Kaka michuzi naomba uniwekee kwenye blog ya jamii ili nipate ushauri na mawazo kutoka kwa wasomaji
Mimi ni kijana wa kiume (39) niliye anza kuoa miaka tisa iliyopita. Mpaka sas nina wake wawili na kwakuwa inmani yangu inaruhusu basi sikuona kwanini niwe na mmoja ili hali dunia imejaa wanawake wazuri na warembo na kila mmoja anamvuto wa pekee.
Nilimuoa bi mdogo miaka 4 iliyopita, nikiwa tayari nina watoto 2 kwa bi mkubwa. Mungu kanibariki sasa ninao 3 yaani bi mkubwa 2 na mdogo 1 na sina mpango wa kuendelea tena kuzaa. Kuna tatizo moja ambalo limejitokeza ndio maana nimeamua kuja hapa kutaka ushauri wenu.
Wake zangu hawa bi mkubwa na bi mdogo wanapendana sana, kiasi kwamba napata raha kuish nao, mdogo kwa sheria zetu basi anamwita mkubwa dada. Kila mtu ana mji wake wa maana kwamba nimewajengea ila siyo maeneo ya karibu kiasi kwamba wakitaka kutembeleana lazima wapande gari.
Mimi ninayepanga zamu kwangu hainipi shida kwani yote ni miji yangu so nikiwa kwa dada mtu mdogo mtu najuaa na kinyume chake. Sikuwahi hata siku moja kuchukia urafiki wa wake zangu na nilipendezwa sana wala sikujua nini kimo kati yao wao nisichokijua.
Kumbe wote wawili wana vidumu (mabuzi) katika kuchunguza nikajua kuwa dada na mdogo wake huwa wana vibuzi maringo na nikiwa zamu basi asiye kuwa na zamu anatoka na kibuzi chake. Kiasi kwamba siyo wao tu wenye zamu kumbe hata mimi napangiwa zamu.
kwa kweli nimechukizwa na hali hii na sijui nifanyeje manake sitaki kuongeza mke mwingine hawa nilio nao naona nawamudu isitoshe sitaki kuzaa tena watoto tulio nao wanatosha.
Naombeni ushauri juu ya hili nifanyeje au wewe ungefanyeje kama mwanaume mwingine anakuja kulala nyumbani kwako na kula vyakula mpaka wake zako? kila mmoja anakibuzi chake na hivi vibuzi vinafahamiana.
Nawasilisha


Ingawa imani yako inakuruhusu, ulipoamua tu kuwa na wake wawili hapo ndiyo ulipokosea. Suluhisho hapo ni kumuacha mmoja ubaki na mwingine kwa kuwa huwezi kuugawa moyo wako vipande viwili. Unapokuwa na wake wawili inawafanya wote wasijiamini kwamba unawapenda hivyo kuamua kujifariji some where else. Usipokubaliana na hili basi uendelee kuvumumilia, usishangae utakapoachwa wewe watakapojisia kuwapenda hao unaowaita vibuzi zaidi. Achana na sheria walizotuletea waarabu angalia uhalisia wa mapenzi.
ReplyDeleteIkiwa una uhakika kuwa wote wana wanaume nje wewe usiwe mwanaume ambaye si rijali. Jikaze kiume na waache mmungu atakupa wake wengine bora zaidi ya hao. Huo ndio ushauri wangu kwani hakuna amani katika penzi lenye usaliti ndani yake.
ReplyDeleteNakushauri wacha kuleta dhihaka na imani za wezako. Kama kweli ni wewe ni Mwislam, basi taratibu za kiislam zipo zinazohusu masuala haya nakushauri rejea katika vitabu na utapata jibu la masuala yako.
ReplyDeleteHivi wewe unasema una wake wawili na sasa unaomba ushauri wa jinsi ya kuishi na wake zako hadhari. Jee huu ndio utaratibu?
Narujdia tena ACHA UTANI NA IMANI ZA WENZAKO.
ningewajua wake zako ningewapa pongezi, kama ulioa wake wawili kwa maana ya kwamba dunia imejaa warembo, unadhani watanashati wamekwisha? Basi na we vumilia zamu kama wanavyovumilia wenzako, na ukiongeza mke wa tatu ndo utamu kolea maana zamu itaongeza siku za kuwa off.
ReplyDeletemi sitaki kumshauri huyu kama kwa kuwa sina ushauri ambao utamfaa ila ninachotaka bro ni kuwaambia wanaume wote wanapenda kuoa wake wawili au hata wanaopenda sometimes kulala nyumba ndogo mwanamke ni mvumilivu sana na kwa kawaida hakuna mwanamke anayependa kudhurumiwa penzi lake kwa mfano huo ndio nawaambia wakaka mkiwa nyumba nyingine na wenzenu wanatafuta faraja barabarani. tulieni na wake zenu au wapenzi wenu for realy hakuna penzi la kushea ni uongo tu
ReplyDeleteHahahahahaaaaaa, kijibaba ulihisi unawamudu sasa ushajua mapungufu yako wapi. Hata kama dini inaruhusu nyakati zinztofautiona bob zamani ilikuwa inawezekana ila sio sasa, na yawezekana unalea watoto sio wako> Ushauri ndugu yangu, fuata dini yako sawa ila soma alama za nyakati hizi sio enzi za mababu zetu, mke mmoja anatosha utapasuka msamba
ReplyDeleteMuondoa ujinga
PELEKA KESI MAHAKAMA HUSIKA.
ReplyDeleteNenda kwa shehe wako atakupa mawazo safi.
