Moja ya hospitali kongwe yenye huduma ya kusifika ya mkoani Mbeya, Hospitali ya Igogwe, itaadhimisha Jubilei ya Almasi (a.k.a Diamond Jubilee, yaani miaka 50) toka ianzishwe- tarehe 18 Oktoba 2012. Kamati hii ya maandalizi ya maadhimisho hayo (pichani) ilikutana jana kwa mara ya kwanza kwenye ukumbi wa mikutano hospitalini hapo wilayani Rungwe.
Kamati hiyo iliyojumuisha wadau mbalimbali iliazimia kuchangisha fedha miongoni mwa wajumbe wake, baada ya hospitali na wafanyakazi wake kuchangia jumla ya shilingi milioni saba, na vile vile ilidhamiria kuwashirikisha wadau wa maendeleo wengine katika kufanikisha shughuli mbali mbali za Jubilei hiyo. Wasomaji wa Michuzi Blog ni miongoni wa wadau wa kwanza kabisa kuhabarishwa kuhusu maadhimisho haya na kuhamasishwa kupitia taarifa hii kushiriki kwa hali na mali. Taarifa zaidi zitaendelea kutolewa kupitia blogu hii na vyombo vingine vya habari siku za usoni.
Kamati hiyo ilikutana chini ya mwenyekiti wake Fakilly M Haule. Viongozi wengine wa kamati hii ni Japhet M Kalindu (katibu), Freddy Katoto (mhasibu) Isaac Mtwanga (makamu mwenyekiti) na Faraja Mwalwega (Katibu Msaidizi).
Hospitali hii inamilikiwa na Kanisa Katoliki Tanzania na kutoa huduma kwa Watanzania wote na inawashirikisha wadau mbalimabli katika maendeleo yake.
Hongera sana Igogwe Hospital. Tunajivunia kuwepo kwako, na tunashukuru kwa kunusuru maisha yetu sisi wana Rungwe, wana Mbeya na Ntebela.
ReplyDeleteNinawapongeza uongozi na wafanyakazi wote wa Igogwe. Nimeguswa sana na jambo hilo. Mtoto wangu mmoja alizaliwa hapo Igogwe na wakati wa maadhimisho atakuwa na miaka 32. Ningependa kutoa mchango wangu kama mdau aliyenufaika na huduma za hospitali hiyo. Mimi pamoja na mtoto wangu huyo hatupo nchini kwa sasa. Tafadhali tujulishe zaidi jinsi tunavyoweza kuwasiliana na wahusika. Nashauri mngeweka contacts kama vile e-mail address au simu kwenye hii blog.
ReplyDeleteMbarikiwe sana kwa kazi nzuri mnayoifanya.
Nashukuru sana kusikia mwanao alizaliwa hapa. Mimi ninayesema haya ni Afisa Tawala Hospitali. Jumamosi tulikuwa na Harambee na kufanikiwa kukusanya zaidi ya Tshs 25,000,000 kwa ajili ya ukarabati wa hospitali na kituo cha watoto Yatima. Waweza kuwasiliana nami +255754885261 na mchango wako waweza kuwakilisha NBC Tawi la Tukuyu account Na.038201127120 Jina la akaunti ni IGOGWE HOSPITAL - JUBILEE AU AKAUNTI NA. 61403500064 NMB TAWI LA TUKUYU. TUNATANGULIZA SHUKRANI KWA MCHANGO WAKO
ReplyDelete