Mtangazaji wa kipindi cha Power Break Fast cha Radio Clouds 88.4 Fm,Said Bonge akipanda Mgomba katikati ya Barabara ya Mwananyamala usoni kabisa mwa lango kuu la kuingilia kwenye Hospitali ya Mwananyamala.Mtangazaji huyo amefikia hatua hiyo kutokana na uwepo wa mashimo makubwa na ya muda mrefu kwenye barabara hiyo ambayo yamekuwa ni kero kubwa kwa watumiaji wa barabara hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 21 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 18, 2012

    Good idea, kwa barabara zote ingekuwa hivi.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 18, 2012

    Hayo mashimo hata mgomba haufai, angepanda mbuyu kumaliza kabisa udhia. Hata wadau wengine wafanye hivyo ktk barabara nyingine labda mamlaka zitastuka!!!

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 18, 2012

    Ila kweli, ladba hii inawezakuwa jinsi nzuri ya matumizi ya barabara zetu. Kwani hapo gari halipiti na kuna shimo zuri, sasa kwa nini lisitumike?

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 18, 2012

    .....HAHAHAHAAAA....! BONGE NJOO NA HUKU MTAA WA UHURU. HUKU NJOO NA MBUYU KABISA MAANA HAYA SIO MASHIMO NI MAHANDAKI HAYA

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 18, 2012

    YAANI BONGE SIJUI NIKUPE ZAWADI GANI,LAKINI NGOJA NIENDE BKB SI AIR TZ INAFANYA KAZI?NILETE MIGOMBA MINGI,UPANDE JIJI ZIMA TUTAKULIPA.UWEZI FANYA KAZI BILA MALIPO.
    MDAU BONGO.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 18, 2012

    SAFI SANAA BONGE! Tafuta migomba mingine uende ukapande na kule KIJITONYAMA NA MIKOCHENI. BONGE NIFIKISHIE SALAMU HII KWA MH MAGUFULI.

    Hii ni salamu kwake Mh. Magufuli na watendaji wake wote kwenye Wizara ya Ujenzi.

    Hii barabara ni muhimu sana kwa wakazi WOTE wa Bagamoyo road kwani wengi tunaitumia.

    Mh. Magufuli, barabara hizi zinazojengwa kwa fedha za ROAD FUND ni AIBU KUBWA.

    Kwa mfano :

    (1) Hii barabara ya kuelekea Hospitali ya Mwananyamala huu ni mwaka wa 16 toka nianze kuitumia HAIJAWAHI HATA SIKU MOJA KUKOSA SHIMO/MASHIMO YA KUTOSHA. Kwa mfano juzi nimeshuhudia Mark II ilingia kwenye shimo kubwa mpaka ikazima huku ikiwa na mgonjwa hoi ndani yake, dreva ameshuka akijaribu kuisukuma wakati hapo ilipokuwa ni mita chache kuingia ndani ya hospitali.

    (2) Haya barabara za Kijitonyama ndiyo usiseme, maana ni kiungo KIKUBWA NA MUHIMU kwa wakazi wa wengi, lakini barabara hizi hazitamaniki. Ilikwisha tangazwa kwenye vyombo vya habari kuwa zitafanyiwa matengenezo lakini mpaka sasa ni moja tu nayo ni barabara ya Kachube Road, ambayo nayo niliona kibao kuwa imejengwa kwa fedha za ROAD FUND. Duh! imechakachuliwa kiasi cha kuwa ‘BIG G’ kwa sasa nayo hata mwaka bado imeshaharibika ina mashimo.

    (3) Barabara nyingine ambayo nayo hatuelewi ni kwanini haitengenezwi ni ile ya kutoka Kijitonyama kuelekea AFRIKA SANA, nayo ina maandaki ya kutosha. Tena hii kutwa utaona wakandarasi wanashindilia na vifusi wakati ni barabara ya miaka tele.

    Mh. Huu ni wakati wa kufanyakazi na kuwawajibisha watendaji wako. Kwa mfano mimi ni mfuatiliaji wa barabara nyingi zijengwazo.

    Mh. kuna ujenzi wa aina Fulani hivi ambao unaendelea hizi sasa, utakuta wajenzi wetu wanamwaga vifusi vingi na kushindilia. Kisha wanamwaga uji wa rami halafu wanamwaga kokoto ndogondogo nyeusi halafu wanamwagia tena ule uji kidogo na kupitisha shindilia tena basi, barabara tayari. Nimeyaona haya barabara ya Yombo Vituka, Magomeni Kagera na pande za Kijitonyama. Sasa vile vikokoto vilivyogoma kushika kwenye rami unakuta vinawarukia wapitanjia ni HATARI SANA.