Humu subiri utapata kejeli hasa kutoka kwa watu wa imani inayopinga mitaala. (MAHAKAMA ISIYOHUSIKA)
Watakwambia "mke mmoja mme mmoja bila kujali kuwepo na tofauti ya imani, kwani isilamu si lazima aishi maisha ya ki-biblia"
wengine watakwambia ukome hiyo ndo dawa ya wapenda mitaala, hii yote kwa sababu somo linawaudhi.
HAWAONI KUNA WASIO MITAALA LAKINI NYUMBA NDOGO NA VIBUZI KWA WINGI.
DINI INATUTAKA TUNAPOCHAGUA MKE PAMOJA NA KUPENDEZWA NA UZURI, MALI ALIYONAYO AU UMAARUFU WAKE NI LAZIMA KWANZA UANGALIE KAMA ANA DINI, MKE MWENYE DINI YAKE HAWEZI AKAVUMBUA KIBUZI KWA SABABU MAFUNZO YANAKEMEA JAMBO HILO KWA UKALI SANA.
ReplyDeleteMOJA YA USHAURI NI KUWAACHA BILA KUWAFANYIA UBAYA WOWOTE NA KUOA MKE MWENYE DINI HATA KAMA SI MZURI KAMA WAO. KISHa UENDELEE KUWAJIBIKA KWA ULEZI WA WATOTO WAKO ULIOZAA NAO.
nilikwambia watasema "PENZI HALIGAWANYIKI"
ReplyDeletemimi ni msichana mwenye umri mdogo sana, ila katika miaka hiyo michache niliokuwa duniani, hakuna kitu nilichokuwa nakisubiri kama kuolewa. Ila kusema ukweli jinsi kaka zetu na dada zetu mnavyofanya inatukatisha tamaa sana. Kweli hizi ndo zimekua ndoa za sasa hivi? Kweli haya ndo maisha tunayoenda kuyakuta huko mbele? Tutaolewa kweli sisi? Sijui. Kweli inakatisha tamaa na pia kuogopesha kweli. Unakuta msichana kama mimi umejitahidi kujiweka vizuri, kuwa mtulivu, kujifunza vyote unavyodhanni vitampendeza mume wako mtarajiwa halafu unakuja kukuta anoa mke mwengine? Mimi ntakuwa nakoasoro gani jamani ambayo hatujaweza kukaa tukarekebisha kama mume na mke? Au hivyo basi, namimi pia ikanibidi nitoke nje, kweli utaenda kutangaza kwa watu bila kukaa na mimi tuyatatua kimya kimya? labda nimawazo yangu yakitoto ila mi naona niseme hayo tu.
ReplyDeleteFata sheria soma vitabu uliza wenye elim sio magazetini utatukanwa bure, una uwezo piga teke chukua watoto na taraka ni halali kama kweli unamaadili ya dini yako kama ulivojibiwa kua rijali ,we mwenyewe unajua dunia imejaa wanaongojea kuolewa na chagua wenye imani sio mradi ya uzuri kumbuka "mzinzifu haowi wala haolewi ila na mzinzifu mwenzie".
ReplyDeletesi ulitaka chai, kwanini useme unaungua?
ReplyDeletePole sana, ila kwa masuala ya kiimani kama haya na ambayo yanagusa imani ni bora utafute suluhisho mahali muafaka sio kwa kila mtu. Na mahali pazuri nenda kwenye blogu yetu waislamu www.alhidaaya.com ambayo tunauliza maswali hasa yanayohusu imani na kupata majibu mazuri na muafaka kama swali lako. Hapa utapata ushauri kwa watu ambao imani yao haiwaruhusu kuoa wake wawili, hakuna watakachokushauri zaidi ya kuponda imani zetu waislam ambazo kimaumbile na hata kiimani wanaume ruksa kuowa wake wanne. Wao unaweza kuzini na kuwa na kimada nje ya ndoa lakini sio kuongeza mke mwingine, na hata maudhi yakizidi hakuna kuachana, Je kiulasia haiingii akilini. Na Upande wangu ninachokushari ulikosea wakati wa kutafuta mke wa kuoa kwani dini yetu waislamu inasema tafuta mwenye dini na mchamungu.Hao wake zako sio wacha Mungu na wala hawana hofu ya Mungu kwani Adhabu ya muislam anayezini nje ya ndoa ni Kupigwa mawe mpaka kufa. Hivyo kaa nao kwa upole na uwausie adhabu ya Allah na pia magonjwa sasa ni mengi. Pia ufanye uchunguzi utakapobaini na kushuhudia ni kweli unaandika talaka kwani hata dini yetu inasuluhisho la kila tatizo kama tunaisoma vizuri na kuilewa kuanzia Quran hadi Suna za Mtume Muhamadi.
ReplyDeleteSharia ya kuoa zaidi ya mke mmoja haijaletwa na waarabu kama anavyosema mchangiaji wa kwanza. Hii ni sharia ya dini ya kiislamu. Na kuna sababu na masharti yake. Na mimi namuuliza sharia ya kua na mke mmoja na mahawara wengi imeletwa na nani?
