TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua BIBI MWANAHAMISI OMARI KITOGO kuwa MSAIDIZI WA RAIS, HUDUMA ZA JAMII.
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi (KMK) Balozi Ombeni Y. Sefue leo, Jumanne, Mei 8, 2012, mjini Dar es Salaam inasema kuwa uteuzi huo umeanza Mei Mosi, mwaka huu, 2012.
Kabla ya uteuzi wake, Bibi Mwanahamisi Omari Kitogo alikuwa Mkadiriaji Ujenzi Msaidizi (Assistant Quantity Surveyor) katika Kampuni ya COWI, Tanzania.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
8 Mei, 2012
Mkadiriaji ujenzi na huduma za jamii wapi na wapi jamani??????????
ReplyDeleteJamani huku utumishi (civil service) nasi wenye elimu, ujuzi na uwezo tuko twasubiri kupangiwa idara za kazi kuitumikia serikali yetu sehemu yetote serikarini. Huko sekta binafsi wawacheni huko huko kwani sisi tumeshatayarishwa kutumikia serikarini. alexbura dar
ReplyDeleteTatizolenu ni nini? Si na nyinyi muende huko.
ReplyDeleteFrom Assistant Quantity Surveyor to Assistant to the President, Social Services.
ReplyDeletemmh angemtupa kwenye ushauri wa ujenzi, usanifu na majengo.
Wewe mtumishi wa Serikali endelea kukaa ukisubiri Sitting Allowance uone kama utakumbukwa kwenye uteuzi wa aina yeyote.
ReplyDelete