Asallaam Aleykum wasomaji wote wa globo hii
Namuomba Allah anijalie niweze kusema yenye kutufaidisha duniani na kesho akhera inshaallah...

Ndugu zangu nimesoma nakala na maoni mbali mbali yanayochangia mjadala wa tukio la  vurugu zilizotokea Zanzibar, ndugu zangu ni kweli kwamba si wazanzibar wote na wala si waislamu wote kuwa ndio waliosababisha vurugu hizi, ni baadhi yao tu na kwa sababu zao wanazozifahamu wao wenyewe, ingawa wazanzabar wote, waislam na dini yetu ndio tunashutumiwa na kushambuliwa bila kutofautisha. 

Hata hivyo naelewa hisia na uchungu wa yaliyotokana na vurugu hizo kwenu. Kwanza kabisa nawapa pole wote walioadhirika na vurugu hizi kwa namna yoyote ile, iwe mali, kimuili na hata kisaikologia. Pili mimi binafsi kwa dhati na kutoka ndani ya moyo wangu naomba na nawaombea radhi waliosababisha machungu haya makubwa ndani ya nyoyo zenu (katika jamiii). Naomba Allah atujaalie moyo wa subra na kutulipa malipo yaliyo bora zaidi.

Ndugu zangu nashuhudia mbele ya Allah na mbele yenu kwamba uislam ni dini ya amani, upendo, ushirikiano na uvumiliano na hivyo ndivyo inavyotutaka tuwe, si tu baina ya muumini na muumini bali hata nnje ya hapo. Kuchoma moto makanisa na kuharibu mali za watu hata mali binafsi si mafundisho ya kiislam, Uislam unakemea haya na naomba Watanzania wote tulaani na tukukae fujo. Naipongeza serikali kwa hatua ilizochukua, Kwa tukio hili, naomba tunaopenda amani wote tuipe ushirikiano serikali yetu. 

Na kwamba wote waliohusika wachukuliwe hatua inayostahili haraka iwezekanavyo. Kumbukeni kwamba bila Amani hakuna Tanzania, Bila Amani hakuna Zanzibar, Bila Amani hakuna Pemba na kamwe pasipo Amani UROJO HAUTALIKA.  Bila Amani hakuna Ushirikiano na wala hakuna Upendo. Na pasipo na Amani hapatakuwa na haki wala maendeleo. Tulinde Amani ili tupate Maendeleo. Na tukitengeneza chuki kurudisha Amani itatugharimu. Inshaalaah !
Kwa sababu kila tukio lina fundisho, Ndugu zangu nawaomba tutitazame tumejifunza nini katika tukio hili la fedheha na kusikitisha. Lakini pia sina budi kuwashukuru sana wale wote waliosababishiwa madhara na fujo hizi kwa uvumilivu mkubwa waliatuonyesha katika hili. Mmeonyesha burasa na hekma kubwa katika jamii yetu, na hii ndio maana ya kuishi kijamii hongereni sana, na wito wangu kwa Wazanzibar na waislam wote tujifunze uvumilivu wa namna hii, Uvumilivu ni moja ya ibada na kila mwenye kuvumilia (SUBRA) yuko na Allah. Ghadhabu, hasira na fujo ni dalili ya kuwa na shetani.
Ndugu zangu, kwa mapungufu yoyote yaliyojitokeza katika maandiko yangu, namuomba Allah na nyie wasomaji mnisamehe, kwani aliye msahihi ni Allah na ndie anayestahiki sifa zote nzuri, rehma na Amani zimongezekee mbora wa viumbe mtume wetu Muhamad (SAW).
EEEH MWENEZI MUNGU NAKUOMBA, UJAALIE AMANI NCHI YETU TANZANIA, ALLAH NAKUOMBA UTUJAALIE AMANI NA UPENDO WATANZANIA WOTE,  ALLAH NAKUOMBA UTUEPUSHE FUJO HIZI ZILIZOTOKEA SIJETOKEA TENA NCHINI MWETU.
Asalaam Aleykum
Mdau Zenji

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 31, 2012

    Alaykum Salaam,

    Mdau wa Zenji, ahsante sana kwa Hekima na busara zako.

    Wewe ni miongoni mwa Wazanzibar wachache ambao ni Rasilimali na muhimu sana kwa Jammii yetu.

    Dunia ina nchi ambazo zina Serikali za Kiislamu mfano, Saudi Arabia,Iran,Misri, na nyingine nyingi ambazo Waumini wa Dini zingine ni miongoni mwa Raia wa nchi na wanatendewa haki, je kwa nini Zanzibar watu wa Dini zingine wafanyiwe ubaya?

