Dr Engineer Shaban Kachua mwenye joho lenye rangi nyekundu na Bluu akiwa na waafrika wenzake wakati wa alipotunukiwa Shahada yake ya Udaktari wa falsafa Nchini Canada.
Hapa Dr Kachua akiwa amekaa mstari wa mbele kabisa na wahitimu wenzake.
Mama Mzazi wa Dr Kachua (mwenye blauzi nyeusi), akiwa na Mama mkwe wake, wote kwa pamoja walishiriki katika tukio la kihistoria la kutunukiwa Shahada ya PHD kwa mtoto wao nchini Canada.
Mrs Dr Shaban Kachua (Jemima) akiwa na furaha pamoja na watoto wao walishiriki katika shughuli ya kutunukiwa Mume wake shahada ya udaktari wa Falsafa (PHD).
Kwa sasa Dr Shaban Kachua anaishi Nchini Canada pamoja na familia yake. Sisi kama watanzania wenzake tunapenda kumpongeza sana kwa kuweza kuipeperusha vema Bendera yetu, tunapenda kumshauri pia, elimu yake hiyo aweze kuitumia pia kulisaidia Taifa lake la Tanzania hasa katika nyanja hiyo ya Sayansi, kwa kutambua zaidi tuna upungufu mkubwa wa wanasayansi katika Taifa letu.HONGERA SANA
hongereni Jemina na familia yako...
ReplyDeletensubisi - dar!
Jemima hongereni sana
ReplyDeletebeda - dar
insikitisha kuona mtu anasoma miaka kadhaa kisha badala ya kulisaidia taifa lake anasaidia mataifa ya wengine-brain drain
ReplyDeleteKwanini sisi ni limbukeni wa nchi za watu, na kwanini tusijenge nchi zetu kwanza?
Mtu akisikia ulaya au america basi anaweza kuuza nchi kwa dhaman ndogo mno. Tujenge nchi yetu kwanza, uwezo tunao, nguvu tunazo, nia hatuna.
Good Job buddy,on a different note, I will start to call my wife Mrs Dr Gangwe Bitozi, smirk.
ReplyDeleteDr Gangwe Bitozi.
Uncala sasa unatutia haibu what this "Dr engineer????" ukimwita Dr...., or engineer.... inatosha. Punguza uswahili.
ReplyDeletenahitaji kusoma masters nje ya nchi ktk fani ya mhandisi ujenzi.nataka kusaidiwa kama kuna uwezekano wa kupata scholarship/sponsorshp...ijuvye hapa loptz@yahoo.co.uk
ReplyDeleteMkuu wa kazi SHABANI hongereni sana kaka tunajivunia kuwa na wewe mtu, nimefurahi sana kuona picha ya mama na GEMINA na watoto lol
ReplyDeletekaribu Tanzania jimbo la Tanga mjini ni kama lipo wazi tuu uje tukupe lile jimbo MKUU
PETER SHIRIMA
Hongera sana Dr. Kachua. Salamu kwa familia pia.
ReplyDeleteBendera
Hongera san Dr. Kachua na familia yako
ReplyDeletehongera sana Mkuu.duuh Wasomi wote wenye asili ya Tanzania kama wangekuwa na moyo wa kutoa ushauri au kufanya kazi za kujitolea wakati wa likizo zao Bongo,tungefika mbali sana.Bahati mbaya huo moyo haupo kwa watu wenye asili ya Tanzania au WaTanzania,ni wanchoweza ni kuilaumu Serikali usiku kucha.
ReplyDeleteHongera sana Dr Eng. usisahau tu mambo ya slab pale foe!
ReplyDeleteNdugu mwandishi wa Fri May 18, 02:58:00 PM 2012. Punguza jazba, kila mtu anaamua kuishi kulinga na utasi wake. Huko kujenga taifa unakokusema ina maana mpaka leo hujajua hilo taifa lina wajenzi wake? Ndugu yangu kama wewe hujapata nasfasi ya kufika majuu basi waache waliofika waishi watakavyo. Tusipangiane maisha, just put your comment with regarding the guy success and not go further than that. I think it is clear and u'v understand. God bless you kwa maisha uliyochagua wish u success
ReplyDeleteBaada ya shule kuisha, hapo ndipo Maumivu ya Kichwa huanza Pole Pole.
ReplyDeleteMaana Recession ndo inazidi kushika hatamu kwa kasi ya ajabu.
Kasheshe la Nigeria ni kuwa na wasomi mpaka ngazi ya Profesa lakini wako tu huko huko majuu wakibeba mabox.. We bwana rudi tu huku tujenge nyumbani kwetu hata kama utafundisha chekechea itasaidia maendeleo ya bongo
ReplyDeleteMdau wa Sat May 19, 06:14:00 PM 2012
ReplyDeleteumezungumzia Nigeria, sasa huko wana wasomi kibao lakini hakuna ajira. Hivyo wenye PhD na hao Maproffesor ndiyo mainjinia wa kutengeneza Orginised Crimes na Fraud kwa kutumia internet. Tanzania ya leo njia ni hiyo hiyo