Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na wabunge, John Mnyika wa Ubungo (kushoto), Kabwe Zitto wa Kigoma Kaskazini  na Hamad Rashid wa Wawi, kwenye jengo la Utawala la Bunge Mjini Dodoma Aprili 21, 2012. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. PINDA:
    Ndugu zangu, nina mke na watoto ambao bado ni wadogo, hivyo tuhurumiane jamani.. nawaomba sana ndugu zangu msinimwagie ugali.

    WAPINZANI: .......mmh!!!

    ReplyDelete
  2. Mtanzania halisiApril 21, 2012

    Naona Mh.Rashid anawapoza vijana. Hii ndiyo tafsiri yangu kutokana na muongozo wa picha hapo juu. "Jamani sikilizeni tuliyotaka kufanyika yameshatokea wenzetu wameamuwa kujiuzulu. Sasa hili swala la sahihi naona tuliache kwa sasa ili tupate ya kuwashuhurikia hawa mabwana waliyojiuzuru ipasavyo. Maana hii haishii hapa hata kidogo. Tumpeni Waziri mkuu ushirikiano afanye yale tuliyoyaazimia"

    Mh.Rashid acha magirini Pinda lazima aondoke, tunataka viongozi shupavu wenye kuchukua maamuzi magumu hata kama hayana faida kwao. Au yatawaweka kwenye mazingira magumu kwa muda mfupi lakini yakayoletea faida kubwa na ya muda mrefu kwa Taifa letu changa na maskini, Tanzania. Hivi mtu na akili zako unaweza kweli kwenda pale mjini halafu ukampora au kumwibia wale ombaomba wanajikusanyia visenti ili mradi apate mkake wa kila siku. Hii inawaingia kweli akilini wale wanaowatetea hawa jamaa.

    Uongozi ni wito hajalizishwa mtu kama huwezi achia, hatutaki waziri mkuu pambo, tunataka awe mtendaji mwenye kufanya maamuzi ya kiuongozi.Wao ndio walikuchagua uwe kiongozi wao iweje ushindwe kufanya maamuzi. Basi kama ikiwa hivyo kuna ulakini hapo wa sifa zake za uongozi.

    Na ukimwangalia Mh. Pinda kwenye sura yake inasema kabisa hapa nimechemsha. Lakini swali amejifunza nini kutokana na hili tunamwachia mwenyewe?

    Zitto na Mnyika msikubali kurubuniwa mkilegea hapo na nyie nitawatilia mashaka kuwa ni wababaishaji. Mtizameni Mh.Pinda kwenye sura yake na mwambieni mzee umechemsha na hili linakughalimu, tunaamini iko siku utapata fursa ya kuwa kiongozi tena na utajifunza kutokana na hili.

    Tutapigana kwa umoja kuhusu hili kama watanzania na wala si itikadi za vyama vyenu. Mimi sina chama ila nitapigana kuona mali ya Tanzania inalindwa.

    I can see why ile fedha ya Rada Waingereza walikuwa wanakataa kuwapa japo yenu sababu hamuaminiki nyie. Ukishakuwa waziri tu unafungua akaunti nje ya nchi.

    ReplyDelete
  3. jamaa anaonekana anafaa kuwa rais so humble anaponzwa na watendaji

    ReplyDelete
  4. JAMANI HAO MAWAZIRI MBONA VING'ANG'A?

    ReplyDelete
  5. Do yaani baba wa watu anatia huruma kwa kweli. Hii mifisadi inamaliza nguvu sana. Lakini ndio mambo ya uongozi ndio ukubwa huo.

    ReplyDelete
  6. Haya ndiyo madhara yatokanayo na Katiba iliyopo sasa.Waziri Mkuu yupo yupo tu lakini hana madaraka ya kuwatimua Mawaziri walio chini yake kwasababu hakuwateua yeye,japo ni Kiranja wao!mpaka awasiliane na Bwana Mkubwa wake,akubali,ndipo WM atamke, so and so wamejiuzulu nyadhifa zao!Lakini Waziri Mkuu kwa tafsiri sahihi ya cheo hicho alipaswa kuwa na mamlaka ya kuwatimua mawaziri hao bila ya kusubiri mradi tu apate ushahidi wa kutosha wa kile kinachodaiwa kutendwa na mawaziri hao na akajiridhisha kwamba kweli hii ni kashfa ambayo itaweza kuhatarisha "serikali yake",japo sote tunajua ni serikali ya Rais!Pole sana Baba!

    ReplyDelete
  7. Anony Sat Apr 21, 11:56:00 PM 2012-Well said.Liangaliwe hili kwenye Katiba mpya..ndiyo maana Mawaziri wanakuja na jeuri kwa WM,wanamdharau hadi mkuu wao awapigie simu za kujiuzulu...rubbish

    David V

    ReplyDelete
  8. Pinda for presidency 2015. You have my vote

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...