Msemaji wa Klabu ya Simba Ezekiel Kamwaga(kushoto)akisalimiana na Meneja Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Rukia Mtingwa wakati walipofika katika viwanja vya TCC kuuaga mwili wa aliekuwa mchezaji wa klabu hiyo marehemu Patrick Mafisango na kutoa mkono wa pole wa kiasi cha shilingili 1M/-kulia ni Afisa Udhamini wa Vodacom Tanzania Ibrahim Kaude.
Meneja Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Rukia Mtingwa akimkabidhi rambirambi ya kiasi cha shilingi 1M/-mjumbe wa kamati ya utendaji na Makamu mwenyekiti wa kamati ya fedha wa klabu ya Simba Bw.Saidi Pamba,anaeshuhudia katikati ni Afisa Udhamini wa Vodacom Tanzania Ibrahim Kaude.
Meneja Mawasiliano wa Vodacom Tanzania,Rukia Mtingwa pamoja na Afisa Udhamini wa Vodacom Tanzania,Ibrahim Kaude wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliekuwa mchezaji wa klabu ya Simba,marehemu Patrick Mafisango kwenye Viwanja vya TCC,Chang'ombe jijini Dar.
Jamani huyu anayepiga picha ya mwili wa marehemu, imekaa kaaaje hii ?? je huu niutamaduni wetu ?? yaani sasa kwenye hiyo camera yake ya kiganja ,hiyo picha ya marehemu atakuwa anaiangalia kila siku ?? au ndo anaiweka kama screen server !!!! au ndo manjonjo watu waone kana kwamba ana simu ya gharama ?? maana ndugu zangu, kwenye makusanyiko ya watu ,huwa kuna mengi sana kama haya.
ReplyDeletepatrick mafisango hatasahauliwa mapema na wapenda soka kote afrika mashariki, mashabiki na wanachama wa simba hasa ukizingatia kuwa amechangia sana hadi kuifikisha timu hapa ilipofikia.
ReplyDelete