Baadhi ya waandishi wa habari mkoani Ruvuma,Joseph Mwambije wa kwanza kushoto Kassian Nyandindi wa kulia na Andrew Chatwanga wa pili kutoka kulia wakimsikiliza meneja wa kituo cha maabara katika hospitli ya mkoa wa Songea Anusiata Nyoni jana, kwa ajili ya zoezi la kutoa damu wakati wa siku ya uhuru wa vyombo vya habari Duniani kwa lengo la kuwasaidia watu wenye uhitaji.
Mwandishi wa habari wa gazeti la majira kituo cha mbinga mkoani Ruvuma,Kassian Nyandindi akitoa damu katika hospitali ya mkoa wa Songea ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari Duniani.
Mwandishi wa habari mkoani Ruvuma Joaseph Mwambije akitoa damu jana katika hospitali ya mkoa Ruvuma wakati wa siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani ambapo waandishi wa mkoa huo walifanya usafi katika maeneo mbalimbali pamoja na kuchangia damu kwa watu wenye uhitaji.
Katibu wa chama cha waandishi wa habari mkoani Ruvuma Andrew Chatwanga akitoa damu katika hospitali ya mkoa Songea ikiwa ni moja mambo muhimu katika kuadhimisha siku ya uhuru wa vyombo vya habari Duniani.PICHA NA DENIS CHALE - GLOBU YA JAMII.


.jpg)
.jpg)


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...