Habari kaka Michuzi,
Naomba sana uniwekee swali langu hili kwenye blog yetu ya jamii.
Wadau,
Je, kuna mtu yeyote aliye na ushahidi wa kumfahamu mtu aliyedhaniwa amekufa kumbe hajafa? Yani mtu alichukuliwa na wachawi (msukule).
Nimekua nikiona habari nyingi za mikasa kama hiyo , zikidai kuwa mtu alidhaniwa kufa na kuzikwa but akarudishwa kwa nguvu za  Mungu( sala/maombi) au waganga.
Naomba kama kuna mdau yeyote anayefahamu  au aliyeshudia hii mikasa aniambe.
Asante sana.
MDAU E.H.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 01, 2012

    Hakuna kitu kama hicho wewe Mdau. Ni uzushi tu, watu wanazusha tu mpaka watu kama nyie mnaanza kuamini.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 01, 2012

    Mara nyingi hizo nimPromotion za Makanisa ya aina ya 'Kibwetere' aliyefanya mavituz yake huko Uganda na yule jamaa wa Davidians kule Arizona Marekani.

    KIFO HUPANGA MWENYEZI MUNGU, KIKITOKEA HAKUNA WA KUREJESHA MAISHA KILICHOBAKI NI KUTOANA DAMU TU KWA MIUJIZA ISIYOTEKELEZEKA NA USANII KUPITA MAELEZO!

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 01, 2012

    Mara nyingi hizo nimPromotion za Makanisa ya aina ya 'Kibwetere' aliyefanya mavituz yake huko Uganda na yule jamaa wa Davidians kule Arizona Marekani.

    KIFO HUPANGA MWENYEZI MUNGU, KIKITOKEA HAKUNA WA KUREJESHA MAISHA KILICHOBAKI NI KUTOANA DAMU TU KWA MIUJIZA ISIYOTEKELEZEKA NA USANII KUPITA MAELEZO!

    ReplyDelete
  4. MATANGALUMay 01, 2012

    The clue is in the heading of your thread. The word "uzushi".

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 01, 2012

    Ukosefu wa Elimu mkuu..Hakuna kitu cha namna hiyo..Juzi vyombo vya habari vimeripoti huko mkoa mmoja wa Nyanda za juu kusini habari ya kusikitisha sana..sana.Mtu mmoja amezikwa na kufukiwa akiwa hai...ndiyo akiwa hai.Kisa?eti 'kamuua' mtoto wa kaka yake.Tangu nimezaliwa sijawahi kusikia mtu akizikwa akiwa hai..nilitetemeka mwili mzima

    David V

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 01, 2012

    we unayetaka kufahamu ,mambo hayo,je ? unasababu za kishilikina au una andika kitabu? yaani sikuelewi !!! kitu gani kikubwa unachatafuta,je? kama mimi nitasema nimewahi kushuhudia ,hii itakufanya na wewe uamini ?? wangapi wamesema nwamaona msalaba ukutani unatikisika au picha ya Mariam mama yake na Yesu inatoa machozi ndani ya kanisa ukutani !!! wewe umeamini habari hizo ??? anyway sijui wadau watasema je ,lakini mimi naona swali lako nin kweli la uzushi,lakini michu hana hiyana kakuwekea kwenye blogi yetu tukufu,lakini kumbuka ,kuna akina David V wanaweza kukutoa lesi. Zebedayo wa Zebedayo ( Mwanza) ongelea mambo ya maana kama kung,olewa kina Mkulo n.k hizo ndiyo mada mzuri.

