Nahodha wa timu ya mpira wa kikapu kutoka chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) akipokea kombe la ushindi wa timu yake UDOM Social kutoka kwa Mgeni rasmi pichani kati,Diwani wa kata ya Mnadani,Mh.Steven Masangia mara baada ya kuibuka kinara kwenye ligi ya mashindano ya mpira wa kikapu iitwayo DODOMA BASKETBALL DEVELOPMENT LEAGUE 2012,ambayo imefikia tamati leo kwenye uwanja wa mchezo huo uliopo ndani ya uwanja wa mpira wa miguu wa Jamuhuri mjini Dodoma.
Nahodha wa timu ya mpira wa kikapu kutoka chuo cha MIPANGO-Dodoma akipokea kombe la ushindi wa timu hiyo kutoka kwa Mgeni rasmi pichani kati,Diwani wa kata ya Mnadani,Mh.Steven Masangia mara baada ya kuibuka mshindi wa pili kwenye ligi ya mashindano ya mpira wa kikapu iitwayo DODOMA BASKETBALL DEVELOPMENT LEAGUE 2012,ambayo imefikia tamati leo kwenye uwanja wa mchezo huo uliopo ndani ya uwanja wa mpira wa miguu wa Jamuhuri mjini Dodoma.
Pichani kati ni Mgeni rasmi na Diwani wa kata ya Mnadani,Mh.Steven Masangia akizungumza mapema leo jioni mara baada ya kuisha kwa fainali ya ligi ya mchezo wa kikapu iitwayo DODOMA BASKETBALL DEVELOPMENT LEAGUE 2012,ambayo imefikia tamati leo kwenye uwanja wa mchezo huo uliopo ndani ya uwanja wa mpira wa miguu wa Jamuhuri mjini Dodoma,Ligi hiyo ilizishirikisha timu tisa,ambazo ni UDOM,Chuo cha Mipango-Dodoma,St.John,CBE,Don-Bosco,Dom Warriors,Dom Spears,Dodoma Spurs pamoja na UDOM Education
Wachezahi wa timu ya UDOM-Social wakilisakama vilivyo goli la timu ya chuo cha MIPANGO.
Mchezaji wa timu ya UDOM-Social akitaka kumtoka mchezaji wa timu ya MIPANGO.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...