UN Club Chairperson at Ben Bela Secondary School, Miss Salma Khamisi Ali presenting a report about the club during school outreach in Zanzibar.
Ben Bela Secondary school students listening to presentation by outreach team.
Vikokotoni Secondary school students during school outreach to Zanzibar.
UNIC Information Officer, Stella Vuzo with Ben Bela Secondary School UN Club leaders during school outreach in Zanzibar.
Maashallah, hili vazi linapendeza sana kwa watoto wa kike awe mkubwa au mdogo na hii ndio zanzibar tunayoijuwa sisi na inavyotakiwa hasa mwenyezi mungu awazidishie na muliendeleze hili vazi kwani ndio ID CARD YETU ZANZIBAR na sio chengine
ReplyDeleteVazi limewapendeza mno watoto wa skuli na hili vazi la heshima ndilo linalotakiwa
ReplyDeletemungu awape wepesi mulienzi vazi hili na kizazi kijacho,
zanzibar itabakia na vazi lake la heshima kama mutalidumisha nyinyi kioo cha wengine
na heshima yako itabakia, unapojiheshimu wewe mwenyewe. mungu ibariki zanzibar
MAshaALLAh watoto wamependeza SANA SANA SANA ! na idumu Amani Zanzibar na MSIKUBALI KUBADILISHWA DINI KAMA WADARISALAMA!
ReplyDeleteAnkal, huyu Stella mbona ameacha mabega wazi na sehemu kubwa ya kifua. Haoni kuwa anawatia wenzie majaribuni? Na hapo anapomsogelea huyo mkaka, mh!
ReplyDeleteShule yangu Ben Bellah
ReplyDeleteMimi ni kijana wa zamani. Katika miaka ya 80 tulisoma UDSM na wanafunzi wengi kutoka Zanzibar lakini wale wa kike walikuwa wanavaa kama wale wa Darisalama! Kaswali kangu kadogo kwa wadau wa hapo juu - huu utamaduni wa vazi hili tukufu kwa wanawake wa kizenj ulianza lini? Je, kabla ya miaka ya 90 hao waliokuwa wanavaa kama waDarisalama walikuwa wakiwatia wanaume wa kizenj majaribuni? Huwa napata tabu sana kuelewa kuwafunika wanawake vichwa wakati wanaume wanaweza kutembea vifua wazi!
ReplyDeletendugu yangu wajuu hapo nitakuelewesha kidogo tu, nikuwa vazi la kujihifadhi kichwani kwa mwanamke halikuanza jana au miaka ya 80
ReplyDeleteila hili ni tokea uislamu uanze hii ni sheria kwa muislam wa kike asionekane kichwa chake wazi, na kama unavyojuwa asili ya mzanzibari ni muislam, na hao waliokuwa ukisoma nao bara sio kuwa walikuwa vichwa wazi kwamba hawajui ila hii ni kutokana na mtu mwenyewe kuamuwa ila ukweli unabakia pale pale unatakiwa uwapo muislam ufunike kichwa chako sasa hao waliokuwa wazi ni maamuzi yao binafsi
na hawa waliovaa sasa hivi ndio tukasema kuwa waendeleze kwani huu ndio mfumo wa tokea uislamu ulipoanza wakati huo mimi na wewe na mababu zetu hawajazaliwa wala hawakujuwa kuwa watazaliwa
na tunawafagilia hawa watoto hata ukiwaona wewe binafsi lazima uwapende kwani vazi limewachukuwa na ndio maana tukawataka waendeleze,ila kumbuka kuwa hili ni vazi pekee zuri kwa mwanamke wa kiislam
na hao wanaume unaosema wako vifua wazi hilo sio tatizo kabisa hilo joto la hapo linawasababisha kuwa vifua wazi hao
Nakubaliana kabisa na mdau 04:17 pm.Siyo tu huko Zenji ila TZ yote imeshakumbwa na utamaduni huu.Imekuwa ni shida sana kwa dada/mama zetu kuvaa kwa uhuru wao eti tu kwa sababu ukivaa kama dada yetu hapo kwenye picha alivyovaa basi unaoanekana "umekiuka maadili"hebu kwanza tizameni alivyopendeza na anaonekana ana heshima zake pia.Mwanamke hatathminiwi kwa kujifunikiza mwili wote,wako wengi tu wanaojifunikiza na ndani ya hiyo mifuniko kumefunikwa mambo ya kutisha küliko hata asiyejifunikiza.Sisemi hivi kwa imani ya dini yoyote la,ila jinsi ambavyo TZ imekumbwa na jambo hili bila hata kujijua.Miaka ya nyuma mama zetu walikuwa wanavaa hata nguo zilizokuwa juu ya magoti nawalikuwa na heshima zao, na watu wote TZ tulikuwa hatusumbuliwi na hili jambo, wote tuliheshimiana na kukubaliana bila kupeana majina mabaya.Leo hii ukijaribu tu hata (maofisini) au mashuleni watoto wadogo wa kike hawawezi hata kucheza vizuri kwa ajili ya kujifunga,basi kila mtu atakuangalia vibaya kukupa jina baya na kukujudge.Nakumbuka mpaka rais Alhaji Mwinyi anamaliza kipindi chake cha kutawala wanawake wote walivaa kwa uhuru na hawakubughudhiwa na mtu yeyote,ghafla tu mambo yamebadilika vibaya sana.Nafikiri wakati sasa umefika kwa sisi waTZ kuliangalia hili kwa undani,kwa nini mwanaume atembee na kaptula inayoonyesha hata makalio yake kifua wazi na isimsumbue mtu yeyote?Najua watu watasema watatiwa majaribuni swali langu:je hii miaka ya nyuma wakati dada/mama zetu walipokuwa wakivaa namna ile hawakuwatia/kututia wanaume majaribuni?au wanaume wakati ule hawakuwa na hisia?nafikiri wanaume wa sasa tumepoteza ubinadamu kwa kushindwa kutawala hisia zetu za kuwa na kiasi.Tumeruhusu tamaa zitutawale na kuwa kama WANYAMA ambao mahali popote akikutana na wa-kike basi ni lazima aridhishe hisia zake.Tubadilika na tuheshimiane kama ambavyo wa miaka michache iliyopita walivyoheshimiana na wa-kike.
ReplyDeleteNawakilisha kwa nia nzuri bila kuhusisha maswala ya dini,na sina maana ya kutembea nusu uchi.