    Mh. Kuna barabara moja mpya ingawaje ni nyembamba inakatiza maeneo ya Mwananyamala kuelekea HOMBUS – Biafra kwa kweli naomba nichukue fulsa hii kumpongeza mjenzi yule. Kwanza, alifuata step zote katika ujenzi wake mitalo na matoleo ameyasindikiza vizuri, pili alitumia PAVER kumwaga rami, tatu ameweka MATUTA barabarani na nne ameweka TAA. Sasa ukitoka hapo inatakiwa ije ikutane na ile ya Kijitonyama, MWEE! Yaani huko unafikia kwanza kwenye MAANDAKI (njia zote tatu ziingiazo Kijitonyama kutokea kwa mama Zakaria HAZIFAI) ndipo uje uianze barabara ya ‘BIG G’ halafu tena MAANDAKI YA AFRIKA SANA kuelekea Mwenge.

    Mh. Naomba ufuatilie huku hata leo utayaona mambo hayo, Fedha za walipa Kodi zinaliwa na wachache.

    ReplyDelete
  7. Mimi binafsi naona amewakilisha mawazo yake ambayo c mabaya ni njia nzuri tuu ya kutoa dukuduku,sasa sijui sheria zinasemaje maaana tusije tukamsifia hapa,baadaye kumbe sheria inasema vingine akajikuta yupo segerea,then waosha vinywa wote hapo watakua pole,dooooh jamani !huku unateseka.big up anyway.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 18, 2012

    Hongera sana bonge,Tunataka wanahabari kama wewe wanaoweza kuisaidia jamii,Hii inaweza kuleta mabadiliko Ni aibu sana kwa barabara mhimu kama hiyo inafikia hatua manispaa kusituliwa kwa kupanda mgomba.

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 18, 2012

    Mdau, ni mahandaki, sio maandaki.
    Ni Lami, sio rami...... Sawa mkuu???
    Tunaelemishani tu, usishtuke, au siyo?

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 18, 2012

    Naomba hili zoezi liwe endelevu, very impressive indeed! Need I say more!!!? Over!

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 18, 2012

    barabara ya Kachube Road .... sheng - Swahili english, tehe tehe.
    Barabara ya morogoro road, nk.

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 18, 2012

    Bongeeee!!! WE MKARRRRIII!

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 18, 2012

    KAKA MICHUZI HATA OLD BAGAMOYO ROAD KARIBU NA SUPRMARKET MOJA KUNA SHIMO LINALOZIDI KUKUA SIKU HADI SIKU.NASHANGAA HUKO WANAISHI WAKUBWA WENGI ILA SHIMO SIJUI HAWALIONI.HII NI TANZANIA ZAIDI YA UIJUAVYO

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 18, 2012

    Lakini nyie mnalipa kodi TZ kweli au mnakosoa tu

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 18, 2012

    Bonge big up sana. Tafadhali bonge kama utasoma hizi comment nipatie namba yako nakutafuta sana tena sana kwa kazi ya maeneo ya kwetu, siwezi kukuambia kwa sasa ila tukiwasiliana nitakujuza kinachoendelea. Mdau 0756554055 / 0786 554055

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 18, 2012

    Ni ubunifu mzuri na ni ujumbe tosha kwa watendaji wetu.

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 18, 2012

    Labda tuvunje baraza la mawaziri tena.Tuwaweke walipa kodi maana "siri ya mtungi auijuae maji" Au pengine watafurahi waanze kujirudishie za kwao mapema LOL!

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 18, 2012

    System mbaya.. Huku Canada budget inayotokana na Property tax ndiyo inayotengeneza ma barabara. Kwa mfano kwa mwaka kukarabati barabara zote za eneo la Sinza ni milioni 20 na kuna nyumba 2000 ina maana kila mwenye nyumba atalipa shilingi 10,000. Na Meya (mfano) wa eneo anawajibika kila mwaka kutoa mehasabu wazi kwa wakazi wake jinsi pesa zilivyotumika katika kufanyia ukarabati. Nafikiri umefika wakati wa wakazi wa eneo kumili haya mabarabara na wawe wakali na siyo kila kitu kutegemea Serikali kwa kila kitu. Neyere alisema madaraka M ikoani na vijijini. Tuige jinsi wenzetu wanavyofanya.

    ReplyDelete
  19. Big up, it needs a brave man to do what u have done, keep it up but you are going to be a very busy body shortly.
    I salute ur creactivity.
    sasa huo ni mshale au matoke les us know we will keep an eye, tukumbukane siku ya mavuno

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 18, 2012

    Bonge!!! Poa sana mwana kama una mgomba uliobakisha basi upeleke pale feri mbele ya soko la samaki shimo tayari lipo bado kupanda tu!! Hii ndio bongo ukistaajabu ya Musa basi utayaona ya Tanzaniaaaaa .. tehe tehe tehe eeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee. I love this country bwana!!

    ReplyDelete
  21. AnonymousMay 19, 2012

    Tatizo watu wa Dar es salaam mnajipendelea sana, ingawa serikali imejitahidi kujenga barabara kila uchochoro wa Jiji hilo sisi wa mikoani barabara zetu nyingi ni za vumbi tumetulia lakini nyie ni wa kwanza kuisema hamna hata shukurani hebu njooni huku Rukwa muone tuna kipande tu cha lami nyie kelele na kejeli, hebu Manispaa ziacheni wapate hata miembe tuone.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...