Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,akiwahutubia wageni waalikwa na wanachama wa CCM, waliohudhuria katika hafla ya uzinduzi wa vitabu viwili vya Binadamu na Kazi na Ukweli kwa mujibu wa Biblia, na Kurani Tukufu,Suna za Mtume na Sheria za nchi, vilivyotungwa na Katibu Mkuu Mstaafu wa Chama cha Mapinduzi CCM, Yusuph Makamba. Hafla hiyo imefanyika leo katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, imefanyika sambamba na hafla ya kumpongeza kwa kuitumikia nafasi yake ya Katibu Mkuu wa CCM hadi anastaafu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,akionyesha Kitabu cha Ukweli kwa Mujibu wa Biblia, Kuran Tukufu, Suna za Mtume na Sheria za Nchi, baada ya kukizindua kitabu hicho kilichotungwa na Katibu Mkuu Mstaafu wa Chama cha Mapinduzi CCM, Yusuph Makamba (kulia) wakati ya uzinduzi huo uliofanyika kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo,sambamba na hafla ya kumpongeza kwa kuitumikia nafasi yake ya Katibu Mkuu wa CCM hadi anastaafu. Kushoto ni Mke wa katibu huyo, Mama Makamba.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,akizungumza jambo na Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM, Yusuph Makamba, wakati wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa vitabu vya Ukweli kwa Mujibu wa Biblia, Kuran Tukufu, Suna za Mtume na Sheria za Nchi na Binadam na kazi,vilivyotungwa na Katibu huyo. Uzinduzi huo umefanyika leo kwenye Ukumbi wa Karimjee Dar es Salaam.
Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria hafla hiyo.Picha na Muhidin Sufiani-OMR.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 27, 2012

    Badala ya kutatua matatizo na kuzungumzia huo udini unaoendelea huko zanziba mna zindua vitabu mnaacha mambo ya usalama wa nchi

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 28, 2012

    Zanzibar hakuna udini isipokuwa wamechoka kudhulumiwa na Tanganyika, kwa usupi tunataka haki ya nchi yetu, na hivi sasa hao viongozi wa serikali zote(SMT na GNU)hawataki kutusikiliza na kutoa hiyo haki yetu.

    ReplyDelete
  3. Mwangwitwa ChrisMay 28, 2012

    Wewe anonymous wa pili sasa ktk kudai haki zenu kufanya vurugu kanisani kunakuja vipi ktk madai yenu?ina maana watanganyika ndio wapo kanisani hakuna wazanzibar wakristu?wewe waelimishe wenzako ktk madai yenu hakuna haja ya kufanya vurugu kanisani,msipende kuiga mambo ya nchi nyingine,mkumbuke huku Bara tunao ndugu zenu wengi sana wanaishi huku kwa dhana ya muungano wana utajiri wa haja lakini hakuna mtu yeyote anayewafuata ni maisha mazuri na tunaheshimiana kwa kwenda mbele,ninachoamini ninyi wachache mnafanya vurugu hamjawahi kufika huku bara muone wenzenu tunavyoishi kwa amani na upendo waulizenu hao ndugu zenu wanaoishi huku wawaambie maisha yalivyo matamu,acheni ujinga wa namna hiyo,sasa hivi kuna tume ya katiba ya maoni pelekeni maoni yenu mtasikilizwa nini mnataka kuhusu huu Muungano,wewe anonymous wa pili nimekupa hiyo kazi ya kuwaelimisha hao wenzako juu ya hizo vurugu zenu

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 28, 2012

    We Anonymous wa pili nonesense kweli. you need to grow up you think and act a child

    ReplyDelete
  5. Huwa nin msemo wangu ninaopenda sana kuutumia, ambao ni huu hapa; Kutunza amani uliyo nayo ni rahisi sana kuliko kutafuta amani iliyopotea ambayo gharama nyingi hutumika kama umwagaji wa damu na uharibifu wa mali. Mungu atusaidie. Kutafuta amani sio kumwaga damu jamani tuelimishane ndugu zetu

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 28, 2012

    Wakristo tuweni macho na hii tabia ya udini. Angekuwa askofu, padri au mchungaji kaandika chochote kuhusu uisilamu au kurhani pasingetosha hapa mjini. Jamani tuacheni ni imani zetu hakuna kufundishana au kurekebishana. Charity start at home. Je huko misikitini kukoje mpaka mtu aingie kanisani na kwenye biblia?

