Hayati Munga Tehenan
Kwa wadau wote wapenda Elimu ya Saikrojia wale na waliokuwa wapenzi wa Gazeti la JITAMBUE, ni miaka minne sasa imepita tangu mwanasaikrojia na mwandishi Mahiri wa vitabu Tanzania Hayati Munga Tehenan afariki Dunia tarehe Mei 5, 2012.

Familia pamoja na mke wa Hayati Munga Tehenan na wana FAJI, wanafanya kumbukumbu ya kifo cha MUNGA TEHENAN. Shughuli hiyo inafanyika katika msikiti wa BAITUL MUQAEAS Kibo Kimara na sadaka ya chakula itatolewa katika ofisi za Faji Kimara Rombo.

Tunamkumbuka mwalimu huyu aliyefundisha masomo ya utambuzi na kusaidia wengie waliokataa kutoka na matatizo ya kisaikrojia ikiwa maradhi leo tunamkumbuka kutokana na mchango wake katika jamii inatupasa kukumbuka na kuenzi yale yote aliyotenda kwa jamii.

Munga alifundisha njia mbalimbali ikiwa kupitia katika Gazeti la Jitambue, vipindi vya Televisheni vilivyorushwa kupitia kituo cha TBC 1 wakati huo ikijulikana kama TVT.

Wanao Kilonzo, Nuru, Rajab na mkeo Salma wanakukumbuka wanajitambue wote wanakukumbuka tutaenzi kazi zako, elimu yako pamoja na upendo uliotuonyesha na tunakumbuka kwa kusema maneno yako haya.

"Elimu hii ya Utambuzi imezidi kuenea sana dunia na kuna watu ambao wamebombea sana katika elimu ya Utambuzi lakini kujua si kutenda, ukijitambua fanya mazoezi kukabiliana na maisha ya mazoea, kwani mtu akijitambua jamii umuona ni mtu wa ajabu kutokana na Mazoea," MUNGA TEHENAN

"Fedha si kila kitu, kama fedha ni kila kitu? Kabla ya fedha jamii iliishije? Matumizi ya fedha yameanza miaka 2000 iliyopita," Munga Tehenan.

Soma vitabu na makala zilizoandikwa na mwanasaikrojia Munga Tehenan ili uwe huru katika maisha. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 06, 2012

    Ni SAIKOLOJIA na sio SAIKROJIA.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 06, 2012

    jamani RIP. Munga. Nilikuwa mpenzi mkubwa wa makala zake Niko nje ya nchi sikujua kama alishaaga dunia. Kweli hapa duniani tunapita tu. Pumzika kwa amani Kaka.

    Mdau nje ya nchi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...