Taswira za Festival inayoandaliwa kila mwaka na mabalozi ya kiafrika nchini ugiriki ilianza jana 12/05 nyumbani kwa Balozi wa Afrika kusini. Festival hii ilikuwa ni ya 11.
Kwenye banda la Tanzania tuliwakilishwa rasmi na tawi la kina mama lililoandaa aina tofauti ya vyakula vya kinyumbani.
Mwimbaji wetu RICHMOND (maarufu kwa jina MICHAEL JACKSON ) kama kawaida yake alionesha umahiri wake alipopanda jukwaani kuwakilisha nyimbo za lugha ya taifa letu zilizowafanya baadhi ya wageni waliohudhuria waulizie CD zake!!!!
Kayu Ligopora
Katibu wa Jumuiya ya watanzania Ugiriki
hiyo njaa tunayoisikia huko ugiriki bado inawaruhusuni kwenda festival?
ReplyDeletekazi kwako you haters,here life goes on
ReplyDeletewewe, shika adabu yako, njaa iko kwenye magazeti tu na tv, otherwise mambo ndo kwanza Umangani life is usual, kutesa kama kawaida na watoto waKimanga ndo kwanza wanahusudi ngozi nyeusi. Wewe kaa huko huko uliko, hapa sasa haturuhusu wageni, maana tukitoa anuani tu kwamba uje , si ajabu ukaja na vikete tumboni na kutuharibia sifa . Nakuomba , wewe endelea kusoma magazeti .
ReplyDeleteswali: hivi ni kwanini watanzania wengi ambao hawajawahi kuishi nje ya tanzania wanapenda sana kujifanya wanajua au kuponda sana wenzao ambao wanaishi nje ya Tanzania?
ReplyDeleteWivu, chuki binafsi au wanajua sana kuhusu nje kuliko nje kwenyewe kulivyo labda, nashindwa kuelewa
ACHENI UBISHI:
ReplyDeleteUGIRIKI IMEISHA FILISIKA, MSIJIFARIJI TAFUTENI VIWANJA VINGINE NENDENI CANADA NA MAREKANI ANGALAU KUNA UNAFUU AU RUDINI NYUMBANI BONGO MJE MUANZE AKILI MPYA!
1.UMOJA WA ULAYA UMEANGALIA UWEZEKANO WA KUITOA UGIRIKI KTK UMOJA KWA KUSHINDWA KUENDESHA NCHI BAADA YA KUPEWA MIKOPO KUTOKA BANK KUU YA UMOJA WA ULAYA (ECB) MARA ZAIDI YA MBILI (2).
2.HIYO HIYO UGIRIKI EMESABABISHA RAISI ALIYEPITA WA UFARANSA NICOLAS SARKOZY AANGUKE KWENYE UCHAGUZI MWEZI JANA KUTOKANA NA MATATIZO YA KIFEDHA NA KIUCHUMI ALIYOSABABISHA KWA KUIBEBA KIUCHUMI UGIRIKI AKIWA RAISI.
3.PANA UWEZEKANO MKUBWA UGIRIKI IKAANGUKIA MIKONONI MWA MABILIONEA WA KIRUSI KWA BEI YA MKOPO,,,HUKU WABONGO MKIWA TOTORO USINGIZINI MKICHEZA FESTIVALS NA KUALIKA TARAABU NA MIPASHO YA KHADIJA KOPA NA KUJISIFU KUWA MAISHA YAPO KAMA KAWAIDA!!
4.KWA TAARIFA YENU HAKUNA MBONGO MWENYE AKILI TIMAMU ATAKAYETAFUTA KUJA HUKO UGIRIKI,,,HAKUNA SABABU YA KUTAFUTA ANUANI YA KUFIKIA HUKO UGIRIKI KAMA MTU ANAKUJA ATAFIKIA HOTELINI KWA MPANGO WAKE NA ATAMALIZA SHIDA ZAKE NA KUENDELEA NA SAFARI.
5.BORA KWENDA MSUMBIJI AU MALAWI(Malawi AMBAKO THAMANI YA FEDHA IMESHUKA JUZI ILIKUWA M.Kwacha 168 kwa US$ 1 NA SASA M.Kwacha 250 kwa US$ 1) KULIKO KUTUMIA US$ 1,000 AU ZAIDI KWENDA UGIRIKI KWA SABABU UTAJIKUTA UNAVUNA 'MABUA' !!!
