Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Ijumaa, Mei 4, 2012, amemteua Bibi Saada Mkuya Salum kuwa Mbunge katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Uteuzi huo unaanza mara moja.
Rais amefanya uteuzi huo kwa mamlaka aliyo nayo chini ya Ibara ya 66 (i) (e) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, kama ilivyorekebishwa.
Chini ya Ibara hiyo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anapewa mamlaka ya kuteua wabunge 10 kuingia katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mpaka sasa, Rais Kikwete ameteua wabunge saba. Novemba mwaka 2010, aliteua wabunge watatu na jana, Alhamisi, Mei 3, 2012 ameteua wabunge wengine watatu ambao ni Professa Sospeter Muhongo, Bibi Janet Mbene na Bwana James Mbatia.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
4 Mei, 2012
Katiba inamruhusu Raisi kuteua Wabunge 10.
ReplyDeleteMwaka 2010 Novemba aliteua Wabunge 7, halafu 2012 Mei, 3 wengine Wabunge 3, halafu tena leo Bibi. Saada Mkuya Salum,
Sasa wanakuwa 7+3+1=11
Ameteua Wabunge 11 badala ya 10 hapa inakuwa vipi?
Amestuka kuwa aliwasahau vibarakashie wenzie!!
ReplyDeleteHIKI NI KATI YA VIFUNGU VINAVYOTAKIWA KUFUTWA KTK KATIBA
ReplyDeleteFanyeni haraka mkuu keshamaliza kazi Ikulu..
ReplyDeleteDavid V
Hatimaye James Mbatia amepata ujira wake, kwani anafanya kazi nzuri sana ya CCM kule Upinzani.
ReplyDeleteWewe ulikuja total 11 soma habari vizuri usikurupuke ka mkojo wa asubuhi
ReplyDeleteAmevunja katiba, tutamfanyahe huyu mkuu wa kaya? 7+3+1=11
ReplyDeleteWewe mdau wa kwanza wacha uzushi.
ReplyDeleteKabla aliteuwa wabunge watatu (Meghji, Shamsi na Mnyaa), juzi watatu (Mbatia, Muhongwa? na Janet) na jana mmoja (Sada).
Piga jumla ya darasa la kwanza mwenyewe.
Hao 11 umewatoa wapi? Au amekuchagua wewe hatukupewa taarifa?