    Wewe Mdau wa Zenji Muungwana pamoja na wenzio wenye fikra kama zao ni Jukumu lenu sasa kuwaelimisha hao Wajinga wachache kuwa:

    1.Dunia nzima ina matatizo ya Kiuchumi na Kifedha achilia Zenji sema Marekani na Ulaya hata Arabuni nchi zilizoimarika zaidi zinahaha, hivyo wasiilaumu sana Mamlaka/Serikali na Chama Tawala kwa kuwa tatizo hili lipo juu ya uwezo wa nchi zote Duniani, cha muhimu ni kujifunga mikanda na kukabiliana na matatizo.

    2.Kwa sababu ya hapo juu No.1 waeleze kuwa Kuvunja Muungano siyo suluhisho la wao kupata maisha bora,na wala matatizo yao ya ugumu wa maisha kamwe hautokani na wao kuwepo ktk Muungano.

    3.Waelimishe zaidi kama nilivyosema hapo juu nchi nyingi za Kidini duniani zinaheshimu dini zingine hivyo kigezo cha MUAMKO WA UISLAMU SIO KUMFANYIA UBAYA MUUMINI WA DINI NYINGINE (WAREJEE QURAN NA SUNNA ZA MTUME MUHAMMAD S.A.W) na kinyume chake badala ya 'UAMSHO' wa Kiimani itakuwa ni 'UANGUKO' wa Kiimani!

    WA BILLAH TAWFIQ

    Mdau Mohamed M.
    mohamedtzn@AOL.COM
    Dar Es Salaam

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 31, 2012

    Ewaaa, umenena. SHUKRAN JAZEERA.

    Mdau, bara

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 31, 2012

    Hakika mdau Umenena vema! Ila mbona hii ni kama sindano ya Ganzi Mara baada ya da utaviona tena! na kisha tutaambiwa Subra na uvumilivu na hongereni kwa hayo wakati mali zimiharibiwa na majeraha tumebaki nayo!! Tusaidieni kuwafichua hao wasio wenzenu tuwajue na sheria na haki viwaamulie hatima yao!

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 31, 2012

    Tuwe wakweli. Issue ni Muungano!/ Udini ama Yote Pamoja!!?
    Ubara na Uzanzibari/Upemba? Ama yepi/ Daima tumtangulize Mungu wetu katika kufikiri na kabla ya kutenda. Vema sana Tukiyakumbuka ya Mwl J.K Nyerere. Dhambi ya Ubaguzi ni mbaya sana Na ukishaianza hutaishia hapo1 N a huta baki salama! Simple Tuache ubinafsi! God Bless Us All

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 31, 2012

    Nakupongeza kwa kuandika maneno yenye hekima na busara. Watu wote tungekuwa na busara kama yako basi maisha yangekuwa ya raha sana. Maana umeonyesha binadamu tunavyotakiwa kuishi. Ni jambo la msingi sana kuvumiliana maana sote tu waja wa Mwenyezi Mungu na kwake tutarejea hakuna aliyeumbwa na Shetani. Sote tu waje wake kwahiyo hakuna haja ya kujiona wewe ni bora zaidi ya mwingine. Na anayetakiwa kutuhukumu la Allah peke yake siyo sisi binadamu.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 31, 2012

    yes bro umesema kweli sio kila mzanzibar anapaswa kulaumiwa na sio waislam wote walifanya fujo! mimi binafsi nalielewa vizuri na natamani kama watanzania wote wakielewa hivyo badala ya kulaumu kwa ujumla. huku ughaibuni tunaishi vizuri sana bila kuangalia mtanganyika au mzanzibar. zaidi wachache wanaofanya haya mambo wanawaharibia wengine bila kuangalia madhara ya wanachokifanya

    MUngu ibariki Tanzania

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 31, 2012

    Mdau i congratulate you, kwa kuwa muungwana. Wazanzibar tokea zamani walikuwa wakisifika kwa kuwa watu wastaarabu, sasa mambo kama haya yanaharibu kabisa picha ya kisiwa chetu cha zanzibar. Tunaomba mungu mwenyezi nungu wa rehema awasamehe wale wote waliosababisha hizi fujo na kuwaonyesha njia. na watu kama wewe muzidi kuwa wengi kisiwani na Tanzania kwa ujumla.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 31, 2012

    Assalam Alaykum !

    Muungwana mpenda amani pia waelimishe hao wafanya fujo huko Zanzibar ya kuwa wasichukulie kuwa Wakristo wote huko Visiwani ni watu wa Bara sio kweli.

    Inajulikana kuwa wapo Wazanzibari ambao ni Wakristo pia!

    'Jamhuri ya Kiislamu ya Iran' , Jamhuri ya Kiarabu ya Misri na Ufalme wa Saudia (KSA)zina raia Wakristo itakuwa Zanzibari?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...