ReplyDeleteUlivyoamua kuoa mke wa pili ulijua sheria zake au uliamua tu kuoa kwa sababu kipato chako kiliongezeka? na ingekuwa unawaridhisha wake zako wasingeamua kuwa na mabuzi nje, kaa chini ufikirie mwenyewe unataka nini katika maisha yako? nani ni muhimu kwako? na ushauri wnagu ni kwamba hakuna mwanamke anataka mume wake akaoe mke mwingine kwa hiyo wewe amua mwenyewe katika roho yako unataka nini kwani ushauri wetu hautakusaidia kutatua matatizo yako, ulivyoamua kuoa hukutaka mashauri ya mtu na sasa pia fanya maamuzi kutokana na roho yako, ila kama unaona raha na wewe kuwa na zamu na waume wenzio basi hayo ndio maisha unayoyataka, na usipoangalia utampoteza mwanamke ambae ana maslahi na wewe.
ReplyDeleteNimefurahishwa na hii mada, Kijana umri wako si vyema kuwa na wake wawili japo dini ya kiislam inaruhusu ila wewe huijui dini-Dini ya kiislam inaruhusu kwa sababu za msingi kuongeza mke wa pili kama mke wa kwanza ana matatizo ya maradhi au hakujaaliwa kupata kuzaa na mengine yakupelekea kuoa mke wa pili!!! Wewe unaonekana ni mwenye tamaa na uroho-Unadhani unaweza kugawa mapenzi sawa kwa wake zako???? Mimi ni Muislam na umri mkubwa kwako-Lakini kutokana na tabia yako hiyo ya tamaa nimefurahishwa sana na uamuzi wa wake zako kweli vijana wa siku hizi mna akili na mnaenda na sayansi na Technologia-wewe ulikosa nini kwa mkeo wa kwanza? NAWAPONGEZA SANA HAWA MABINT kama ulijiona wewe ni mali na wao ni mali vilevile., na iwe fundisho kwa vijana wengine.
ReplyDeleteNakubaliana na Mchangiaji no.3, kwa asilimia 100!
ReplyDeleteACHA KUFANYIA DHIHAKA DINI ZA WENZAKO,MARA MOJA!
Kama wewe kweli ni Muislamu,basi dini ya kiislamu ina taratibu zake na ndio maana qur-ani haikusema tuongeze wake kwa 'UREMBO' wao, bali tuwaoe ikiwa tumejiridhisha kwamba, tunaweza kuwafanyia 'UADILIFU'. Sasa, kama wewe ni Muislamu 'kweli', kiasi yakukute hayo,kwavile 'UMEDHARAU' amri ya Mungu kwenye qur-ani, lakini kama sio Muislamu, basi rudi kwa viongozi wa 'IMANI' yako watakupa maelekezo!
MCHANGIAJI WA 8:46 AMBAYE ANADAI KUWA JAMAA ANATANIA DINI ZA WATU YEYE NDIE ANATANIA. HUO NDIO UKWELI WA MAISHA YA SASA. KAMA KAULIZIA HADHARANI NI HAKI YAKE KWANI ANAPATA MAONI KWA UPANA ZAIDI KULIKO KUBAKIA KATIKA KAYTA YAKE....UKWELI NI KUWA KWA TAMAA UNAWEZA KUWA NA WAKE HATA WANNE, LAKINI KIUKWELI WA MAISHA YA UAWAZI HUWEZI KUWATIMIZIA HAWA KIMAPENZI. KINACHOTOKEA NI WANAWAKE AMBAO HAWANA CHAGUO ILA KUKUBALI NA PIA WASNAOBANYWA MAWAZO YA WATU KAMA MCHANGIAJI WA 8:46 NA HAPA UNAONGEA NA MWANAUME RIJALI. USHAURI... KUBALIANA NA HALI HALISI ..CHAGUA MMOJA..KAMA ATAKUKUBALI.????
ReplyDeleteHata kama ningekuw me,ucngenlzsha kama navotaka,waschana wnapenda kujaliwa kila mda sasa ww uko huku n kule htoweza kuwalzsha,lamcng kuw n m1
ReplyDeleteEti unawake wawli na unawamudu!!,sasa kama unawamudu unalalamika nini humu?hauwamudu na ndio maana wenzio wanakusaidia,siku zote waswahili husema mpanda farasi wawili huchanika msamba,wewe hujui hii methali?ushauri wangu ni kwamba hao wake zako wote wameshakua wachafu hawakufai tena,maana wameshaonja utam wa nje,hawaji kuacha kamwe,wapige chini wote,oa mwingine,lea watoto wako,na achana na imani za kizamani kuoa wake wengi,dunia imebadilika kaka,upo wapi wewe? Mdau Tottenham London.
ReplyDeleteEti dunia imejaa warembo... Sasa wahangaika nini na jibu unalo? Kwani hao warembo wameisha? Sababu ya mwislam kuoa wake wengi ni hiyo ya warembo kuwepo wengi duniani? Nilidhani ni tofauti na hapo.Halafu sheria za kizamani za kuoa wake kibao, zimepitwa na wakati baba?
ReplyDeleteKajipange upya.
Pole sana.
ReplyDeleteKabla ya kufanya maamuzi yoyote ningeshauri wewe na wake zako mkapime mjijue status za afya zenu. Pili muangalie maslahi ya watoto. Hapo ndipo ufafanuzi wa swala lako utapatikana.
Kumbuka; More Women,More Problems!
Yaani nimewapenda saaaana sana anon wa Wed May 30:08:48:00AM 2012 na Wed May 30, 08:50:00 AM 2012 kwa kumpa vipande vyake huyo jamaa.
ReplyDeletehakunaga mapenzi ya wa tatu,ndomana wametafuta viburudisho,kwani unapokuwa na mwingine jua anayekuwa peke yake unampa muda wa kuwaza vitu vingi vibaya juu yako,si lazima tufanye kila alichofanya mtume,sisi ni binadamu na yeye Mtume so hatufanani kabisa.