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 28, 2012

    Mbona huu mkutano wa makamba nao umekaa kidini sana?

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 28, 2012

    Hawa Mabwege wa Zanzibari tuuvunje Muungano ili waende wakaungane na Mwarabu wanayemtegemea ambaye yeye Mwarabu mwenyewe kwake yupo maji ya shingo kwa misala na majanga mawili haya (2)

    1.Ana maandamano ya Mapinduzi na Machafuko ya 'Arab Spring'.

    2.Huku akiwa amefilisika 'Kifedha na Kiuchumi' (WORLD FINACIAL AND ECONOMIC CRISIS) sambamba na nchi za Magharibi anazoshirikiana nazo ktk Uchumi wa Mafuta na Masoko ya Hisa.

    HAWA MABWEGE WAZANZIBARI TUUVUNJE MUUNGANO ILI TUONE KAMA MSAADA WA MWARABU WATAUPATA KWA MAZINGIRA HALISI KAMA HAPO JUU NO.1 NA NO.2?

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 28, 2012

    i hate Tanzania now and its because ya huyo mwenye nyumba.. udini umezidi na hamfiki kokote labad muanze kwenda shule hata mkienda kwakuwa majumbani mwenu hamkufundishwa busara na hekima basi ni bure tupu.. kwani hicho kitabu ni cha dini ama upuuzi tu1mh huyo mwenye kitabu namstahi

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 28, 2012

    siasa ni mbaya na chafu sana watu wanauwana zanzibar huko wakati huku shughuli zinaendelea kama kawaida na hakuna hata anaefatilia shida za wananchi

    ndio maana wanataka nchi yao maana mnawaonea kikweli yani ni dharau za hali ya juu na uwazi kabisa utasema hakuna kinachoendelea huko zanzibar

    mungu atawahukumu.

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 28, 2012

    Wewe anony wa pili,jaribu kuelimika,
    Unaposema Zanzibar hakuna Udini,bali mnadai haki ,haki hipi? ya kuvunja muungano? sasa inausiana vipi ?kuchoma nyumba za ibada za dini zingine?
    Mimi ni Muislam mwenzio,nakuelezea lazima ujue nini? maana ya Islam (dini ya amani) lazima uwe muumini unayependa na kuidumisha amani,maana ya Uislamu ni kujisalimisha kwa mwenyezi Mungu(Mola),
    Sasa kama ni madai ya haki,mbona tahasisi ya kidini ndiyo inayoshawishi kuandamana na fujo,ambazo zimeleta maafa na hasara.
    Kwa huu Muungano si uliasisiwa na viongozi wa bara na visiwani kwa vikao,katiba na mikataba ? kwa nini?basi zisitumiwe njia hizi hizi katika kuuvunja au kuudumisha muungano

    ReplyDelete
  12. sijui kinachoendelea sasahivi zanzibar ila ninavyojua always kunawachache wanaotaka kuiharibia dini ya uislam kama watu sijui wanadai haki zao au wameamua kufanya vurugu why wengine walachome kanisa , kawaida lazima wachache wajitokeze waiharibie dini ya uislam wakati dini inasema uislam sio dini ya vurugu ila cha kuchangaza waumini wake wengine wanapenda vurugu ,

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 28, 2012

    Hakuna sababu ya kulazimisha ndoa,

    Hao Wazanzibari waende zao kwao na Wabara waliopo huko warudi huku.

    HAKUNA KITU KIGUMU KAMA KUMBEMBELEZA MTU KWA SUALA AMBALO YEYE MUHUSIKA ANANUFAIKA NALO (MUUNGANO)

    HII KITU '''MUUNGANO''' BARA INAPATA HASARA SANA KWA KUIBEBA ZANZIBARI.

    NI KUWA WAZENJI NI GOI GOI NA WANADEKA SANA WANATAKA KILA MMOJA APEWE HUDUMA ZOTE ZA MAISHA (KULA, KULALA NA KUVAA) NA SERIKALI !, KITU AMBACHO HATA SERIKALI YA MAREKANI HAIWEZI!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...