Acheni kujikaza kisabuni, tatizo ni kuwa hamfuatilii Habari za Kimataifa mpo busy kwa kubeba Mabox Madukani kila kukicha!
huko hali mbaya hata picha quality inagoma!!
ReplyDeleteEhhh
ReplyDeleteUgiriki imezinduka tena?
Tulishaambiwa nchi imefilisika na watu wanatapatapa kufuatia Matatizo ya Kifedha na Kiuchumi!
Ahhh inakuwa hatuelewi,,,Mzungu (MGIRIKI-Mwenye nchi) na (EUROPEAN UNION/ EUROPEAN CENTRAL BANK/ BENKI KUU YA ULAYA) anathibitisha amefilisika Kifedha na Kiuchumi ninyi (WABONGO-Wageni) mnasema Maisha bora bado mnayo, tumwamini nani?,,,!!!
Hahahahaha,
ReplyDeleteKatibu wa Watazania Ugiriki Kayu Ligopora usituletee za Mohamed Al Sahaaf (ALIYEKUWA WAZIRI WA HABARI WA IRAQ UTAWALA WA SADDAM HUSSEIN) akiwahakikishia watu Duniani kupitia BBC kuwa Majeshi ya Marekani yapo Km 3,000 kutoka Mji Mkuu Baghdad kumbe yapo Km 3 tu!
Isije kufikia mnachungulia Kaburi ndio mtutafute Msaada, mtoe taarifa ili msaidiwe kabla!
Ndugu zenu
Toronto-Canada.
Anonymous wa Mon May 14, 08:07:00 AM 2012
ReplyDeleteDunia ni siku hizi ni Kijiji:
Watu hawajawahi kuishi nje ya nchi lakini kupitia wigo wa Kiteknolojia mawasiliano yanafanyika kuliko ilivyo kuwa zamani.
Hivyo kupata taarifa (sio za nchi moja kama Ugiriki) sema za Dnunia nzima ni kiasi cha kitu kuwa kiganjani!
'Dunia imesasambuliwa' na mtandao wa habari kuliko ilivyokuwa kabla na ndio maana unakuta mtu yupo nchi husika lakini yanayojiri nchini kwake wanafahamu zaidi waliopo nje ya hapo,,,upo hapo?
NATU WANAFUATILIA HABARI ZA KIMATAIFA KUTOKA VYANZO MBALIMBALI SEKUNDE HADI SEKUNDE, NCHI MBALIMBALI NA DUNIA INAVYOPUMUA SEKUNDE HADI SEKUNDE WATU WANASHUHUDIA!,,,upo hapo?
HII KAMWE SI DUNIA YA KUWADANGANYA WATU KAMA ZAMANI!,,,upo hapo?
Tatizo kubwa wandugu huko Majuu wapo bize ktk ubebaji wa Mabox na kuwa hawafuatilii kabisa vyombo vya habari za Dunia!
ReplyDeleteNdio maana unakuta hadi mambo yamefikia pagumu ndio watu wanazinduka.
Mfano ndugu zetu Watanzania miezi kadhaa nyuma mwanzoni mwaka huu 2012 huko Mali yalipotokea Mapinduzi ya Kijeshi wandugu zetu
walikuwa hata habari hawana wanaendelea na kuchakarika huku mambo yakiwa tete ndio wanazinduka na Taarifa kutoka Balozi za Tanzania nchi jirani ndio zinawafikia kuhusu hali halisi ilipofikia.
Sasa kwa mfano huu wa nchini Mali kuhusu hulka ya Watanzania ya sintofahamu, kuna Ubishi kuhusu hali halisi ilivyo huko Ugiriki?
Hahahaa
ReplyDeleteNiacheni nicheke, Watanzania huko Ugiriki uwezo wa kumwalika Khadija Kopa au Mzee Yusuf kwa mipasho na mkajirusha kwenye Matamasha sio kigezo cha kuwa na maisha bora!
Pana kila dalili mnajaribu kufa na tai shingoni!
Wandugu hamjawahi kuona watu wanshinda Baa kutwa wakilewa na kujirusha hadi usiku wa manane huku wana matatizo kama utitiri?
ReplyDeleteHaya ndio yanayojiri huko Umangani-Ugiriki!
Ahhhh ahhh ahhh
ReplyDeleteWewe Mwenyekiti wa Watanzania Ugiriki acha ujasiri huo mbaya na hatari!