ReplyDeleteMimi si Mwislam lakini nimewahi kusikia kabla hujaoa mke mwingine kwa sheria ya dini yenu unatakiwa kwanza ukubaliane na mke wa kwanza ndio uongeze mwingine je hilo ulifanya? kama ulitumia mfumo dume ukaoa mke mwingine bila kumshirikisha wa kwanza hayo ndiyo matunda.
ReplyDeletePili mimi ni mwanamke kwa hiyo naongea hapa kwa kumwangalia mwanamke mwenzangu, Unajua hata dini yenu inasema oa wawili kama unaweza kuwaridhisha wote lakini kama huwezi acha. Sasa mwenzangu tunaolewa ili ukiwa na haja/hisia(feelings) ya mwili upate mwenza wa kukutuliza lakini inakuwaje pale ninapokuwa na haja ya mwili mwenza yupo zamu nyumba nyingine? Wewe huna haja hata siku moja kwa kuwa wazunguka, lakini wake zako zipo siku wana haja wewe haupo uko zamu kwingine Je wafanyeje na haja zao? Je hapa umetimiza ile amri ya kuwaridhisha kama dini inavyosema? au kwa kuwa wao ni wanawake watulize haja zao na wakusubirie wewe uje? Think out of the box utapata jibu wapi umekosea.
Asante Nawakilisha pia kama niliyoyasikia kuhusu Uislamu niliyoandika hapo juu nimekosea samahanini sina nia ya kuchambua dini bali ni jinsi ambavyo nimewahi sikia and not otherwise
Kaa nao chumba kimoja
ReplyDeleteAngalia mmoja ataanza kuwa na mkanda wa jeshi na mwingine kifua kikuu. Acha uhuni kwa kujidanganya kuwa ni imani yako. Haya sota nayo sasa
ReplyDeletemuosha huoshwa!Kaka wewe tulia tu, na inawezekana hata hao unaowaita watoto wako pengine si wako. Kosa lako ni pale tu ulipoongeza kidumu.Pia inawezekana hata kimahaba huwaridhishi kwakua unakua umechoka sana kutokana na zamu; na wao ni binadamu walipotest nje wakakuona huwafai. Ila kama ungekuwa na mmoja ungeweza kum-service vizuri. Imekula kwako, pole.
ReplyDeleteHabari ndugu yangu unaeomba ushauri.
ReplyDeleteSina hakika Imani gani uliyoikusudia katika ombi lako la ushauri. Ninavyofahamu mimi, kuna imani za Kidini na Kimila ambazo zinaruhusu kuoa wake zaidi ya mmoja. Ndio maana nimesema unaposema Imani yako imekuruhusu kuoa wake zaidi ya mmoja unakusudia Imani ya Kidini au ya Kimila.
Kwa priambo hiyo, majibu yangu juu ya ombi lake la ushauri ni kwamba, kama ameoa kwa imani ya didi basi arudi katika maelekezo ya dini yake nasemaje hali inapofikia hapo na kama ameo kimila basi arudi katika maelekezo ya mila zake kwamba anatakiwa afanyeje hali inapofikia hivyo.
Mwisho, si dhani kama kijana amefanya sahihi kumwaga madudu yake makubwa yasiyoweza hata kusikilizika katika mtandao wa kijamii kama huu.
Mambo ya ZINAA na kumtilia mashaka MKEO/MUMEO ni jambo gumu kabisa ambalo hufanya hiyo dhana uliyonayo kuwa ni TALAKA kamili na wala huna haja ya kuandika talaka ya maandishi pale unapomdhania UZINZI MKEO (Hii ni kwa mujibu wa baadhi ya imani fulani)
Ujumbe kwa wote: Mambo mazito kama haya huzungumzwa 'Chamber Court'.
Pole sana.
sasa hapo tatizo ni nini? mbona wewe unao wawili? hivi katika uislam tunavyoambiwa uongeze mke kama utawatimilizia, huwa mnafikiria chakula na malazi, no inamaanishwa kuwatimilizia, yani anachopata mmoja na mwingine apate, wakati sawa, siyo zamu kama mnavyofanya waislam uchwara wengine, wake zaidi ya mmoja kwa maisha ya sasa si ruksa, sababu hautawatimilizia. stress kibao, mavyakula yanaondosha mambo mengi, mazingira tuishiyo, kwahiyo sihaki kuoa mke zaidi ya mmoja, nina hakika na haya niyasemayo, tafuta hata msahafu wa kiswahili usome mwenyewe siyo mambo ya kwenda kwa wengine kuulizia, ukweli ndio huo, mke ni mmoja tu, ukioa wapili unajitafutia dhambi tu maana hautamtimilizia
ReplyDeleteasante sana, leo nimecheka, nimewapenda hao kidada. Ulidhani we ndo mjanja kumbe ukigeuka kinadada wanakung'ong'a.
ReplyDeleteOn serious note:
Kaa na wake zako mtatue hilo tatizo ila ujifunze, acha kusingizia imani kufanya yasiyo faa
Yani hawa wanawake nawapa big up sana hivyo ndivyo ilivyokwa wote wenye vimada nje sema hamjagundua tu na wake zenu hivyo hivyo halafu wananifurahisha kwani vibuzi vinajuana. Unajidai kidume hiyo ndo komesha yako hakuna cha dini wala nini umalaya wenu tu
ReplyDeleteKULA RAHA WEYE ...KULIWA JE???????? HALA
ReplyDeleteEti dunia imejaa warembo... Sasa wahangaika nini na jibu unalo? Kwani hao warembo wameisha? Sababu ya mwislam kuoa wake wengi ni hiyo ya warembo kuwepo wengi duniani? Nilidhani ni tofauti na hapo.Halafu sheria za kizamani za kuoa wake kibao, zimepitwa na wakati baba?
