Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Afya,katika utekelezaji wa mpango wa kazi za Wizara hiyo huko Ikulu Mjini Zanzibar leo.Kushoto ni Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar,Maalim Seif Sharif Hamad.
Baadhi ya watendaji wa Idara mbali mbali za Wizara ya Afya,wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,alipokuwa akizungumza nao katika mpango wake wa kuzungumza na kila Wizara katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja. [Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
Kuna haja ya kutahmaini, jee kuna mabadiliko katika utendaji wa Serikali baada ya Mikutano hii!!
ReplyDeleteWizara yako hii mheshimiwa ndio imeoza. Mgonjwa amepata ajali anawaambia madaktari msinifunge p.o.p nina sukari, wao wanakaidi matokeo yake donda linakua kubwa mpaka linaoza. Yuko Muhimbili ingawa na huko hali kadhalika lakini watu kidogo makini angalau penye udhia unapenyeza rupia. Eeh Chadema wenyewe wanaosema watapiga rushwa mpaka tone la mwisho sijui watapigaje vita hii ya manesi na wauguzi wengine kudai pesa ya chai baada ya kukuhudumia. Ukifikwa ndio unajua tatizo na huthubutu kusema.
ReplyDelete