kwenye kuimarisha mtangamano wa Afrika Mashariki kutokana na mchango wao katika nchi wananchama.”


“Kupitia mwamvuli huu, tunaweza kuishauri serikali juu ya namna ya kuboresha mambo mbalimbali ili kukuza na kudumisha mtangamano wetu.”


Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri Afrika Mashariki, Musa Sirma alilipongeza jukwaa la waajiri kwa kuja na mkakati wao wa namna ya kudumisha mtangamano wa Afrika Mashariki.


Sirma ambaye ni Waziri wa masuala ya Jumuiya ya Afrika Mashariki nchini Kenya alisema jukwaa hilo limekuja katika wakati muafaka ambapo jumuiya inatekeleza itifaki ya soko la pamoja.


Alisema jumuiya itafanya kila linalowezekana kuhakikisha kuwa waajiri wanafanya kazi yao katika mazingira bora na hatmaye kudumisha mtangamano.


Alisema waajiri ni sekta muhimu katika jumuiya kwa kuwa wao ni waajiri wakubwa wa watu wa Afrika mashariki na kulipa kodi mbalimbali zinazozifanya nchi zetu kujiendesha.


Umoja huo wa waajiri ulianzishwa mwaka 2010 kwa lengo la kukuza uzalishaji na kuongeza ushindani wa kibishara Afrika Mashariki.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Ni wazo zuri sana lakini bado tuko mbali sana katika kufikia hilo.Kwanza kuna vituo vya ajira,TZ ina "labour exchange bureau"lakini kazi zake hazijaainishwa na sioni kama inafanya kazi yoyote.Ulimwenguni kote hakuna chuo kinachofundisha kazi ila baada ya masomo vituo kama labour exchange hufanya kazi za kutrain wahitimu na hii hugharamiwa na serikali na baada ya training vituo hivi hutafutia wahitimu kazi kulingana na offer zilizoko kuliko kmwachia mhitimu ahangaike mwenyewe,nadhani ingekua busara kuanza kufanyia kazi mfumo huu.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 01, 2012

    La muhimu ni kuwapa ukweli kuwa Mamlaka haiwezi kumhakikishia Ajira kila Mhitimu.

    Pia wasijenge imani kwamba kuwa na Shahada au Stashahada haikuhakikishii ya kuwa wewe ni Bosi na kuwa kazi kama kufyaua matofali, kuuza Genge na ukulima wa mobgamboga, na biashara ndogondogo sio stahili kwako.

    Ukweli ni kuwa Jamii zilizopiga hatua kimaendeleo Duniani zimekuwa zikitilia mkazo sana kwa kujiairi kwenye Sekta za Biashara ndogondogo Binafsi(SME) na Sekta ya Mzingo wa chini ktk Jamii (Grassroot)

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...