ZAIDI ya wanaume 6, 500 waliokuwa wakiishi bila kutahiriwa katika Wilaya za Nzega na Igunga mkoani Tabora, sasa wametahiriwa chini ya mpango maalumu unaolenga katika kupunguza maambukizi ya virusi vya Ukimwi.

Meneja wa Shirika lisilokuwa la Kiserikali la JHPIEGO Tanzania, Tawi la Mkoa wa Tabora, Simyoni Nyandenda, alisema hayo ni mafanikio makubwa mno katika utoaji wa huduma hizo mkoani humo.

Kwa mujibu wa Nyandenda, Mkoa wa Tabora, una vituo vinne vinavyotoa huduma za bure za kutahiri wanaume wanaoishi bila kutahiriwa.

Katika Wilaya ya Nzega, vituo hivyo viko katika hospitali ya wilaya na Hospital ya Missioni ya Ndala, wakati katika Wilaya ya Igunga, vituo viko katika Hospitali ya Igulubi na hospitali ya wilaya.

Alisema idadi hiyo ya watu waliotahiriwa, imevuka malengo ya shirika lake na Hospitali ya Mkoa wa Tabora, ya kuwafanyia tohara wanaume 5,000 katika kipindi cha wiki tatu.

Meneja huyo alisema zoezi hilo katika wilaya hizo, limesukumwa na kasi kubwa ya maambukizi ya virusi miongoni mwa wananchi.

Alisema takwimu zinaonyesha kuwa maambukizi ya virusi katika wilaya hizo mbili za Mkoa wa Tabora, sasa yamefikia asilimia 6.4, kiwango ambacho alisema ni kikubwa.

Nyandenda alisema kasi ya maambukizi katika wilaya ya Nzega, inachangiwa na mwingiliano mkubwa wa watu unatokana na migodi na mji kuwa katika njia panda.

Alisema kwa upande wake, Wilaya ya Igunga, maambukizi yanachangiwa na mji kuwa barabarani na wimbi kubwa la wachimbaji wadogo wadogo wa madini.

Alisema watu ambao hawajatahiriwa, wako katika hatari kubwa ya kuambukizwa virusi vya Ukimwi, ikilinganishwa na waliotahiriwa.

Alitoa wito kwa wanawake, kuwahimiza wanaume ili waende wakapate huduma hizo, ili pamoja na mambo mengine, kuwawezesha wanawake kuepuka kupata kansa ya shingo ya uzazi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 06, 2012

    UKIMWI ni ugonjwa hatari..tunahitaji kuwa wawazi kweli kuweza kupambana nao.'Waliotahiriwa wana nafasi ndogo ya kupata maambukizi kuliko ambao hawajatahiriwa'-Kivipi?Sababu za kisayansi zinasemaje?Madaktari mnaotembelea blog ya jamii mwaweza kusaidia hapa katika kuelimisha japo kidogo.

    David V

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 06, 2012

    Mdau wa kwanza kutoa maoni, naweza kukujibu kama ifuatavyo. Kwa kuwa mm ni daktari, sitatafuna maneno ili uweze kuelewa. Kwa mfano ikiwa govi limebana sana kwenye tundu la kukojolea inaongeza 'local irritation or infection' kwenye uume (sijui nisemeje kwa Kiswahili). Bacteria wanajikusanya kwenye ngozi ya ndani ya govi ambayo huwa laini sana na kuidhuru.

    Sasa wakati wa kujamiiana, ni rahisi ngozi hiyo iliyokwishaharibiwa na bakteria kuchubuka, na hivyo kusababisha kupokea VIRUSI kutoka kwa mwanamke. Ieleweke kuwa KUMA ya mwanamke mara nyingi huwa inashambuliwa na bakteria. Kwa hiyo kwa mwanamke ni rahisi sana kwa VIRUSI kuwa ndani ya majimaji ya kumani.

    Kadhalika nyama ya uboo uliotahiliwa ni ngumu. Hivyo, si rahisi kupata mchubuko kama ile ambayo haijatahiliwa.

    Na: Daktari wa Magonjwa ya Zinaa

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 06, 2012

    ashakum si matusi

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 06, 2012

    Ooh my God, kuchafua lugha maana yake ni nini? mbona mdau hapo juu hajazuiwa au ndo kumomonyoka kwa maadali? I think hii blog hata watoto wanafungua so let us be careful for what we are writting about.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 06, 2012

    Mbona hapa nimeachwa njia panda mimi. Ashakum si matusi ndiyo nini?