ReplyDeleteKajipange upya.
kaka moyo wa mwanamke ni mmoyo usio weza kushea penzi na mwanamke mwenzie. kama wake zako wanapata sana ujue nao ni washenzi na wameamua kukukomesha and ofcoz kupata maisha kama unayo wapa. katika hali ya kawaida mwanamke hawezi vumilia kusikia eti leo umeenda kulaa huku then next time kule. afu,hebu rudi nyuma jitazame ulivyo mbinafsi,umeoa mke wa pili ili kuendelea kula raha kadiri utakavyo,do u think hao wanawake kazi wanatakiwa kuhakikisha wew unakula raha tu kwa mateso yao? hata wao wanapenda raha pia, na wote wanahitaji kuridhishwa na kujipatia haki yao bila kizuizi. so kama huwezi kuwa na mke mmoja, waache wenzio nao wajifaidie kwa zamu.
ReplyDeletehahaha....dini yako inaruhusu mke zaid ya mmoja ila ni vizuri ukajitahid kutumia utashi wako pia. mbona watu kibao wana wake but kazi za nje wanapiga kwa staha bila wake zetu kujua afu maisha yanaendelea tu. pole kaka!
Hata kama una mmoja, vidumu ni kama kawa kijana. Usiniambie hujui, hujawahi kusikia. mke kuwa na kidumu, wala haina uhusiano na kuwa nao wawili!
ReplyDeletesubiri ukimwi ndio utatia akili. Anza ARV mapema kabla dalili hazijajitokeza.
ReplyDeleteNi dhahiri wewe ndie the odd man out;maana wakezo wanaelewana.Je,bi mkubwa ulimshirikisha ktk kuoa mke wa pili? Na je,wajua huko Asia kuna nchi ambapo mke huoa waume wengi?Ndoa sio mizaha mizaha.Kaa nao mkubaliane,mpate suluhu.Umeyavulia maji;sasa ni budi uyaoge baba.Uislamu ni dini thabiti,sio mteremko wa mihemko.
ReplyDeleteHi,
ReplyDeleteKaka pole sana kwayaliyokupata ila naona kwamba wake zako walikwisha kusoma kwamba huwatoshelezi hivyo kujiandaa na kutafuta vibuzi nje jitahidi kuwatosheleza uone kama watakuwa na nguvu ya kutoka kwa vibuzi. Kila la heri.
Ni dhahiri wewe ndie the odd man out;maana wakezo wanaelewana.Je,bi mkubwa ulimshirikisha ktk kuoa mke wa pili? Na je,wajua huko Asia kuna nchi ambapo mke huoa waume wengi?Ndoa sio mizaha mizaha.Kaa nao mkubaliane,mpate suluhu.Umeyavulia maji;sasa ni budi uyaoge baba.Uislamu ni dini thabiti,sio mteremko wa mihemko.
ReplyDeletepiga chini hao utaumia maisha yako yote ukikaa nao no trust
ReplyDeleteushauri wangu ni huu, ishi nao wote wawili si wanaelewana? ungeuza nyumba zako 2 ukajenga gorofa 2 ndogo tu juu mke mkubwa chini mdogo, hapo utakata mzizi wa fitna, otherwise utajibeba kama king mswati wataliwa tu!
ReplyDeleteKwanza na wasiwasi hii ni story ya kupika.
ReplyDeleteLakini kwa ujumla dini yetu we wafahamu kabisa imekamilika na wala haikuacha kitu. Ni vema kwanza ukakaa na wake zako na frankly mkaongea kuona tatizo lipo wapi. Mimi nikiwa na mke mmoja na Inshallah sababu za kuongeza zikija nitaongeza kama maneno ya Allah mwenyewe.Lakini kikubwa tafuta watu wenye ilmu sahihi ukileta jambo kama hili humu utahangaika kupata jibu sahihi maana kuna watu hawana imani na suala hili wajua ni la imani.
mimi nakubaliana sana na mtoa maoni wa pili hapo juu, kama uhakika unao kuwa wake zako wanakuendea kinyume na kuwa wote wanamabwana wengine
ReplyDeletebasi wewe usirudi nyuma wote waache kwa siku moja na usiangalie nyuma hao hawafai kwako, na tafuta mke bora atakaekuheshimu wewe kuwa ni mume
laa wewe unafanya mchezo humu kwenye mtandao kuchezea dini za watu na si muislamu una joke tu, basi mwenyezi mungu akushushie lana mazito usipate hata kuijuwa hii computor ukiiona kwa macho uwe unaikimbia mwenyewe amin,
Ndio shida ya kuwa na wawili, unapokuwa small house wa big house anajisikia lonely nayeye anatafuta mbadala vivyo hivyo ukiwa big house. POLE
ReplyDeleteAcha utani na dini za wenzako! Ungekuwa ni imani yako usingeweka hadharani humu! Viongozi wa dini na shahidi wako wapo walipaswa kutafita ufumbuzi wa tatizo lako na sio humu. Acha dhihaka.
ReplyDeleteAcha uwongo wako wewe.
