·      ¼ shilingi kwa sekunde kuanzia saa 4 usiku hadi saa 1 asubuhi kutoka Vodacom kwenda Vodacom
·      Punguzo la SMS la 45% hadi Tsh. 25 kwa SMS kwenda mtandao wowote Tanzania.
·      Kurambaza mitandao ya Facebook na Twitter bure
·     Simu za wateja wa Vodacom wa malipo ya  kabla zitajisajili moja kwa moja kwenye ofa hii

Vodacom leo imezindua ofa mpya ya kusisimua iliyoandaliwa hususan kukidhi mahitaji ya mawasiliano  ya umma wa soko la vijana ili kuendelea kukuza idadi yake ya wateja kwa kutoa huduma za mawasiliano ya simu yanaomudika kwa Watanzania wote.

Katika kampeni mpya iitwayo Wajanja wateja wa Vodacom wa malipo ya  kabla watatozwa kiwango cha chini kabisa cha robo shilingi kwa simu za Vodacom kwenda Vodacom kuanzia saa 4 usiku hadi saa 1 asubuhi. Ofa hii mpya vile vile itawatoza bei ya chini kabisa ya ujumbe mfupi ya Tsh 25 kwenda mtandao wowote Tanzania, pamoja na kurambaza tovuti ya Facebook na Twitter bure.

Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Bw. Rene Meza alisema ofa hii mpya imeandaliwa kukidhi mahitaji ya walio wengi katika soko la mawasiliano la simu za mkononi, hususan vijana- na itawawezesha kuwa  na taarifa motomoto kila wakati na kuwawezesha kuwasiliana kwa simu za sauti, ujumbe mfupi na Intaneti kwa bei wanazozimudu. Hakika vijana si vijaba tu watakaofurahia ofa hii mpya bali  wateja wote wa Vodacom wa huduma ya kulipia kabla watafaidika na huduma pamoja na viwango hivi vipya vya chini.

“ Vodacom imenuia kutoa huduma kwa bei ambazo Watanzania wote wataweza kuzimudu. Kwa kuwawezesha Watanzania kupiga simu, kutuma ujumbe mfupi na kutumia Intaneti kwa bei nafuu, tunaamini kwamba wateja wa simu za mikononi wa Tanzania sasa wataweza kuwa sehemu ya dunia ya kisasa kupitia simu zao za mkononi, “ alisema Meza.

Ofa hii haihitaji wateja wa huduma za kulipia kabla kujisajili. “ Hakuna haja ya wateja kujisajili kwenye ofa hii. Watafaidika ili mradi wako hewani kwenye mtandao wa Vodacom”, Meza alisema.

“ Tukiwa na wateja hai wapatao milioni 20, sawa na 44% ya soko la simu za viganjani, soko la Tanzania linatoa fursa kubwa ya kukua kwa biashara, fursa ambayo Vodacom inataka kushiriki kikamilifu huku tukiendelea kuongoza soko la simu za mkononi kwa kutoa huduma za bei ambazo wateja watazimudu”, Meza alimalizia.

Kuhusu Vodacom Tanzania:
Vodacom Tanzania Limited ni mtandao unaoongoza Tanzania, unaotoa huduma za mawasiliano kwa kutumia teknolojia ya kileo kabisa ya GSM.
Vodacom Tanzania ni kampuni tanzu ya Vodacom Group (Pty) Limited, South Africa, ambayo ni kampuni tanzu ya Vodafone Group UK. Vodacom Group (Pty) inamiliki asilimia 65%, asilimia 35% iliyobaki inamilikiwa na mwanahisa wa Kitanzania, One Mirambo Ltd.
Kwa maelezo zaidi tafadhali wasiliana :

Mwamvita Makamba
Ofisa Mkuu wa Mahusiano na Mauzo
kwa Wateja Wakubwa

Vodacom Tanzania Limited
SLP 2369,
Dar es Salaam, Tanzania
Simu:       +255754704265 begin_of_the_skype_highlighting            +255754704265      end_of_the_skype_highlighting
Simu ya Kiganja: +255754710865 begin_of_the_skype_highlighting            +255754710865      end_of_the_skype_highlighting





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 07, 2012

    Gharama zenu bado ziko juu sana. Halafu saa 4 usiku ni muda wa kulala...punguzeni mapema zaidi!!

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 07, 2012

    Useless offers. Saa nne ya usk wanafunzi ndio wataweza.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...