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 06, 2012

    Hive daktari pamoja na kuomba radhi hawezi kusema sehemu ya siri ama utupu wa mwanamke na akaeleweka bila kutumia lugha alotumia?

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 06, 2012

    kweli wakati wa Uwazi na ukweli , lakini uliyejitambulisha Dr umechemsha kimaadili kwani hii blong inasomwa na rika za aina tofauti. Ungalitumia uuke au uume ingalitosha.

    Hatahivyo, hongera kwa ujasiri wako hadharani.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 06, 2012

    Hii kali sana. Namshukuru sana, daktari katoa maelezo mazuri sana. Lakini tatizo kayatoa kidarasa darasa zaidi. Maana 'darasani' ni vizuri kutaja viungo vya binadamu kama inavyotakiwa, bila kuficha ficha ili kufikisha taaluma kwa walengwa kirahisi.

    Kitu kingine, sijui viungo hivyo vya binadamu vikitajwa kwa Kiswahili inaonekana ni ukiukwaji wa maadili? Maana kwa kiingereza huwa vinatajwa tu na kuandikwa bila kificho, iwe magazetini au kwenye mtandao.

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 07, 2012

    kelele za nini, message sent!

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 07, 2012

    Asante sana Dr.

    Jamani kwanini tunapenda kuficha ficha ili hali UGONJWA NI HATARI, umetuondolea ndugu zetu wengi na kutuachia yatima kibao, na wengine wanaokunywa dawa za VVU bila hatia.

    Mungu wangu, watoto gani hao mnaowatetea! Yaani watoto wa siku hizi wanajua kila kitu mpaka watoto wanapatikanaje hawadanganyiki NG'O kama sie zamani kuwa watoto wananunuliwa dukani!

    Safi sana Dr., hata mie nitakuwa nitahimiza ndugu zetu wakatahiriwe. Naomba mnisaidie tu kwa kanda ya Coast mnapatikana hospitali zipi?

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 07, 2012

    Hongera Dr. kwa kusasambua kila kitu hadharani.

    Ni wazi kuwa Mwanaume ambaye bado anao 'mzigo' wake kibindoni, yaani ile ngozi (govi) inapoishia na kuanza kwa nyama kwa ndani panakuwa ni laini sana hivyo kama utalifungua 'govi' kwa nguvu utaona panatokea kama wekundu au muchubuko,,,Hiyo ni hali ya kawaida sembuse itokee msuguano kama unaotokea ktk tendo unafikiri kiwango cha athari kitakuwa vipi?

    Na hii ndio inakuwa rahisi 'Virusi' kujipenyeza!.

    Hivyo Dr. anazungumzia ktk hoja hiyo.
    Kumbukeni kuwa:

    1.Mficha maradhi kilio humuumbua,
    2.Mficha uchi hazai,
    3.Mvuka mto lazima kuyakoga maji

    Mpo hapo?

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 07, 2012

    Enhee hili balaa sasa!.

    Ktk zama hizi mtu bado anastahimili kuishi na Govi?

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 07, 2012

    Huyu daktari ana akili sana. Hapa kaweza kufikisha ujumbe vizuri. Unajua sisi watanzania Kiswahili chetu huwa ni kigumu kueleweka kwa wageni sababu ya kutafuna tafuna maneno.

    Kuna siku Mkenya alikuwa akisoma habari za Kiswahili toka IPP Media, alikuwa akinihoji sana maana ya maneno mengi, na nilipokuwa nampa Kiingereza chake, ananiambia kwa nini hawakusema hivi (anataja neno la Kiswahili) ambalo mwandishi alilikwepa kwa makusudi. Kisa eti ni maadili mazuri. Big up doctor. Kwa kweli nimeelimika.

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 08, 2012

    Ahhh Jamani 'zoba' mzigo, tuwahimize wenzetu wamwone Dakitari ili wasije wakatuchafulia!

    Maana alipopita mwenye 'zoba' mnafikiri itakuwa vipi ikifika zamu ya Muungwana kupita hapo halafu akaambiwa mtangulizi wako alikuwa nao mzigo?

    Si ni kuwa Mahusiano au Ndoa itavunjika?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...