ReplyDeleteNamuunga mkono Said, Naamini alioandika hii mada sio mwisilamu ila ana lake jambo, natoa onyo acheni kuchimba mambo ambayo yanaweza kuvuruga amani ya nchi. fuata mnachokiamini msichezee imani za watu.
ReplyDeleteHivi wewe kweli una imani ya dini hiyo inayo ruhusu mitala?. Mwenye imani ya dini hatotaka kutafuta ushauri kwenye mitandao, imani yako ya dini itakupa jibu moja kwa moja ya nini cha kufanya juu ya hili.
ReplyDeleteNaomba ujiulize au kujijibu masuala Yafuatayo; Je dini yako inakuruhusu kuchangia shamba lako? Je na wewe upo ktk kutoka nje ya ndoa hizo? Je uliyo waoa nao wana imani safi ya dini yako hiyo (to mean u are sharing the same religious values)?. Naamini kwa muongozo wa dini hiyo inayoruhusu mitala-kama kweli wote mnafata misingi iliyo ndani ya dini hiyo basi hilo ulilolisema halitokuwepo, lakini kama wote mliivamia tu imani ya mitala kwa kukidhi mahitaji yenu fulani (kila mmoja)na hamfuati imani nyingine zilizo ndani ya dini hiyo (to mean maadili na maaamrisho ya dini hiyo) basi hayo yatawakuta sana.
Hivyo basi tatizo hili haliwezi kutoweka either Kwa kuwaacha au kuwaolea mwenziwao, instead tatizo litatoweka kwa kuanza kusafisha imani zenu za kidini na muanze kufata maamrisho yote ya imani hiyo bila kuchagua kipi ni suitable kwenu.Anzeni mafundisho ya imani ya dini hiyo (though hukutaka kuitaja ni ipi).
Nimependa pale uliposema "hawa wawili nilio nao naona nawamudu" ha ha ha! unawamudu? kama unawamudu mbona wana vibuzi?
ReplyDeleteNakubaliana na mdau hapo juu, wewe unafanya dhihaka na dini za watu tu, kwani kama ni muislamu unajua tu kuwa kwa kuwa wanatoka nje ya ndoa suluhisho ni talaka tu, sasa unakuja kuuliza nini hapa?
Nakuonea huruma, but I cant resist telling you; serves you right, what is good for the goose is good for the gander.Hii ruhusa ya kuoa wake wawili au watatu iliwekwa wakati ilipowekwa kwa sababu maalum,kutia viraka matatizo yaliyokuwa ya wakati ule. Haikuwekwa kusatisfy your jando.
ReplyDeleteKimsingi dini ya kiislamu inaruhusu kuoa mke zaid ya mmoja kwa sharti la uwe na uwezo wa kumhudumia katika nyanja zote ikiwemo kufanya tendo la ndoa pamoja na huduma zingine ambazo mwanaume anapaswa kumpa mke wake. Wewe utakuwa umeangalia kipengele cha uwezo wa kiuchumi upande wa tendo la ndoa hujaangalia. Inawezekana wewe kama mwanaume unaridhika inapokuja suala la tendo la ndoa kwa kuwa
ReplyDeleteNaungana na Anny. wa "Wed May 30, 08:48:00 AM 2012" Kumbe ulioa kwa sababu wanawake wazuri ni wengi"! Kwa taarifa yako hata wanaume wa shoka wapo wengi pia. We unavyowagawa kimapenzi unadhani nini. Eti wanapendana, hakuna urafiki kwenye mapenzi! Lol, imekula kwako, we si unasema imani yako inakuruhusu, endelea kuwavumilia baba, unalia nini. Wanaume acheni tamaa kisingizio eti imani, kama we unakula huku na huku kwa nini na mkeo asiitafute hiyo raha! Pole ndugu yangu, nenda kwa viongozi wako wa dini watakusaidia zaidi, kwa maana kuwaacha siyo solution wala kuwaolea mke mwingine siyo jawabu, na yeye anaweza kuwa kama hao wenzie tu. Angalia baba wasije wakakutia wadhimu bure!
ReplyDeleteMie nakushauri uwaache wote kwani kama warembo unaowataka wapo telee na kila sekunde wanazaliwa chagua wengine baba.
ReplyDeleteNA WEWE TAFUTA MUME KAMA UNAWAONEA WIVU WAKO ZAKO.
ReplyDeleteUshauri wangu na wewe tafuta mwanamke buzi wako mzuri kuliko wao mtafune vizuri na hakikiksha wao wanajua.Halafu waache hao wake zako tunza watoto na kula raha maisha ni mafupi sana ndugu yangu ukiwa na imani ya zamani ya kuvumilia katika ndoa watakuua na ugonjwa.
ReplyDeleteMi nakushauri ujinyonge. Dini yako inakufundisha kuwa kigezo cha kuoa mke zaidi ya mmoja sio kwa ajili ya kukidhi matamanio yako bali kutoa hifadhi (social Protection) kwa wajane. Mtume hakuoa mke zaidi ya mmoja kwa kufuata matamanio.
ReplyDeleteHalafu wewe inaelekea hujui hata hiyo dini unayoizungumzia. Mwenye dini haombi ushauri wa mambo ya chumbani hapa. Wewe inaelekea umelewa tu hujui unalolifanya au labda UNAFANYA MZAHA NA IMANI ZA WENZIO. JIHADHARI.
lAANTULLAH ALA LKAARIN. AMIN.
