Mchezaji kutoka Chuo cha St.John cha Dodoma, Obiara Anyoti akicheza dhidi ya mpinzani wake Kweka John (hayupo pichani) wakati wa mashindano ya Safari Higher Learning Pool Competition yanayoendelea Mkoani Iringa.
Mchezaji kutoka Chuo cha Ushirika Moshi (MUCCOBS), Kweka John akicheza dhidi ya mpinzani wake Obiara Anyoti (hayupo pichani) wakati wa mashindano ya Safari Higher Learning Pool Competition yanayoendelea Mkoani Iringa.
Wachezaji wakishindana kulagi wakati wa mashindano ya Safari Higher Learning Pool Competition Mkoani Iringa.

Na Ripota Wetu,Iringa

AFISA Utamaduni Manispaa ya Iringa,Carlos Mbinga amewataka Watanzania kuupokea mchezo wa pool kwa mikono miwili kutokana na kwamba hivi sasa umekuwa ni sehemu ya ajira kwa vijana na hivyo kufuta zana ya kuwa ni mchezo wa kihuni.

Mbinga aliyasema hayo wakati alipokuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa fainali za taifa za mashindano ya pool kwa wanafunzi wa vyuo vikuuu vinane kutoka katika mikoa minane ya Tanzania Bara,uliofanyika Mkoani Iringa jana.

Mbinga ambaye alimwakilisha mkuu wa mkoa wa Iringa katika ufunguzi wa mashindano hayo yanayodhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager, alisema kuwa mchezo wa pool ni kati ya michezo ambayo kwa sasa inatakiwa kuungwa mkono na Watanzania wote.

Alisema kuwa wana kila sababu ya kujivunia kwa wadhamini wa mchezo huo bia ya Safari Lager kuamua kuleta fainali hizo mkoani hapa kutokana kwamba ujio huo umeweza kuongeza kipato kupitia kwenye biashara mbalimbali zinazofanyika.

"Napenda kuwashukuru Safari Lager kwa kuweza kuleta fainali hizi mkoani hapa kutokana na kwamba wafanyabiashara mbalimbali wameweza kujiongezea kipato kupitia fainali hizi,"alisema Mbinga.

Naye mwenyekiri wa chama cha mchezo wa pool Tanzania (TAPA) Fredy Mushi alisema kuwa kila mwaka mashindano hayo yanazidi kukua zaidi kutokana na uwezo unaoonyeshwa na wachezaji wa vyuo vyote.

Mushi alisema kuwa kila mwaka unaonyesha kuwa na mabadiliko makubwa katika mashindano hayo kutokana na kila chuo kuonekana kujiandaa vizuri na hivyo upinzani kuzidi kuongezeka.

"Ninavyoona upinzani wa fainali za mwaka huu kwa wachezaji kuonyesha viwango vya kutisha, mabingwa watetezi chuo cha IFM kutokana Dar es salaam wazitegemee mteremko maana kila chuo kinaonekana kujiandaa kutwaa ubingwa wa mashindano hayo,.'alisema Mushi.

Mratibu wa fainali hizo, Peter Zacharia (Kosovo), alisema kuwa maandalizi kwa ajili ya fainali hizo yameenda vizuri ikiwemo usafiri, malazi na kila kitu kinachohusiana na fmashindano.

Zacharia alisema kuwa timu zote zimewasili mkoani hapa bila matatizo yoyote na kupokelewa na mamia ya wakazi wa Iringa kwa furaha na nderemo.

Fainali hizo zinashirikisha vyuo vikuu vinane ambavyo vilifanikiwa kuwa mabingwa kwenye mikoa yao katika ngazi ya mikoa ya mashindano hayo.

Vyuo hivyo ikiwa ni pamoja na mikoa vinakotoka ikiwa kwenye mabano kuwa ni mabingwa watetezi IFM (Dar es Salaam), RUCO (Iringa), TIA (Mbeya), IAA (Arusha),St John's (Dodoma),MUCCOBS (Kilimanjaro),St Agustine (Mwanza) na Mzumbe (Morogoro).

Bingwa wa fainali hizo kwa timu ataondoka na kitita cha fedha taslim Sh.Mil.2.5, mshindi wa pili Sh.Mil.1.5, mshindi wa tatu Sh.Mil.1.3 na mshindi wa nne Sh.Mil.1.

Kwa upande wa mchezaji mmoja mmoja wanaume bingwa atazawadiwa Sh.300,000, mshindi wa pili Sh.200,000, mshindi wa tatu Sh.150,000 na mshindi wa nne Sh.100,000.

Kwa upande wa wanawake bingwa atajizolea Sh.200,000, mshindi wa pili Sh.150,000, mshindi wa tatu Sh.100,000 na mshindi wa nne Sh.50,000.

Mashindano hayo yanatarajia kufikia kilele chake kesho ambapo mgeni rasmi atakuwa ni Meya wa Manispaa ya Iringa, Amani Mwamwindi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Hongera wadhamini vijana tunatakiwa kuwa pamoja michezo ni afya

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 27, 2012

    Duh! Wewe uliteinama usije ukaja kucheza huo mchezo huku zenj, huo huku kwetu wanacheza wanaume ambao ni mchicha mwiba

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...