Tawi la CHADEMA Washington DC.

Kwa niaba ya uongozi wa tawi la CHADEMA Washington DC. napenda kuchukua fursa hii kutoa shukrani zangu za dhati kwa watu wote walio hudhuria ufunguzi wa tawi la CHADEMA uliofanyika Tarehe 27 May 2012 Washington DC nchini Marekani katika ukumbi wa Mirage Maryland.

Aidha nawashukuru wageni waalikwa, Naibu katibu mkuu wa CHADEMA na Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mh. Zitto Kabwe, Mbunge wa Viti maalum kutokea Jimbo la Kwimba Mama Leticia Nyerere, Mbunge wa Iringa mjini Mh. Peter Msigwa, Mbunge wa Arumeru Mashariki Mh. Joshua Nassari na Mbunge wa Viti maalum kutokea Zanzibar Mh. Mariam Msabaha kwa kutumia muda wao wa thamani kukaa na watanzania tuishio Marekani kubadirishana mawazo na kutuelezea mstakabari wa nchi yetu (Mama Tanzania) kijamii, kiuchumi na kisiasa.

Mwisho napenda kuwashukuru watanzania wote walio hudhuria mkutano huu. Kwa kweli tumefarijika sana kuona utayari wa mioyo yenu kutaka mabadiliko (M4C) na uwazi wa kujielezea mawazo yenu bila kua na hofu.

MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI CHADEMA.

Asanteni sana kwa ushirikiano usio na mipaka


Katibu Mkuu-CHADEMA WASHINGTON DC

Liberatus Mwangombe

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 31, 2012

    Mnashuruku nini wakati kazi ngumu mnayo mbele?

    Kabla ya kutoa shukrani mjipe pole kwanza!

    Mwana CCM
    Dar Es Salaam

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 31, 2012

    wewe mwana ccm hujui unalosema sijui nakujibu kitu anyways kaa na huo mkokoteni wenye tetenasi utajibeba I hope uko juu ya 55yrs
    Mwana CHADEMA FOREVER

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...