Baadhi ya wachezaji wa Simba SC wakishangilia pamoja na kombe lao wakati wakipita katika mitaa ya jiji la Dar es Salaam jana.
TIMU ya Simba SC ya jijini Dar jana ilisherehekea ubingwa wake wa 2011/2012 pamoja na mashabiki wake katika ukumbi wa burudani wa DAR LIVE. Sherehe hizo zilitanguliwa na msafara wa magari, pikipiki na watembea kwa miguu ambao walianzia safari yao makao makuu ya klabu hiyo Mtaa wa Msimbazi na kupitia mitaa kadhaa ya jiji kabla ya kumalizikia katika ukumbi wa Dar Live.
Katika msafara huo wachezaji wa Simba walikuwa katika lori la wazi lililopambwa bendera na vitambaa vya rangi nyekundu na nyeupe huku wakiwa na kombe lao walilolibeba.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...