Mashindano ya urembo ya Redds Miss Tanzania yameanza kushika kasi baada ya hatua ya awali, ngazi ya vitongoji maeneo mbalimbali kufikia fainali zao kuanzia mwisho wa wiki hii.

Akithibitisha kufanyika kwa fainali hizo za Redds Miss Tanzania, ngazi ya vitongoji Meneja wa kinywaji cha Redds Bi Victoria Kimaro amesema; ni kweli mchakato umepamba moto hivi sasa, kwani vitongoji vingi vitakuwa vikifanya fainali zake kuanzia mwisho wa wiki hii. 

Kama wadhamini wakuu wa Redds Miss Tanzania tayari tumekwisha fanya mawasiliano na vitongoji vyote husika ili kuhakikisha kuwa kila kitu kinakwenda kama ilivyopangwa. Tuna hakika mashindano ya Redds Miss Tanzania mwaka huu yatakuwa na msisimko wa aina yake, maana waandaaji wamefanya kazi nzuri ya kupata warembo wenye sifa na wanaokidhi vigezo.

Akiyataja maeneo yanayotarajiwa kufanya fainali zake mwishoni mwa wiki na siku chache zijazo, Afisa habari wa kamati ya Miss Tanzania Bw Hidan Ricco amesema; vitongoji hivyo na tarehe zao ni kama ifuatavyo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...