ReplyDeletehizo comments zinatosha mkuu, sasa changanya na zako, umemaliza kazi
ReplyDeletehii ni selfishnesh za wanaume kusingizia dini(imani),naamini kwamba dini inasema uongeze mke ya kwamba kumsitiri yule mwanamke kwa mfano kama mgonjwa n.k lakini nyinyi mnafanya kwa starehe zenu. na kama ulivyojieleza wanawake wengi sana na warembo, hapo tu inaonyesha ni tamaa imekuponza. watanashati wanakusaidia kukumbatia kwani every woman needs aman all night long, na sio siku za zamu tu.
ReplyDeleteTATIZO KUBWA LA DINI YETU YA KIISLAMU HATUSOMI QURAN WENYEWE TUNANGOJA MAWAIDHA KUTAFSIRIWA NA KULISHWA MANENO YENYE TAFSIRI ZA ANAETOA TAFSIRI.TUJITAHIDI TUSOME WENYEWE QURAN NA KUIELEWA.SIO LAZIMA IWE IMEEANDIKWA KIARABU SASA HIVI ZIPO ZA KISWAHILI NA KIINGELEZA NYINGI.TUSOME WENYEWE JAMANI.HUWA NAPATA SHIDA SANA KUONA KUWA KILA NYUMBA YA MKRISTO INA BIBLIA WAKATI MWINGINE ZAIDI YA MOJA, LAKINI TUKIACHA UNAFIKI KWA SISI WAISLAM KUNA NYUMBA HAZINA WALA HAZIJAWAHI FIKIRIA KUWA NA QURAN NYUMBANI ZAQIDI YA KUIONA MSIKITINI SIKU YA IDD.HUKU KUKARIRISHWA TU BILA KUTAFUTA MUDA TUKASOMA WENYEWE NDIO MATATIZO HAYA YANAYOTUKUTA.UKISOMA QURAN VIZURI UTAGUNDUA NI KAMA TUMEKATAZWA KUOA MKE ZAIDI YA MMOJA.KWAKUWA MASHARTI YAKE BINADAMU WA KAWAIDA HUWEZI YATIMIZA......HAYA TUENDELEE KUWA WABISHI TU NA KUJILINGANISHA NA WENGINE TUTAONA MWISHO WAKE
ReplyDeleteMapenzi ni ya wawili tu, hayagawanyiki na ndi maana penye mapenzi ya kweli, wake wenza huchukiana. Ukishaona wake wenza wanapatana basi ufahamu fika kila mtu ana wake wa moyoni anayempenda, hivyo wewe ni wa ziada. Ndio maana wao wanapendana. Mkome kuoa wake zaidi ya mmoja hivyo nasi tunavyoumia, sasa wewe kushare hutaki wenzako ndio ulitaka wakae wanakusubiri wewe upange ratiba. Ningewajua hao wanawake ningewapa zawadi. Wamefanya vizuri sana!!! Ati unasema wanawake wengi na wana uzuri na mvuto tofauti, na wake zako pia wanaona wanaume ni wengi na wana mvuto tofauti!!
ReplyDeleteBora yule muheshimiwa wa wizara nyeti kule visiwani amejiamulia kuoa na kuacha kila kukicha.
ReplyDeleteAliyedumu nae mpaka sasa ni mke ambae ki umri ni mkubwa kuliko yeye mume, wengine anaoa miezi sita, miwili anatoa talaka anaoa mwingine.
Yaani kawafanya wanawake kama disposable item flani.
Sasa braza na wewe kama unaweza fanya hivyo, ila ndio uangalie utakua na watoto kila kona,mwenzio anao bara na visiwani.
Tamaa na Urohoo mtuupu AIBUUUUUUUUUUU. Sasa ukapime gono ukisubiria ushauri inaweza ikawa too late. halafu ukitoka clinic nenda nyumbani ukasikilize moyo wako unasemaje, any ways sidhani decision yeyote utakayo make ita washtua wakeo kwajili hadi wakatoka nje kuzini 'pendo limeshakufa (broken mirror)' utawaumiza watoto tu. Make sure unawaplz watoto because you dont want to lose them too. Unpaliwa pole.
ReplyDeleteHahaha babuuu utalea tu hao watoto hat kam asi wako, kitanda hakizai haramu, si binadamu kama wewe na hata kama baba zao ni binadadamu wengine, umelikoroga, utalinywa hilo, wewe ulijiona kidume, nao vijike hapo chacha ngoma dro!!!!
ReplyDeleteWape talaka wote hao kwakweli sio wazuri sisi mungu ametupa ruhusa kwa maana yake sasa wanapingana na wewe na pia wanapingana na mungu!
ReplyDeleteKaa nao pamoja waeleze umeshajua dili lao, wasisitizie hatari ya kuwa na vibuzi nje maana magonjwa ni mengi, mtaacha hao watoto wateseke bure. Miaka mingi iliyopita mtaani kwetu kulitokea kama ulivyoeleza huyo baba alikuwa anafuata samaki somewhere huku nyuma wanawake walikuwa wanajinadije? alipogundua aliwaacha wote na kuoa mke mwingine ambaye mpaka miaka ya hivi karibuni alikuwa naye.
ReplyDeleteBro pole sana lakini UKIYAVULIA MAJI NGUO HUNA BUDI KUYAOGA, Je unauhakika ni wake wote wanavibuzi nje au ni mmoja tu? na kabla hujamuoa bi mdogo je bi mkubwa alikuwa anakibuzi pia au ulimpa fursa ya kuwa na kibuzi baada ya wewe kuoa mke mdogo? mie naona wewe hujui unataka nini katika maisha yako, nenda KITUO CHA ANGAZA ukajianglie afya yako wewe na wake zako then nenda kafanye DNA TEST kwa watoto wote upate uhakika wangapi ni wako na wangapi si wako unaweza kujikuta unalea watoto wa wanaume wenzio na wao itakuwa wanajua ila wana kufanya wewe jinga lao na bwege mtozeni, IMEKULA KWAKO BRO, umeyataka sasa wacha yakukute.
