Na Mary Ayo
MADAKTARI wametakiwa kuwa waaminifu kwa kuwa baadhi yao si wahaminifu hasa kwenye ugawaji wa madawa haliambayo inasababisha kila mara vituo vya afya kukosa madawa kwa ajili ya matunizi ya binadamu.
Hayo yameelezwa jijini hapa na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Bw Elasto Mbwilo wakati akifungua semina kwa wadau wa sekta hiyo ya afya kutoka mikoa ya Kilimanjaro na Tanga.
Aidha Bw Elasto alisema kuwa kwa sasa kuna vituo vingi vya afya ambavyo vinakabiliwa na uhaba wa madawa wakati tayari serikali imeshapeleka madawa hayo kwa ajili ya matumizi bora.
Alifafanua kuwa hata kwa wadau wa sekta hiyo ambao wana biashara za uuzaji wa madawa nao wanatakiwa kujua na kutambua kuwa wanatakiwa kutumikia umma na wala sio biashara zao binafsi kama wanavyofanya.
‘leo utakuta daktari ana duka lake la kuuza dawa au huduma ya afya sisi kama sisi hatumnyimi ila afanye kwa muda ambao si wakazi na pia hawa madkatari wanatakiwa wahakikishe kuwa madawa yanayokuja yanakuja
na kufikia malengo na wala sio kupotea kwa madawa kila mara’aliongeza Bw Elasto.
Aliwataka wadau wa sekta hiyo wanakuwa na mbinu mbadala za kuweza kuwasaidia wananchi kwa kuhakikisha kuwa wanaboresha mbinu za utaalamu wa sekta hiyo ya afya kwa kulinda madawa ambayo yanatoka katika bohari kuu ya madawa hapa nchini.
Awali Mkurugenzi wa bohari ya madawa (MSD) Bw Slyvester Matandiko alisema kuwa endapo kama madaktari hao watakuwa na uzalendo wa kweli wa kazi yao basi wataweza kusaidia sana jamii hasa kwenye changamoto ya upotevu wa madawa.
Bw Matandiko aliongeza kuwa changamoto hiyo ya uhaba wa madawa katika vituo mbalimbali vya afya imekuwa ni kikwazo kikubwa sana na walengwa ambao ni Madaktari hasa katika ngazi ya Halmashauri pamoja na Bohari wanatakiwa kujiuliza juu ya changamoto hiyo ya upotevu wa madawa kila mara.
Aliongeza kuwa katika zoezi la utoaji wa dawa mikoa 10 ndiyo inayopata huduma hiyo ya dawa kutoka katika bohari ya madawa wakati mikoa mingine iliyosalia inafikishwa kwa waganga wa ngazi za wilaya hivyo
nao wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanatatua changamoto hiyo ya upotevu wa madawa
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...