Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando akitangaza  kuongeka kwa  zawadi ya  hadi Tsh 143 m/-katika promosheni ya Nani Mkali itakayoendelea kwa muda wa miezi miwili zaidi, kulia ni Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Dangio Kaniki akifuatilia wakati wa mkutano wa waandishi wa habari (hawapo pichani) Ili kushiriki promosheni andika  neno “Mkali” tuma kwenda  15656 bure. Baada ya hapo atatumiwa maswali na kila atakapo toa jibu sahihi atapata pointi 20 na jibu lisilo sahihi pointi 10.Kila ujumbe wenye jibu utatozwa shillingi 350 pamoja na kodi. 
kulia ni Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Dangio Kaniki akifafanua jambo  wakati wa mkutano wa waandishi wa habari (hawapo pichani) jinsi ya kushiriki promosheni  ya Nani Mkali iliyoongezwa muda andika  neno “Mkali” tuma kwenda  15656 bure. Baada ya hapo atatumiwa maswali na kila atakapo toa jibu sahihi atapata pointi 20 na jibu lisilo sahihi pointi 10.Kila ujumbe wenye jibu utatozwa shillingi 350 pamoja na kodi. Toka shoto ni Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando. 

====  ====== ======
Airtel yaongeza zawadi ya Tsh 143 m/-katika promosheni ya Nani Mkali 

·         Promosheni ya Nani Mkali kuendedelea kwa miezi miwili


30, May 2012 Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imeongeza muda kwa wateja wake kuendelea kucheza promosheni yake kabambe ya Nani mkali ambayo ilianza miezi mitatu iliyopita na kuwafaidisha zaidi ya wateja 90 wa Airtel waliojishindia jumla ya miliono 217 kwa mgawanyo wa kuanzia milioni 1 kila siku, milioni 3 kila wiki na milioni 30 kwa washindi wa mwezi

Akiongea na waandishi wa habari leo Meneja uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando alisema promosheni hii imekuwa na faida kwetu Airtel wateja wetu waliokuwa wakishiriki wameifurahia na ndio maana leo tumeamua kuongeza zawadi na muda wa promosheni ya Nani Mkali

Hivyo promosheni yetu inaongezwa muda wa miezi miwili huku zawadi zitakazo toka ni pesa taslim Jumla ya ya shilingi milioni 143 katika mgawanyo wa kuanzia shilingi  milioni 1 kila siku-washindi 52, milioni 3 kila wiki –washindi 7,na milioni 30 kwa kila mwezi  itatoka kwa washindi 2.

Pia tutakuwa na washindi wengine watakaogawana kitita cha shilingi milioni 10 za zaidi ikiwa watakuwa kati ya wachezaji bora wa promosheni ya Nani mkali

Ili mteja kushiriki na kujishindia zawadi hizi kabambe Afisa Mawasiliano wa Airtel bi Dangio Kaniki alisema,” kudhihirisha kauli mbiu yetu ya jisikie huru katika promosheni hii mteja anatakiwa kuandika neno “Mkali” na kutuma kwenye namba 15656 bure kabisa ili kujiunga. Baada ya hapo atatumiwa maswali na kila atakapo toa jibu sahihi atapata pointi 20 na jibu lisilo sahihi pointi 10.Kila ujumbe wenye jibu utatozwa shillingi 350 pamoja na kodi.

Promosheni hii pia itatoa fursa kwa wateja kuchagua lugha wanayotaka kwa kutuma neno “swa” kwa Kiswahili au “eng” kwa lugha ya kiingereza kwenda namba 15595 Kujua alama ulizonazo au point mteja wetu atatakia kutuma neno “point” au “alama” kupatiwa pointi alizojikusanyia. Kujiondoa kwenye promosheni mteja atatakiwa kutuma neno “cancel’ au “stop” kwenda namba 15595

Promosheni ya nani mkali ilizinduliwa rasmi februari 15, 2012 na kudumu kwa muda wa miezi mitatu.Nani Mkali imefanikiwa kuwazawadia wateja wa Airtel kutoa mikoa mbali mbali ikiwemo Arusha, Muheza Tanga and DSM, Tabora, Dodoma, Mwanza, Mbeya, Iringa, Kilimanjaroa na mingine mingi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 30, 2012

    BARUA YA UCHUMBA KWA DANGIO KANIKI:

    HODI HODI TANGA:

    Salamu sana ama baada ya salaam mimi sijambo.
    nazituma kutokea mbali nia na azma nimekuwa nikitoa kilio changu kupitia kwa Mdau mwendeshaji Ankal Michuzi lakini salamu hazifiki.

    Nimechukua fursa hii kwa kuiweka kalamu mkononi na kuandika kwa jinsi Bibie DANGIO KANIKI ambavyo amekuwa akiijeruhi nafsi yangu!

    Mjomba wangu Michuzi anashuhudia hapa jinsi kiumbe mimi ninavyoumia kutokana na kiumbe mwenzangu Dangio Kaniki alivyojaaliwa.

    Mtoto ana macho matamu na usho wa bashasha, kiasi kwamba nikimpata itabidi niombe Likizo au Ofisi yangu niihamishie Nyumbani nifanyie kazi zangu kutokea nyumbani.

    Na yeye nitajitahidi kama ataacha kazi Airtel nitaangalia njia nyingine kama tufanye kazi ya pamoja ili niweze kujihami na WADOKOZI KAMA MDAU MWENYE WAKE WAWILI ALIVYOLALAMIKA LEO HUMU JAMVINI KUWA ANAPIGIWA MIZIGO YAKE MIWILI.

    Naomba mtamke kama ni ndege nitatafuta Mkopo ninunue, kama ni ghorofa pia nitaangalia uwezekano wa kupapatia ili niweze kuwatimizia nanyi mnikabidhi Binti wenu Dangio Kaniki.

    Natanguliza Shukrani.

    Mdau wa Blogu ya Jamii

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 30, 2012

    Ahhh Ankal,

    Nilishaomba contact zake ukaniweka kapuni,

    Nilisha lalamika mara kwa mara ya kuwa huyu kiumbe wa Airtel Dangio Kaniki ananijeruhi nafsi yangu!

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 30, 2012

    kwa kweli huyu mdada ni mzurii mnooooo, kama amolewa duh hongera mkaka, yaani nitahamia Airtel coz of her! vip bibi kavishe kaishia wapi?

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 30, 2012

    I dont think if this is the right forum, unaweza fika ofisi za airtel kuuliza namba zake za simu. Huku tunahitaji mambo ya kimsingi ya kutujenga zaidi inakoelekea sasa hii blog itakuwa kama ileeee nyingineeee ambayo hata kuitembelea siku hizi sina hamu walianza hivi hivi now it is so boring, mwenye blog kuwa makini, kuna vitu vya kujenga tunapost hauvirushi am suprised to see all these ??

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...