Kikosi kamili cha timu ya waTanzania DMV wakiwa na mdhamini mpya wa timu hiyo Mbunifu wa mitindo ya Kwetu Missy Temeke, akiwana na shabiki Didi Vava, katika uwanja wa Greencastle, uliopo Burtonsville, Maryland

Tanzania DMV iliweza kutinga tena uwanjani kucheza mchezo wake wapili na timu ya Ethiopia, hadi mpira kumalizika timu hizo zimetoma 0-0 katika  mpango mzima wa ligi ya 2011 Diaspora World Cup zinazoendelea katika viwanja vya Hyattsville na Germantown jijini Maryland Nchini Marekani.
Mchezaji wa timu ya Ethiopian akipambana vikali na Yousouf Godson Liuzinho, kipindi cha kwanza katika ligi ya 2011 Diaspora World Cupkwenye kiwanja cha  Greencastle, kiliopo Burtonsville, Maryland.
Wachezaji wa wa timu ya Ethiopia wakiwania Freekick katika dakika ya 62 ya mchezo huo.
Mchezaji wa timu ya Ehiopian  akijaribu kumpita beki wa timu ya Tanzania,  Emanuel Oumogbao katika mchezo wa pili wa ligi ya 2011 Diaspora World Cup kwenye kiwanja cha  Greencastle, kiliopo Burtonsville, Maryland.
Jukwa la mashabiki wa timu ya Watanzania DMV, wanne kutoka kushoto akiwa Rais wa Jumuiya ya Watanzania DMV pia alihudhuria katika mpambano huo.
Didi Vava, kushoto akiwa na Sharif Qullatein, Dogo Hudhaifa Shatry, na Mmiliki wa blog ya swahilivilla Abou Shatry, wakiwa katika jukwa la wapenzi wa timi ya waTanzania DMV.
Mdhamini wa timu ya waTanzania DMV ambae ni mwana mitindo na mbunifu wa mitindo ya Kwetu Fashion Design, Missy Tetemeke akiwa na Bendera ya Taifa.
Benchi la timu ya wa Ethiopia wakiwa kama mtu nane njee na ndicho kilicho wasaidia kutoka bila kufungana na Timu ya waTanzania DMV. 

Picha na habari kutoka kwa mwana blog wetu Abou Shatry wa http://swahilivilla.blogspot.com/

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 13, 2012

    hiyo timu hapo katika picha ya pamoja inamana kwakuwa wanaishi nje hawajui hata bendera ya taifa inavyokaa?rangi hizo hazikai tu kunainayotangulia chini na inayokuwa juu.jamani uzalendo zero ingekuwa bendera ya afghanistan msingekosea kuishika

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...