ReplyDeleteuroho mtupu, umepaliwa sasa. kwanza kapime ukisubiria ushauri inaweza ikawa too late.Wakati upo clini fikiria uamuzi wa moyo wako,any ways decision yako sidhani kama itawashtua wake zako, hadi wakaenda nje 'huna kitu babaa KWISHAA' utawaumiza watoto tu. Sasa ndo uwatunze watoto usije ukawapoteza nao pia. Pole, lakini am sure unajua kila ndoa ina matatizo yake we umetaka mbili sasa zimekutokea puani. (fikiria kabla hujafanya)
ReplyDeleteAssalam Alayku Ustaadh:
ReplyDeleteKila kitu kina mtihani wake
1.Kuoa kuna mtihani wake,
2.Kuoa zaidi ya mke mmoja kuna mtihani,
3.Kutokuwa na ndoa kuna mtihani pia,
KUOA KUNAHITAJI UWE NA VIGEZO VYOTE VIKIWEMO VIKUU VITATU (3) CHINI.
1.UWEZO
2.UADILIFU KWA WEMA KWA WAKEZAKO
3.UWEZO WA KIMWILI (URIJALI)
INAONYESHA MAALIM UNA VIGEZO NO. 1 NA NO.2 SASA NO.3 HUNA NDIO MAANA PANA WANAOKUSAIDIA!
WAONE MASHEIKH WAKUPE MWONGOZO!!!
kwa kweli nipenda style ya wake zako maana waswahili husema mkuki kwa nguruwe, na al kisas haki wengine wasema revenge is sweet you better serve hot so enjoy maana nyie kina kaka wa kiislam mko so selfish, iman za dini ziko nyingi lkn hii kwa vile inaridhisha nyoyo zenu ndio mwaipenda na mtenda akitendewa hujihisi kaonewa, I love your wives they deserve medals lol
ReplyDeleteMmm kazi kweli kweli.
ReplyDeleteSheikh wetu pole sana,
ReplyDeleteKwanza kabisa kwa dalili ya kupigiwa wote wawili (2) ni kuwa umesomeka kama hivi:
1.Uwezo wako kimwili upo chini, ingekuwa mmoja inekuwa labda ni hulka zake tu sasa wote wawili??,,,(ni kuwa ina dalili hawatosheki na huduma yako ya kijamii au unyumba)
2.Kama unapigiwa wote wawili (2) ni sawa kuwa kama 'unayechapwa' ni wewe sasa sio wao!
3.Kwa kawaida mwizi wa Gari akipata nafasi anaweza kuamua kuendesha gari kwa 'kinyume nyume' kwa Gea za rivasi, wakati wewe mwenyewe hata kidogo huwezi kuthubutu kufanya hivyo!
4.Ni nafuu kufilisika mali yote uliyonayo (Nyumba mbili na fedha zako zote ukabaki kapuku) kuliko kupigiwa tena wote Wake zako wawili (2) kwa mpigo!
POLE SANA USTAADHI !!!
Ilisemwa maradhi yote ugua lakini kuchacha usiombee,
ReplyDeleteLakini afadhali ya kuchacha kuliko Wake zako tena wote wawili (2) kupigiwa mshipa!
Sio bure!
ReplyDeleteUstaadh wetu kufungwa mabao mawili kwa mpigo Uwanja huo huo inawezekana na wewe ni mwingi wa habari zaidi ya hao Wake zako wawili inawezekana wamebaini una Kimada pia na sasa na wewe unakomolewa!
Assalam Alaykum,
ReplyDeleteUstaadh wetu na Wadau wote NDIYO NI SEHEMU YA DINI YA KIISLAMU KUOA MKE ZAIDI YA MMOJA HADI WANNE.
LAKINI CHA KUSIKITISHA WENGI WANAOOA WAKE ZAIDI YA MMOJA HUOA KWA TAMAA NA UCHU WA WANAWAKE BADALA YA ZAIDI YA MISINGI YA KIIMANI!!!
Zaidi ya Imani,
ReplyDeleteWapo wanao oa mke zaidi ya mmoja kwa KUTAKA SIFA ILI WAONEKANE WAO NI VIJOGOO!!!
Asalaleeee inauma sana!
ReplyDeleteHapo ni sawa sawa na mipira miwili imepigwa na mabao mawili yanaingia Golini kwa mpigo wewe ukiwa Kipa Langoni !!!!.
Bora kufilisika mali zote manyumba na fedha zako zoooteee kuliko kupigiwa 'PU(W).....BU'
Sheikh,
ReplyDeleteUnaonyesha uwezo wako upo chini,,,tafuta ukombozi isizidi kuadhirika mbele ya wake zako,,,usifikiri ukiwa zamu nyingine?, inaweza kutokea kufikia ukaja kuchapiwa wewe ukiwa hapo hapo nyumbani!
Heshima ya ndani kwa dalili hizo imeshashuka!!!
Waone Wataalamu wa miti shamba !
Ahhh uchungu jamani!
ReplyDeleteKwa kufanyiwa namna hii na Wake zangu wawili?
Bora nikate kiungo changu cha siri!!!