Dalili ya neema inajificha?,
Mbona meza zinaonekana nyeupeee, wenzenu walioko kwenye neema baadhi ya Majimbo ya Marekani na Canada wana jichana utaona ktk minuso yao meza zime nona, ninyi meza zipo tupuuu,,,mfano jamaa wenzenu Roma Italia (kwenye njaa kama hapo kwenu) majuzi wamefanya pati Sherehe Muungano, yaani utawaona huruma meza zina chupa mbili (2) kubwa za maji ya kunywa na Chupa moja (1) kubwa tupu ya Soda!!!,,,hakuna vyakula,vitafunio wala vinywaji!!!,,,ama kweli Mtikisiko wa Kifedha na Kiuchumi umepiga sana Ulaya zaidi kuliko kwingine,,,!
Nchi ya Ugiriki inapumulia mashine wewe unasema maisha yapo,,ebo?
Watanzania Ugiriki:
ReplyDeleteMtofautishe kati ya vitu viwili (2) hapa chini:
1.Macro ecomonic (Uchumi wa Jamii nzima) na 2.Micro economic (Uchumi wa mtu binafsi/ yaani mtu hadi mtu)
Sasa basi,
-Uwezo wa wewe na familia yako hapo Ugiriki kumudu kupata 'dona' na 'mbaazi' kwa kupitia ujanja ujanja wako kuganga njaa na Usanii sio 'KIGEZO CHA HALI BORA YA KIUCHUMI YA NCHI NZIMA YA UGIRIKI!'
-Kumwalika Khadija Kopa au Mzee Yusuf kuja kuwaliwaza kwa Mipasho na Taarabu huko sio kigezo za maisha bora!
-Mnaweza cheza mduara huku njaa ziko mifukoni huku Hali halisi ya Jamii nzima ikiwa tete, ni siri yenu au mnaweza msijue kwa vile inaonekana kabisa hamna uelewa na weledi wa Tasnia ya Uchumi.
NADHANI MMEELEWA HICHO KISOMO?
Kwa sasa,
ReplyDeleteNi bora kuwepo Malawi au Msumbiji kuliko kuwepo Ugiriki!
Achilia mbali meza kuwa tupu!
Ninyi hata fulana zenu mlizovaa inaonekana zimepaukaaa, hazifuliwi kwa mashine mnafua kwa mikono Usiku na kuzirudisha mwilini asubuhi 'kauka nikuvae'
Halafu ohhh tunapeta kimaisha Ugiriki!
NJAA HAINA UBAUNSA!
ReplyDeleteHaya ni maneno yameandikwa ktk Chota matope la matairi ya nyuma la basi moja aina ya Toyota-DCM linalofanya huduma za abiria kati ya MBAGALA RANGI 3 hadi MWENGE.
Ni maneno yenye maana kama yakizingatiwa.
Mtu mzima ameumbiwa hekima na suala linajidhihirisha kwa macho, kwa meza zinavyoonekana hapo Athens kwenye hafla /sherehe zikiwa tupuuu, pana dalili hapo!
Inaeleweka kuwa Mtikisiko wa Kifedha na Kiuchumi unaendelea kuunguruma Dunia nzima.
Wandugu majuu inaonekana kabisa kengele imelia na njaa ni kali huko Majuu na hasa Ulaya kama vipi tuwatumie kutoka nyumbani Bongo vigunia vya mihogo mibichi, mahindi na maharage ili mpoze makali ya njaa,,,ni kama maneno ya basi hapo juu yanasema 'NJAA HAINA UBAUNSA'!
Huwezi kamwe kutoa taarifa za upotoshaji kwa wigo mpana wa mawasiliano Duniani uliopo kwa zama zetu hizi.
ReplyDeleteWatu wanasoma 'World reports' kutoka vianzo mbali mbali vya habari Duniani liacha ya mambo au habari nyingi kuratibiwa na kupotoshwa pia.
Lakini kwa asilimia kubwa watu wanafanya ulinganishi kulingana na vyanzo mbali mbali vya habari na wanapata ufasaha wa mambo.
HUWEZI KUPOTOSHA KWA SASA KWA KUKATAA UKWELI YA KUWA UGIRIKI IMEKWISHA FILISIKA!
Huwezi kamwe kutoa taarifa za upotoshaji kwa wigo mpana wa mawasiliano Duniani uliopo kwa zama zetu hizi.
