Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Isongole, Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya wamelazimika kufunga barabara kuu ya Mbeya/Tukuyu kwa masaa manne kuanzia saa 4 asubuhi mpaka 8 mchana, kufuatia kifo cha mwanafunzi mwenzao wa kidato cha pili marehemu Nuru Patrick, baada ya kugongwa na gari ya abiria aina ya Coaster na kufariki papo hapo majira ya saa 1 asubuhi, Aprili 17 mwaka huu.
Wanafunzi hao wakiwa wameshika mabango yenye ujumbe ulioandikwa "Matuta kwanza tumechoka kupoteza ndugu zetu" kufuatkia kifo cha mwanafunzi mwenzao wa kidato cha pili marehemu Nuru Patrick, baada ya kugongwa na gari ya abiria aina ya Coaster na kufariki papo hapo majira ya saa 1 asubuhi, Aprili 17 mwaka huu katika barabara kuu ya Mbeya/Tukuyu.
Mkuu wa Usalama wa barabarani Wilaya ya Rungwe BL Lihwa akimsikiliza Kiranja wa Taaluma katika shule ya Sekondari Isongole Charles Nyingi (26), muda mfupi baada ya ajali kutokea ambapo amesema zaidi ya wanafunzi 15 katika shule za msingi na sekondari Kijijini hapo wamefariki dunia baada ya kugongwa na magari kutokana na mwendokasi hivyo ameomba kuwekwa kivuko na usalama wa barabarani ili kudhibiti mwendokasi wa madereva unaosababisha ajali.
 Mkuu wa Usalama wa Barabarani BL Lihwa akiwasihi wanafunzi kuliachia gari la kusafirishia wagonjwa baada ya kufunga barabara kuu ya Mbeya/Tukuyu kwa masaa manne kuanzia saa 4 asubuhi mpaka 8 mchana, kufuatia kifo cha mwanafunzi mwenzao wa kidato cha pili marehemu Nuru Patrick, baada ya kugongwa na gari ya abiria aina ya Coaster na kufariki papo hapo majira ya saa 1 asubuhi, Aprili 17 mwaka huu.
Gari la wagonjwa ikiwa imezuiwa kupita baada ya wanafunzi kufunga barabara kuu ya Mbeya/Tukuyu kwa masaa manne kuanzia saa 4 asubuhi mpaka 8 mchana, kufuatia kifo cha mwanafunzi mwenzao wa kidato cha pili marehemu Nuru Patrick, baada ya kugongwa na gari ya abiria aina ya Coaster na kufariki papo hapo majira ya saa 1 asubuhi, Aprili 17 mwaka huu.
Jeshi la Polisi lililazimika kutumia mabomu ya machozi ili kuwatawanya wanafunzi hao baada ya kufunga barabara kuu ya Mbeya/Tukuyu kwa masaa manne kuanzia saa 4 asubuhi mpaka 8 mchana, kufuatia kifo cha mwanafunzi mwenzao wa kidato cha pili marehemu Nuru Patrick, baada ya kugongwa na gari ya abiria aina ya Coaster na kufariki papo hapo majira ya saa 1 asubuhi, Aprili 17 mwaka huu.
 Sehemu ya wanafunzi wakiwa na bango lililoamdikwa ujumbe huu "Matuta kwanza tumechoka kuwapoteza ndugu zetu.
Wanafunzi wakiwa wameanza kufunga barabara kuu ya Mbeya/Tukuyu kwa masaa manne kuanzia saa 4 asubuhi mpaka 8 mchana, kufuatia kifo cha mwanafunzi mwenzao wa kidato cha pili marehemu Nuru Patrick, baada ya kugongwa na gari ya abiria aina ya Coaster na kufariki papo hapo majira ya saa 1 asubuhi, Aprili 17 mwaka huu.
(Picha zote na Mdau Ezekiel Kamanga wa Mbeya Yetu Blog.).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. hii kali and sound good, hawa wanafunzi wachaguliwe kuwa wabunge wanamawazo mazuri kuliko wabunge au wakuu wa mikoa

    ReplyDelete
  2. duh kiranja ana miaka 26? hii ni sekondari au college?

    ReplyDelete
  3. yaani kiranja wa taaluma ana miaka 26? au nimekosea kidogo hapo?

    ReplyDelete
  4. Kwanza pole kwa wazazi,ndugu,jamaa na Marafiki wa Nuru.

    Nje ya Mada:Tukuyu nilikfika mara moja mwaka 1995,kuna baridi sana hali ya hewa murua..Picha zinapendesha kwenye backbground..mawingu meusiiiiiiii ,vegetation..evergreen.Nitarudi tena.

    Sijaendesha kupitia barabara hii lakini barabara kubwa nyingi za Tanzania zina alama za shule..Tatizo ni ule uendeshaji wetu wa kutokusoma hata alama za barabarani..Matuta=Ok

    David V

    ReplyDelete
  5. Poleni sana kwa msiba huo. Hongereni wanafunzi kwa uamuzi wenu wa kuweza kumuenzi marehemu kwa kuomba matuta yajengwe. Hii ni haki yenu na watanzania wote. Inasikitisha sana kwa vifo vingi ambavyo vingweza kuepukwa lakini vinatokea kwenye ajali. Mwenyazi mungu awape moyo wa uvumilivu.

    ReplyDelete
  6. They did the right thing, uzembe wa madereva unasababisha maafa mengi sana nchini na hakuna hatua za maana zinazochukuliwa. Mbona polisi wasitupe hayo mabomu kwa hao madereva?!! ALUTA CONTINUA!!

    ReplyDelete
  7. Ndugu yangu usishangae miaka 26 ni secondary. kumbuka watu wengi tanzania bado wanasoma wakubwa hasa vijijini. Ila mjini kidogo ndio utaona watu wanaenda na miaka ila wengi pia wanapunguza.

    ReplyDelete
  8. Tunajenga taifa gani jamani? Badala ya kufuata sheria na kanuni zilizopo tunaunga mkono vitendo vya kihalifu kama hivi kwa kisa cha haki. Hivi matuta ndio suluhisho? Nina hakika matuta si suluhisho la kudumu ni budi watu wetu wakaelimishwa vya kutosha juu ya matumizi ya barabara na sheria zake badala ya kushindikiza kupatiwa vitu visivyo na tija.

    ReplyDelete
  9. muschi b.c.April 19, 2012

    Kwanza poleni wote mliopoteza ndugu, jamaa, watoto, wajukuu na hata mali na mifugo yenu. Kama serekali inaona matuta ni gharama basi awepo askari trafiki akiwavusha watoto hapo! mbona mnawapendelea wa mijini tu?
    Pole sana mzee patrick kwa kumpoteza binti yako wa kidato cha Pili. Mungu akupe nguvu na uwezo wa kuvumilia uchungu huo ulioupata

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...