Home
Unlabelled
Maandalizi ya Barabara ya Mabasi yaendayo Kasi Jijini Dar yaanza kupamba moto
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
kuna yeyote anaeweza kunieleza ni nini hasa "mabasi yaendayo kasi"? na kwa nini yawekewe sehemu yao peke yao? jee mabasi yaliopo sasa nayo yataruhusiwa kutumia barabara hizi?
ReplyDeleteHaya mabasi kwa lugha nyingine ni Eurostar zile zenye mwendo kasi.
ReplyDeletewewe tembea uone sehemu zote duniani mabasi ya abilia hupewa nafasi ya kwanza , kwanza kuwawahisha wafanyakazi makazini na kuwarudisha majumbani haraka na salama -hawa ni walipa kodi-kuna njia zinaitwa express way na hutumiwa na mabasi tu au na gari ndogo ambazo zina watu ndani zaidi ya mmoja, hii inapunguza msongamano wa magari na kuwashauri wale wenye magari madogo kuchukua na wenzao. Kingine , mashimo yooote haya ambayo mpaka raia wema wanapanda migomba barabarani, tuvuteni subira jamani, yote yatakwisha haya, tuna waziri ambaye halali, na pia ni kwamba , sasa technolojia imezagaa-wapigeni picha hao wakandarasi mazishi wanaomwaga vifusi halafu wanafunika na rangi nyeusi kutudanganya kwamba wameweka LAMI-tumieni camera zenu za viganja kuwaumbua hawa watu,tuwasaidieni hawa mawaziri wetu-la sivyo tutawafukuza kazi kila siku-kweli kabisa wengi wa mawaziri wetu ni MAFISADI, hiyo na ikubali 100% lakini siyo wote !!! MAGOMENI sasa hivi, itakuwa kama DUBAI, hongera Magufuli-ngwana wane. Ngwana Zebedayo mna Badugu.
ReplyDeleteMungu jalia huu mradi uishe mapema lakini kuna sehemu pale kimara mwisho inaonekana hawa ndugu zetu wa Tanesco kama hawataki mradi wetu uishe mapema sababu hawatoi nguzo za umeme ili mradi uishe kwa wakati,tunawaomba sana waziondoe nguzo mapema zinaweza kuanguka ikwa issue nyingine,wahusika wazitoe mapema mradi wetu uishe mapema
ReplyDeleteKwanini wasianzishe train ambazo zitabeba watu wengi kama nchi nyingine?
ReplyDeletesababu ni rahisi hazitumii mafuta mengi/au zitumie umeme.
Ofcourse, kuwepo njia ya mabasi (public transport) ni utaratibu wa nchi nyingi sana zilizoendelea. Ndo maana utakuta nchi za wenzetu, watu wanaacha magari yao nyumbani na kupanda mabasi/treni. Kwanza unapunguza gharama lakini pia unawahi kufika unakokwenda. Lakini kwetu sisi ni siasa tu kwa wingi. Maana hakuna haja ya kusema 'mabasi yaendayo kwa kasi', wangesema tu mabasi ya abiria (jina maarufu daladala)
ReplyDeleteLabda kama wana-mpango mabasi hayo yatembee zaidi ya 80 km/hr (yaani zaidi ya maximum speed inaoruhusiwa kwa sasa hapa kwetu Tanzania). Hapo neno 'kasi' itabidi kutumika.
Ndg. Wilson Mukama, HONGERA SANA. I was skeptical that the project was not gonna take off. Hayawi hayawi, yameanza kuwa. I hope it will reduce the mass transit problems in Dar es Salaam.
ReplyDeleteMnamaanisha nini hiyo barabara ya mabasi yaendayo kasi? Ina maana itakuwa ni barabara ya hayo mabasi tu peke yake au......? Mana hata huko kwa 'wenzetu' kwenye 'motorway' mnajichanganya nyote, cha msingi ni kuzingatia 'speed limit' na matumizi sahihi ya alama na sheria husika zilizowekwa kwenye barabara hizo kuzifuata vilivyo, hakuna cha mabasi yaendayo kasi wala yanayotambaa. Sasa hii yetu si ndio itazidi kuchangia ongezeko la ajali barabarani na hasa kwa baadhi ya hawa madereva wetu wazembe (Mwenyeez Mungu atunusuru kwa hilo).
ReplyDeletewadau wengi wanachanganywa na neno KASI, haya ni mabasi yaendayo kasi kwa mantiki kuwa yana barabara zao ambazo magari mengine hayaruhusiwi kupita , hivyo haya mabasi hayatakua na foleni na kuyafnya ya haraka, hayana maana ya speed 120 kwa saa au 80 kama mdau aliposema hapo juu, ni mabasi ya kawaida na speed ni ya kawaida uharaka wake upo pale ambapo haliingiliwi barabara yake na magari mengine, basi, kwa kizungu ni BRT= BUS RAPID TRANSIT, y ajiji letu la dar itajulikana kama DART= DAR ES SALAAM RAPID TRANSIT, hivyo wadau mkumbuke sio speed hapo, na BRT lanes zikikamilika msilazimishe kuendesha huko, myaachie mabsi hayo, ili tuwahi kazini na tuwahi home pia
ReplyDelete