Baada ya kazi pevu ya uzinduzi wa tawi la Chadema jijini Washington Dc wabunge wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wamtembelea rasmi Balozi wa Tanzania nchini Marekani.
Balozi wa Tanzania Nchini Marekani na Mexico Mhe. Mwanaidi Sinare Maajar akipata picha ya pamoja  na Mbunge wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mhe. Peter Msigwa ndani ya Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani
Wabunge wa Chadema  Mhe. Peter Msigwa wapili kushoto, Mhe. Nassari Joshua, Al-Marufu  Dogo Janja, (Watatu kulia), ofisa wa ubalozi  Mhe. Peter Msigwa, Kaimu Balozi Mhe Lilian Munanka pamoja na viongozi wa tawi la Chadema Washington Dc wakipata picha ya pamoja na balozi  Mhe.  Mwanaidi Sinare Maajar baada ya kumtembelea rasmi siku ya Jumanne Mei 29,2012 Washington Dc Nchini Marekani.
Mbunge wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mhe. Peter  Peter Msigwa akipata picha ya pamoja na waTanzania waishio nchini Marekani, ndani ya Ubalozi wa Tanzania Washington Dc.  (Picha na swahilivilla.blogspot.com)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 30, 2012

    Mhe. balozi Mwanaidi S. Maajar, hakikisha wana Chadema wote(akiwemo Joshua Nassari) watoke Ofisi kwako Ubalozini wakiwa kila mmoja na kadi mkononi ya CCM !!!

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 30, 2012

    JAMANI MBONA ZITTO HAONEKANI KWENYE HIZI PICHA? BAADA YA KUCHANWA SANA KAONA ATOKOMEE??? YEYE AMEJIHARIBIA MWENYEWE KW AKUWA MROPOKAJI. NYOTA YAKE IMECHUKULIWA NA WAKINA MASHAKA. ILA USHAURI WANGU KWA WANACHADEMA NI KUMUOMBA JANUARY MAKAMBA NA JOHN MASHAKA WAHAME CCM WAENDE CHADEMA KWANI WAO NDIO MAWAZO MBADALA NA CHACHU YA KIZAZI KIPYA

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 30, 2012

    Vijana wa Mbowe mnapendeza ndani ya suti. Inabidi muachane na magwanda yanayowafanya muonekane kama wana mgambo.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 30, 2012

    Hahahaha Magwandazzz ukivaa Marekani unaonekana mtu wa Joseph Kony Mpiganaji wa Msituni!

    Kwa hivyo unaweza kukamatwa kimakosa ukifananishwa na Mfuasi wa LRA -Lord Resistance Army Uganda ya Joseph Kony!

    Ndio maana Chadema wakiwa Marekani wanachomoa magwanda wanayaweka ktk mabegi Airport wakifika wanavaa suti!

    Upo hapo?

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 30, 2012

    na hapo ubalozini watu wanaingia wamevaa kama wanaenda beach?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...