Mkurugenzi Mkuu wa SSRA bi. Irene Isaka akizungumza na wanahabari juu ya utolewaji wa miongozo ya uwekezaji wa sekta ya Hifadhi ya Jamii.Kushoto kwake ni mkuu wa kitengo cha mahusiano na uhamasishaji Bi. Sarah Kibonde Msika
Wanahabari nawajumbe wa menejimenti ya SSRA wakimsikiliza Mkurugenzi mkuu wakati akiwasilisha mada.
Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), leo hii imetoa miongozo ya Uwekezaji kwa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.
Akizungumza na wanahabari Mkurugenzi Mkuu wa SSRA Bi. Irene Isaka alisema “ miongozo hiyo imetengenezwa chini ya kifungu nambari 26 (2)cha sheria ya Mamlaka, ambacho kinataja wazi kuwa “Benki Kuu kwa kushauriana na Mamlaka ya Usimamizi na udhibiti wa sekta ya Hifadhi ya Jamii-SSRA ‘’ itatoa miongozo ya uwekezaji ili kuhakikisha Mifuko ya hifadhi ya Jamii inawekeza katika maeneo ya vitega uchumi yaliyo bora na salama”.
‘Miongozo hiyo itatumiwa na Mifuko yote ya Hifadhi ya Jamii nchini ‘yaani Mifuko iliyo chini ya Mfumo wa lazima /Mandatory na ile yote chini ya Mfumo wa ziada/ Supplementary Schemes za Tanzania Bara.Miongozo hiyo imeanza kutumika rasmi kuanzia tarehe mosi Mei mwaka huu.
Lengo kuu la miongozo ya Uwekezaji ni kutoa miongozo kwa Wajumbe wa Bodi za mifuko ya Hifadhi ya Jamii,ili kufanya maamuzi ya uwekezaji yanayoendana na utawala bora wenye kuzingatia, kanuni, taratibu na sheria za uwekezaji.
Miongozo wa uwekezaji inalenga kufanya mambo yafuatayo:
i. Kutoa Viwango vya uwekezaji wenye tija katika maeneo mbalimbali ili kuepukana na upotevu wa rasilimali za mifuko zinazowekezwa.
ii. Kulinda na kutetea haki na maslai ya wanachama.
iii. Kuhakikisha kuwa Mifuko inakuwa na Uwezo wa kutosha kulipa mafao bora ya wanachama endapo yatahitajika
iv. Kuhakikisha kuwa kuna mfumo wa utawala bora, ambao utawezesha mifuko ya hifadhi ya Jamii kufanya uwekezaji wenye tija.Mfumo bora wa kiutawala utawezesha mgawanyo mzuri wa kazi,uwekezaji wenye ufanisi na uwajibikaji kwa wale wote wenye majukumu ya uwekezaji, endapo wataenenda isivyo.
v. Kuhakikisha kuwa kuna kiwango kikubwa cha uadilifu,utendaji kazi wenye tija na Ufanisi,ubunifu, uwajibikaji kwenye masuala yote ya kiutawala na uwekezaji wa Mifuko.
Miongozo ya uwekezaji inataja waziwazi majukumu ya Bodi za Mifuko ya Hifadhi ya Jamii katika kuhakikisha kuwa kila mfuko unakuwa na sera yake ya uwekezaji ambayo itazingatia miongozo tajwa na ripoti ya mtadhimini wa Mifuko/ actuarial valuation.
Vile vile miongozo inataja wazi ni nani watakaokuwa wajumbe wa kamati ya uwekezaji ya mifuko kwani ni muhimu kwa kila mfuko kuwa na kamati hiyo , na muda muafaka wa kuanza kutumika kwa muongozo huu, taratibu za kuwasilisha mabadiliko ya sera za uwekezaji nayo yameelezwa kwa kina.
Huo mwongozo kama hauja ainisha jinsi mwanachama atakavyonufaika na faida inayopatikana kwenye uwekezaji bado ina upungufu. Inahitaji marekebisho.
ReplyDelete