ReplyDeleteWatu wanasoma 'World reports' kutoka vianzo mbali mbali vya habari Duniani liacha ya mambo au habari nyingi kuratibiwa na kupotoshwa pia.
Lakini kwa asilimia kubwa watu wanafanya ulinganishi kulingana na vyanzo mbali mbali vya habari na wanapata ufasaha wa mambo.
HUWEZI KUPOTOSHA KWA SASA KWA KUKATAA UKWELI YA KUWA UGIRIKI IMEKWISHA FILISIKA!
Dunia kwa sasa.
ReplyDeleteIpo kama Choo cha 'Passport size' ambavyo haviezekwi kwa mabati vipo wazi juu, yaani ile aina ya vyoo vyetu vya nyumba za Kiswahili ziwe ambazo nyumba bado zingali zinajengwa au makazi kamili.
Sasa anayeingia kwa kujisaidia au kuoga anaonekana kichwani na kama mtu akipanda mahala pa juu kidogo anaweza kupiga 'chabo' kiaina akaona kila kitu mtu alivyo mzima mzima!.
Kila unachokifanya nchini kwako au kinachotokea usifikiri ni siri Dunia nzima inashuhudia tena zaidi kuliko wewe mwenyewe, eleweni hivyo!
Kwa hivyo Dunia ya sasa huwezi kuongopa ipo wazi ni kama Choo cha Pasipoti size!
Watu wanafuatilia taarifa kutoka ktk vyanzo nyeti sana vya mambo ya Dunia nzima achilia mbali hiyo Ugiriki.
ReplyDeletePana vyanzo kama hivi, IMF, WORLD BANK, UN na Taasisi zake, WTO, WTC na mashirikisho kibao tu ya Kidunia.
Pana vitu kama STOCK EXCHANGES ZA DUNIA NZIMA,BENKI KUU ZA DUNIA NZIMA NA MAENEO, NASDAQ, DOW JONES, FEDERAL RESERVES, WALL STREET na kadhalika.
Watu wanapata 'Forecast' yaani utabiri wa yatakayojiri kabla ya mambo kutokea,,mpo hapo?
Watu wanafuatilia 'World Economic review and fore casts' ambazo zinatiririka ktk vyanzo vya habari kutoka dakika hadi dakika sekunde hadi sekunde!
Ulaya itafedheheka sana!
ReplyDeleteMfano miwili ya fedheha:
1.Ugiriki ikitengwa kutoka Umoja wa Ulaya itabidi iangukie kwa ndugu zao 'Wamanga' wenzao asilia Umoja wa Mataifa ya Kiarabu (Ni vigumu kuendesha mambo kama nchi ukiwa mpweke)
2.Umoja wa Ulaya wamekuwa wakiwatenga na kuwakwamisha ndugu zao wa karibu Kijiografia (isipokuwa Kiimani) Uturuki na sasa inadhihirika wazi ya kuwa ndio inayostahili zaidi kuwepo ktk Umoja wa Ulaya zaidi ya hiyo Ugiriki waliyoibeba mno, huku Uturuki waliyokuwa wakiibeza na kuitenga sana kwa miaka mingi tu.
HII DUNIA KILA MUDA UNAVYOKWENDA WATU SEHEMU MBALIMBALI HASA MADHALIMU WANAKUWA WAKIUMBUKA NA MATOKEO HALISI YANAYOJIRI DUNIANI!
Ugiriki,
ReplyDeleteMumeanguka kifedha na kiuchumi, kamwe hamuwezi kujitetea kwa kutumia 'pose'/ mikao ya kupiga picha!
Mseme uwazi kwa kuwa hivi sasa Serikali yetu makini ,imekuwa sikivu, inajituma ili kuwafikia Wana Diaspora mbalimbali Duniani(wanaoishi Ughaibuni).
Mfano Marekani wamepelekewa mipango kabambe ya kuwawezesha kujijenga nyumbani kwa akiba na kujenga nyumba, Ubalozi wa Tanzania Marekani uliopo Washington DC umeanzia mipango hii ktk sehemu ya Maryland.
Hivyo ni muhimu muwe wawazi ili nanyi mfikiwe na iwe ni faida kwa nchi badala ya kizudi kupoteza muda buree.
Hahahaha!!!
ReplyDeleteDunia ipo kama 'Choo cha Pasipoti size'
Ina maana mtu akitoa upepo (akija..a) Ugiriki huku Bongo tunasikia?
Ama kweli Dakitari umetuchambulia!!