MBONI YANGU.Wimbo huu ni maalum kwa ndugu yetu msanii Sajuki ambae anahitaji mchango wako wako wa hali na mali kuokoa maisha yake.Kabla sikupenda kuweka picha yake hapa katika hali aliyonayo sasa ila imebidi ili upate picha kamili.


Sajuki anasumbuliwa na uvimbe tumboni na mwezi huu anahitajika kusafiri kwenda nchini India kwa matibabu.Wimbo tuliokuwa tunaurekodi unatoka katika filamu aliyowahi kuifanya na mkwewe ya MBONI YANGU.Na wimbo huu upo ndani ya filamu hiyo aliuimba Wastara.


Wimbo huu tumeurekodi kuhamasishana kuchangia na utaanza kusikika kesho katika radio ya clouds fm na video ya tukio zima la kurekodi itaonekana clouds tv.Na kesho tutahakikisha tunakusanya angalau 
Tsh ml 12,000,000 hapa clouds fm


.Nakuomba sana mtanzania mwenzangu tushirikiane katika hili.
- DINA MARIOS

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 05, 2012

    urafiki na mapenzi ya kweli ni sasa jamani.
    tusiwe wanafiki na washabiki wa mambo.kutoa ni moyo.
    tumsaidie ndugu yetu.
    "it begins with me"


    mdau znz

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...