    ReplyDelete
  7. Mdau E.
    Wacha nikupe mchapo wa hiyo sehemu unayouliza kama ipo.Mimi hawajanichikuwa nilikwenda mimi mwenyewe kwa miguu, sio mbali hivyo.Ilikuwa kwenye miaka ya 1527 na nikabomoa na kuchoma moto hizo sehemu zote na nikahakikisha hazirudi.Kwa hiyo kama wakikwambia bado zipo waongo hao.
    God Bless.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 01, 2012

    yah ni kweli imeshatokea..kwa baba yangu mdogo amabe alikuwa bodyguard wa raisi mwaka 95.alikufa...lkn alikuwa amechukuliwa kichawi zaidi..wakati wa usiku alikuwa anawatokea familia yake..mara kwa mara..familia nayo ikaamua kwenda kwa waganga..tofauti tofauti..na wakawaeleza the same story kuwa baba mdogo hajafa kawekwa msukule...na yupo sehemu flan..na waganga wakasema kuwa hawezi tena kurudi ana atakayefanya hivyo..basi atakufa yy..na tokea..kipindi hicho alikuja kufa ki kkweli kweli mwaka..2007..na waganga walipa simu..na kutuambia kuwa mzee wenu ameshakufa kabisa sasa hv na kazikwa sehemu flan...na tulipoenda na kufukua kweli tuliiona maita yake...ilisikitishsa.na waganga walituambia mtu aliyefanya hivyo na hadi leo yupo hai..

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 01, 2012

    Kwishaona mbusi nabatasamu,...Mbado, Nyau Anamwanya,...Mbado, Huajaona hujaona,...Mbado!

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 01, 2012

    hiyo ipo mdau ila kumrudisha kuwa hai haiwezekani ila unawezakumtoa kwenye hiyo himaya ya wachawi akawa himaya nyingine ambayo atakuwa hamilikiwi na hao watu wabaya vilevile kazi ipo kumtoa si ajabu unayetakakumtoa hata na wewe rohoyako ikachukuliwa maana hawa wachawi ni watu wabaya lakini kwa karama na kudra za mwenyezi mungu unafanikisha mimi ninayeandika nimeishawatoa wawili na mmoja kumzuia asichukuliwe ukitaka kujua zaidi nipigie 0787450966 hata huyu aliyekufajuzi huyu maarufu naye nikweli kachukuliwa lakini mwenyekiti hiyo sio abrakada

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 01, 2012

    hakuna hicho kitu, mtu aliyekufa kurudishwa kwa aina yoyote ile kuna wakati watu hukosea na kuzika mtu mwingine alf yule aliyezaniwa akarudi watu wakjua kuwa kafufuka

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 01, 2012

    ndugu mdau kwa imani yangu huwa siamini hayo mambo no mambo ya kishirikina kwasababu wanafikiri kila kt kibaya ametumiwa na mganga na ndio wanavyodanganywa wakienda huko kwa waganga wao.

    ReplyDelete
  13. Huwa hawarudi, ni story tu za watu na watu kutokua na uelewa na kudanganyika na mambo ya dini au kiganga. Binafsi sijawahi ona mtu akirudi hata kusikia pia kwamba fulani alofariki akarudi sijawahi kusikia so ni uongo tu.

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 01, 2012

    Freemasonism

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 01, 2012

    Mi nina ushaidi, si katika suala lako bali katika suala jingine. Yule mchezaji wa mpira kule Uingereza jina lake Muamba, inasemekana alifariki kwa dakika kama 78 na sasa anaishi. Je, hii inawapa mwanga wowote? Kufufuka kwa mtu ni mapenzi ya Mungu. Hakuna mtu anayeweza kufufua mtu kama Mwenyezi hakupenda. Ruksa hutoka kwa Mwenyezi Mungu, tena kwa nguvu zake Mwenyezi Mungu na si kwa binadamu asiyemcha hata kumjua Mungu. Ila wachawi wapo na wanawanga pia. Ila hawawezi kushindana na Mwenyezi Mungu.

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 01, 2012

    Ndugu Yangu Cha Muhimu Soma Vitabu Vya Dini na Muombe Mwenyezimungu Jiweke Mbali na fikra za vitu kama hivyo visikuumize kichwa wakati kuna mambo Mengi ya kufanya Duniani hasa Elimu ya Dunia na Sayarini na Akhera Hao wenye Imani za Kichawi tuepuke nao kabisa Mwenyezimungu tu ndio Mjuwa wa mambo na mwenye uwezo wa kila kitu wengine hawana uwezo wa Mwenyezimungu. Washindwe kabisa katika Nguvu za Muumba. MZ

