Mdau Elietha Abrahamu Ayo baada ya kumeremeta na bi Eva Mrindiko wakiwa katika ibada maalum iliyofanyika mapema leo katika kanisa la FPCT Sombetini jijini Arusha
Mchungaji kiongozi wa kanisa hilo bi Elinansha Abrahamu akiwa na Askofu mkuu wa kanisa hilo Boniface Nko wakiwa wanafunga ndoa ya maharusi hao.
Akifunga harusi hiyo askofu Boniface Nko amewataka wanandoa wote nchini kuhakikisha kuwa wanasimamia misingi ya ndoa kwa kuwa wengi hawasimamii misingi hiyo hali inahyopelekea ndoa hizo kuvunjika mapema.
Vile vile amewataka wanawake kuacha kudai haki kwa kupita kiasi kwani wanapotumia mabavu kudai haki ndio chanzo cha ndoa kufarakana.
Picha na Mary Ayo
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...