Mkuu wa Wilaya mpya ya Nyasa mkoani Ruvuma,Mh. Ernest Kahindi akila kiapo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,Mh. Said Mwambungu wa kuwa Mkuu wa Wilaya hiyo katika viwanja vya Ikulu ndogo mjini Songea
Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma,Mh. Abdul Lutavi akila kiapo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,Mh. Said Mwambungu wa kuwa Mkuu wa Wilaya hiyo katika viwanja vya Ikulu ndogo mjini Songea.Katikati ni Katibu Tawala wa Mkoa huo,Sevelin Tossi.
Mkuu wa Wilaya ya Songea, Mh. Joseph Mkirikiti akila kiapo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,Mh. Said Mwambungu wa kuwa Mkuu wa Wilaya hiyo katika viwanja vya Ikulu ndogo mjini Songea.Katikati ni Katibu Tawala wa Mkoa huo,Sevelin Tossi.
Mkuu wa wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma,Mh. Senyi Simon Ngaga akila kiapo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,Mh. Said Mwambungu wa kuwa Mkuu wa Wilaya hiyo katika viwanja vya Ikulu ndogo mjini Songea.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,Mh. Said Mwambungu (kushoto) akimuongoza Mkuu mpya wa Wilaya ya Tunduru mkoani humo,Mh. Chande Bakari Nalicho kushika nafsi hiyo kufuatia uteuzi uliofanywa na Rais Jakaya Kikwete kwa baadhi ya wakuu hao wa wilaya hapa nchini wiki iliyopita.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,Mh. Said Mwambungu (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wakuu wapya wa wilaya za mkoa huo baada ya kuwaapishwa katika viwanja vya ikulu ndogo mjini songea.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,Mh. Said Mwambungu (kushoto) akiteta jambo na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbinga,Kanal mstaafu Edmund Mjengwa (katikati) na Mkuu Mpya wa Wilaya hiyo,Mh. Senyi Ngaga.
Mkurugenzi wa Uzalishaji wa Shrika la Umeme nchini,Boniface Njombe (kushoto) akimsikiliza aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma,Kanal mstaafu Edmund Mjengwa, katika viwanja vya ikulu ndogo mjini Songea kabla ya kuanza kwa shughuli za kuwaapisha wakuu wapya wa wilaya.
Mwanasiasa mkongwe nchini,Alhaji Mustafa Songambele akizungumza na wakuu wa wapya wa wilaya za mkoa huo (hawapo pichani) baada ya kuapishwa katika viwanja vya ikulu ndogo mjini songea.
Picha ya Pamoja.Picha na Muhidin Amri wa Globu ya Jamii.
Ankal, nimefurahi sana kumuona Mzee wetu Alhaji Songambele. Tangu zamani tulipokuwa tunasoma Dar mzee huyu mkombozi alikuwa mstari wa mbele katika kutetea haki za wazalendo Watanzania.
ReplyDeleteSenyi wa Honolulu Street, Kijitonyama hongera sana
ReplyDeleteMiaka ya zamani alitoa amri wanawake wote wanaovaa nguo fupi wakamatwe.
ReplyDeleteNakumbuka huyo mzee Songambele alikuwa kiongozi kipindi cha Nyerere na hao ndiyo walikuwa viongozi wa kweli walikuwa siyo mafisadi na walikuwa wanaishi maisha ya kawaida tofauti na viongozi wa sasa.
ReplyDeleteMdau Geofrey Mosha,
ReplyDeleteNakuunga mkono ni vile viongozi wa zamani walikuwa waadilifu zaidi na wa sasa wengi ni hatari sana.
Ni vigumu kwa sasa kumtofautisha kati ya Kiongozi na Mfanya biashara.
Mara nyingine unaweza kumdhania Kiongozi kumuona ni kuwa kama TAJIRI MKUBWA WA BIASHARA!