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 01, 2012

    Mimi newahi kusoma watu walio kufa na kufufka kaiti hizi blog hapa chini

    http://nukta77.blogspot.com/2009/10/alikufa-na-kuzikwa-2005-akutwa-yupo-hai.html

    http://www.mwananchi.co.tz/news/3-habari-za-mikoani/14135-aliyezikwa-mwaka-1999-apatikana-hai-z-victoria.html

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 02, 2012

    Mfano mdogo tu, hebu yateme mate yako chini (Ardhini) na kisha jaribu kuyarejeshea tena kinywani uone kama yatarudi au laa! Hapo utapata jibu.

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 02, 2012

    wewe mdau unayeongelea swala la Muamba ndhani hujaelewa. Moyo wake uliacha ku-pump damu kwa hizo dakika.

    Moyo wako unapoacha kuleta mapigo unaishi kwa muda mrefu mpaka ubongo wako unapokufa kwa kukosa oksijeni, O2.

    Mara nyingi sana watu wengi mioyo yao huacha kupiga kwa dakika wakiwa wamelala hasa watu wenye uzito mwingi.

    Hufi mpaka umekosa kabisa ubongo wako kufanya kazi. You are dead when your brain No Longer is receiving signals from the Heart)au kitaaluma inaitwa, Brain Dead! Hii sio ilivyokuwa kwa Muamba.
    Dr. Me

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 02, 2012

    mm nishashuhudia mtu kafa miaka mingi sana na walishasahau kabisa, akaja kuoneka wakampeleka polisi na akapata ndugu zake, inasikitisha mambo haya sana shinyanga na mbeya ndo wana mitindo hii, na hakimu mmoja alishawahi kupelekewa ushahidi wa maiti ambaye siye mtu lkn ilijulikana mtu kafa, na ile maiti ikachanwa tumboni kukatoka majani ss utasema ni mtu huyo duniani kuna mengi sema ukiyafatilia utaumia kichwa ni kumwachia mwenyewe mjuzi wa yote

    ReplyDelete
  21. AnonymousMay 02, 2012

    Tafiti zinaonyesha kwamba TZ ni nchi ya pili au ya tatu kwa kuamini ushirikina.
    Imani ya uchawi ni kama dini vile. Anayeamini humwambii kitu. Wanaoamini kwenye matambiko ni rahisi zaidi kuamini nguvu za giza. Unaitwa ushirikina kwa sababu mtu huyo huyo utakuta anamwamini Mungu. Anamwomba Mungu amlinde huku amevaa hirizi au pete aliyopewa na maganga imlinde.
    ACHENI KUCHANGANYA MAMBO! mkimuamini Mungu mtegeeni kwa kila jambo - - siyo ooh mpaka nikaombewe na Mchungaji fulani au Shehe fulani!!
    Hili la Msukule tunalisikia tu - linatokea kwenye jamii za vijijini hasa kule wanakoamini sana uchawi.
    Toeni taarifa ya Mr. X, aliyekuwa amepanga nyumba ya mzee Y, pale Temeke/Kinondoni, etc aliugua ugonjwa fulani, akaenda hospitali ya Temeke/Mnyamala/Amana/etc akalazwawodi fulani akafariki tarehe..., mwili wake ukachukuliwa mochwari tarehe...etc, etc, etc. siyo story za ee Jamaa mmoja kule mkoa wa ..blah..blah..blah..
    AMKENI WATANZANIA. FANYENI KAZI, SIYO MNALETA UZEMBE, MNAFUKUZWA KAZIAU HAMFANIKIWI HALAFU MNASEMA .. HAPA LAZIMA KUNA MKONO WA MTU!!!?

    ReplyDelete
  22. AnonymousMay 02, 2012

    Mimi nimewahi kuona hao misukule kwenye TV,CHANNEL TEN niliona kwa macho yangu mchungaji RWAKATARE alikuwa anawatoa hao misukule,kwa ushahidi mzuri nenda kwenye kanisa la mama Rwakatare Mikocheni nawe ukapate ushahidi uliokamilika,watakuonyesha ambao walikuwa misukule

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...