Kampuni ya Michelin ya Ufaransa na kampuni ya Kizalendo ya Superdoll Tanzania Ltd. wamezindua matairi yenye ubora na usalama kwa magari aina ya Michelin XM2 yenye uwezo wa kuhimili barabara mbovu katika Afrika Mashariki na kati. Mkurugenzi mkuu wa Superdoll Bw. Seif Ally Seif amesema matairi hayo yametengenezwa kwa utalamu wa kisasa ili kuzuia kupasuka yanapokanyaga kitu ambacho kina weza kusababbisha kupasuka. Amesema matairi hayo ya Michelin XM2 yanapunguza gharama kwa watumiaji katika kuokoa fedha kwa vile yanadumu kwa muda mrefu na kuokoa matumizi ya mafuta.
Mkurugenzi mkuu wa superdoll Bw Seif Ally (kulia) akimsindikiza balozi wa ufaransa hapa nchini Mh. Marcel Escure ambaye alihudhuria uzinduzi wa kampuni ya Michelini Ufaransa katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam
Bwana Jamal Bayser akiwa na ofisa mwenzake wa kampuni ya Superdoll na sanamu ya Michelin |
HONGERENI SUPERDOLL KWA BIDHAA ZENYE UBORA WA HALI YA JUU. MATAIRI YA MICHELIN NI IMARA NA MADHUBUTI.
ReplyDelete