Mkuu wa Wilaya mpya ya Nyasa mkoani Ruvuma,Mh. Ernest Kahindi akila kiapo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,Mh. Said Mwambungu wa kuwa Mkuu wa Wilaya hiyo katika viwanja vya Ikulu ndogo mjini Songea
Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma,Mh. Abdul Lutavi akila kiapo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,Mh. Said Mwambungu wa kuwa Mkuu wa Wilaya hiyo katika viwanja vya Ikulu ndogo mjini Songea.Katikati ni Katibu Tawala wa Mkoa huo,Sevelin Tossi.
Mkuu wa Wilaya ya Songea, Mh. Joseph Mkirikiti akila kiapo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,Mh. Said Mwambungu wa kuwa Mkuu wa Wilaya hiyo katika viwanja vya Ikulu ndogo mjini Songea.Katikati ni Katibu Tawala wa Mkoa huo,Sevelin Tossi.
Mkuu wa wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma,Mh. Senyi Simon Ngaga akila kiapo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,Mh. Said Mwambungu wa kuwa Mkuu wa Wilaya hiyo katika viwanja vya Ikulu ndogo mjini Songea.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,Mh. Said Mwambungu (kushoto) akimuongoza Mkuu mpya wa Wilaya ya Tunduru mkoani humo,Mh. Chande Bakari Nalicho kushika nafsi hiyo kufuatia uteuzi uliofanywa na Rais Jakaya Kikwete kwa baadhi ya wakuu hao wa wilaya hapa nchini wiki iliyopita.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,Mh. Said Mwambungu (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wakuu wapya wa wilaya za mkoa huo baada ya kuwaapishwa katika viwanja vya ikulu ndogo mjini songea.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,Mh. Said Mwambungu (kushoto) akiteta jambo na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbinga,Kanal mstaafu Edmund Mjengwa (katikati) na Mkuu Mpya wa Wilaya hiyo,Mh. Senyi Ngaga.
Mkurugenzi wa Uzalishaji wa Shrika la Umeme nchini,Boniface Njombe (kushoto) akimsikiliza aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma,Kanal mstaafu Edmund Mjengwa, katika viwanja vya ikulu ndogo mjini Songea kabla ya kuanza kwa shughuli za kuwaapisha wakuu wapya wa wilaya.
Mwanasiasa mkongwe nchini,Alhaji Mustafa Songambele akizungumza na wakuu wa wapya wa wilaya za mkoa huo (hawapo pichani) baada ya kuapishwa katika viwanja vya ikulu ndogo mjini songea.
Picha ya Pamoja.Picha na Muhidin Amri wa Globu ya Jamii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 17, 2012

    Ankal, nimefurahi sana kumuona Mzee wetu Alhaji Songambele. Tangu zamani tulipokuwa tunasoma Dar mzee huyu mkombozi alikuwa mstari wa mbele katika kutetea haki za wazalendo Watanzania.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 17, 2012

    Senyi wa Honolulu Street, Kijitonyama hongera sana

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 18, 2012

    Miaka ya zamani alitoa amri wanawake wote wanaovaa nguo fupi wakamatwe.

    ReplyDelete
  4. Geofrey MoshaMay 18, 2012

    Nakumbuka huyo mzee Songambele alikuwa kiongozi kipindi cha Nyerere na hao ndiyo walikuwa viongozi wa kweli walikuwa siyo mafisadi na walikuwa wanaishi maisha ya kawaida tofauti na viongozi wa sasa.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 18, 2012

    Mdau Geofrey Mosha,

    Nakuunga mkono ni vile viongozi wa zamani walikuwa waadilifu zaidi na wa sasa wengi ni hatari sana.

    Ni vigumu kwa sasa kumtofautisha kati ya Kiongozi na Mfanya biashara.

    Mara nyingine unaweza kumdhania Kiongozi kumuona ni kuwa kama TAJIRI MKUBWA WA BIASHARA!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...