Mtangazaji wa Kipindi Kipya Mboni Show, Bi. Mboni Masimba kinachotarajiwa kuruka hivi karibuni katika sresheni ya EATV akiongea na waandishi wa habari juu ya kuanza kwa kipindi chake. Pembeni yake ni msimamizi wa kipindi hicho Bw. George Tyson na msimamizi wa vipindi vya EATV. Kipindi hichi cha Mboni Show  dhima yake ni kuburudisha, kuelimisha, kufundisha, uonya, uadhibu na kuelekeza jamii ya Watanzania inayokabiliwa na changamoto nyingi katika maisha ya kila siku. Na pia kipindi kinakusudia kuleta mapinduzi makubwa katika muendelezo wa vipindi vya mahojiano.
Meneja wa Vipindi kutoka EATV akizungumza katika uzinduzi huo wa kipindi cha Mboni Show kinachotarajiwa kuanza kuruka Mei 31 ndani ya EATV.
Msimamizi wa kipindi cha Mboni Show Bw. George Tyson akielezea ubora wa kipindi hicho.
 ======   =====  ======
WASANII wametakiwa kutumia vipindi vya Talk Show kwa ajili ya kutangaza kazi zao sanaa ndani na nje ya nchi ikiwa pamoja na kuitangaza nchi ya Tanzania.

Wito huo ulitolewa na Mtangazaji wa kipindi kipya cha Luninga, Mboni Masimba wakati wa kuzindua kipindi chake kiitwacho Mboni Talk Show chenye kuburudisha, kuelimisha na kufundisha  ambacho kitaanza kuoneshwa Alhamis ijayo katika kituo cha East Africa Television.

Mboni alisema kuwa vipindi vya Talk Show kwa sasa vinapendwa na kutazamwa na watu wengi zaidi kutokana na uvutiaji wake na mijadala mbalimbali ambayo inazungumzwa katika vipindi hivyo.

Akizungumzia kipindi chake Mboni alisema kuwa kipindi hicho kitakuwa na sehemu tano ambazo ni Ufunguzi, wakati wa maswali kutoka kwa mtangazaji kwa wageni na kutoka kwa hadhira kwenda kwa wageni, na pia kutakuwa na kipengele cha My dreams come true ambapo kipindi chake kitatoa misaada kwa watu wenye mahitaji mbalimbali na pia kutakuwa na Tamati.

Alisema kuwa kutokana na ukubwa wa Luninga ya East Africa Tv anahakika kuwa watu kutoka nchi za Afrika Mashariki wataburudika na kufurahishwa na kipindi hicho cha kipekee huku akiwataka wadau mbalimbali kutoa maoni yao mara baada kitakapoanza kurushwa.

“ Ni kwamba Tanzania kuna watu wa aina mbalimbali na wenye vipaji mbalimbali ambao wanatakiwa kuendelezwa na hapa ndipo nguvu ya Tv Talk Show inahitajika na mimi nitahakikisha kuwa kupitia kipindi change cha Mboni Show nitawafikiwa kila wenye kuhitaji msaada wa kuendelezwa kuwa wanafanyiwa hivyo” alisema Mboni .Picha kwa hisani ya www.kajunason.blogspot.com.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 18, 2012

    Oy bab huyo anaitwa Sophia Proches nimesoma nae shule ya msingi Muhimbili darasa moja. Mpe heshima yake bana weka jina lake sio kuishia kuandika Meneja wa vipindi EATV, kha!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...